Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Katekesi siku ya Jumatano

Ukishiriki na watu waliobaguliwa wewe ni chombo cha faraja!

Barua ya kwanza ya Mtume Petro ina uwezo mkubwa wa kutoa faraja na amani, ili kufanya utambue ni jinsi gani Bwana yuko karibu nasi, na hatuachi kamwe, na zaidi hasa katika kipindi kigumu cha maisha yetu - ANSA

05/04/2017 17:00

Ndugu mnapaswa kuwa na moyo mmoja, na fikira moja; mnapaswa kupendana kidugu, kuwa wapole na wanyenyekevu ninyi kwa ninyi. 9 Msiwalipe watu ovu kwa ovu, au tusi kwa tusi; bali watakieni baraka, maana ninyi mliitwa na Mungu mpate kupokea baraka. ? 14 Lakini, hata kama itawapasa kuteseka kwa sababu ya kutenda mema,basi, mna heri. Msimwogope mtu yeyote, wala msikubali kutiwa katika wasiwasi. 15 Lakini mtukuzeni Kristo kama Bwana mioyoni mwenu. Muwe tayari kumjibu yeyote atakayewaulizeni juu ya matumaini yaliyo ndani yenu,( 1Pt 3,8-9.14-15).

Katika barua ya kwanza ya Mtume Petro, yenyewe ina uwezo mkubwa wa kutoa faraja  na amani, ili kufanya utambue ni jinsi gani Bwana yuko karibu nasi,hatuachi kamwe,zaidi hasa katika kipindi kigumu cha maisha yetu.Lakini ni siri gani iliyomo katika  barua hii kwa namna ya pekee sehemu iliyosomwa (1 Pt 3,8-17)?. Hayo ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa katekesi yake ya kila Jumatano katika viwanja vya Mtakatifu Petro tarehe 5 Aprili 2017.Baba Mtakatifu akichambua barua ya kwanza ya  Mtume  Petro amesema;Hawali ya yote siri ni kwamba maandishi hayo yana msingi wa mizizi yake moja kwa moja kutokana na  Pasaka, katika moyo na  matendo yanayofanyika kwa wakati huu na ili kuweza  kutambua  jinsi ya mwanga na furaha ambayo inatokana na kifo na ufufuko wa Kristo.Bwana amefufuka kweli kweli na anaishi na kila mmoja. Hiyo ni salamu nzuri ya kupeana wakati wa Pasaka , “Bwana amefufuka kweli kweli kafufuka; kama jinsi watu wengi duniani utakiana  matashi mema ya Pasaka.Wanakumbuka Kristo amefufuka na yuko hai kati yetu.

Ndiyo maana Mtakatifu Petro anatualika kwa nguvu zote kumwabudu katika mioyo yetu .Siyo simu ya mkono, na wala mrundiko wa utajiri:hapana bali matumaini yetu ni Yeye,ni Bwana Yesu tunaye mfahamu aliye mzima, yupo sasa kati yetu na katika ndugu zetu , kwasababu amefufuka.Baba Mtakatifu Francisko ametoa mfano wa salam za watu wa Mungu katika nchi za Ulaya ya Mashariki kwamba wamezoea kusalimiana habari za asubuhi na jioni kwa pamoja na kipindi cha pasaka ni  "Bwana amefufuka".Anathibitisha kwamba ni watu wenye furaha kubwa kwasababu ni Yesu Mfufuka anayetupatia asubuhi na Jioni. 

Pili kwa njia hiyo tunaweza kutambua matumaini haya ambayo hayatokani na sababu za kinadharia au kwa maneno tu, zaidi ni kwa njia ya matumaini  ya maisha; hiyo ni kwa upande wa ndani ya jumuiya ya kikrsto na  nje yake.Kama Kristo alivyo mzima kwa maana ya kuishi ndani ya  mioyo yetu, tunapaswa kuacha nafasi  aonekane ndani na nje yetu .Ina maana ya kwamba lazima Bwana Yesu daima azidi kuwa mfano wa maisha ambayo tunapaswa kujifunza , namna ya kuishi kama yeye alivyoishi. Matumaini yaliyomo ndani mwetu hayawezi kubaki yamefichika ndani ya mioyo yetu.

Kama  isomekavyo kwenye zaburi ya 33 aliyoitumia Mtakatifu Petro  lazima itutoe katika vifungo na kutoka  nje tukiwa tumekuwa mfano mpya usiyolezeka wenye upole,heshima na wema kwa wengine , kiasi cha kufikia kusamehe hata wale walio tutendea vibaya.  Ametoa mfano kwamba mtu asiye na matumaini hawezi kusamehe na kutoa faraja ya msamaha na wala kupata faraha ya kusamehewa. Lakini Hayo ndiyo matendo aliyo fanya Yesu na anazidi kuendelea kutenda  hivyo kwa kupita wale wanao acha nafasi katika mioyo na katika maisha yao. Kwa utambuzi kwamba ubaya haushindi kwa kwa ubaya bali kwa ni kwa njia ya unyenyekevu, huruma na umasikini wa roho. Ametoa mfano wa mafia wanafikiri kwamba ili kushinda ubaya ni kwa njia ya kufanya vibaya, na kwa njia hiyo hufanya kulipiza visasi  na kufanya mambo mengi tunayotambua.Lakini hao hawatambui nini maana ya unyenyekevu, huruma, upole wa mioyo je ni kwanini hawa vikundi vya mafia hawa matumaini. Mfikirieni ninyi. 

Njia ya tatu baba Mtaktifu Francisko ameeleza, Mtakatifu Petro amesisitiza kwamba  ni afadhali kuteseka kwa sababu ya kutenda mema, kama Mungu akipenda, kuliko kuteseka kwa sababu ya kutenda uovu. Hiyo haina maana ya kusema kwamba ni afadhali kuteseka , bali tunaposteseka kwa ajili ya wema, tunashiriki na Bwana ambaye alikubali kuteseka , na kutundikwa msalabani kwa ajili ya ukombozi.
Tunapokubali hata sisi hali ndogo  au  kubwa katika maisha yetu, tunakubali kuteseka kwa ajili ya wema, ni kama vile unapanda mbegu ya kukuzunguka ya ufufuo na maisha , ambayo inaangaza katika giza nene kwa mwanga wa Pasaka. Ndiyo maana ya mtume Petro anatualika tuwatakieni baraka, maana sisi tumeitwa  na Mungu tupate kupokea baraka. Baba Mtakatifu anaongeza kusema, baraka siyo kama ishara ya kufanya utafadhali, bali baraka ni zawadi kubwa ambayo sisi wenyewe tumekuwa  wa kwanza kuipokea  na ambayo sisi tuna uwezo wa kuwashirikisha ndugu. Huo ni ujumbe wa  upendo na upendo wa dhati usiopimika ambao hauna kikomo,  ni msìngi wa kweli wa ukombozi wetu.

Baba Mtakatifu Francisko memaliza katekesi yake akisisitizia zaidi juu ya yote aliyo tafakari akisema  ndipo tunaweza kutambua Mtume Petro amekuwa na maana gani kusema heri  hata kama itawapasa kuteseka kwa sababu ya kutenda mema, maana ni nani atakayeweza kuwadhuru ninyi kama mkizingatia kutenda mema?. Amefafanua kwamba siyo  sababu tu ya kimaadili au mambo ya utauwa, bali ni kwasababu mara tu tunaposhiriki katika ya watu wa mwisho na kubaguliwa,au hatujibu ubaya kwa ubaya bali kusamehe na kutoa baraka,sisi tunaangaza kama ishara hai inayoang’aa na matumaini, na pia kuwa chombo cha faraja na amani kutoka katika moyo wa Mungu.Baba Mtakatifu Francisko ametawka wpt waendelee mbele kwa ukarimu, upole wa moyo , kuwa mpendeka na kuana wema hata kwa wale wasio tutakia mema , au kutafanya vibaya.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

05/04/2017 17:00