2017-03-30 16:57:00

Wakristo wawe wajasiri na uwezo wa kukemea umasikini na ubaguzi


Namna gani ya kuendeleza kutoa ushuhuda wa kiekumeni katika  Makanisa kwa kuhamasisha utunzaji wa mazingira katika maisha ya kila siku kwenye Jumuiya mahalia. Hayo ni baadhi ya majibu yaliyotolewa hivi karibuni huko Bangalore nchini India , katika Mkutano ulio andaliwa na kituo cha Kikristo cha kiekumeni(Ecc) kwa ushirikiano wa kamati kuhusu imani ya kiinjili .Maelezo hayo yanatoka katika Gazeti la Osservatore Romano yakieleza ,lengo la mkutano huo kwamba , umekuwa kutazama na kuhakiki umuhimu wa kuona nafasi ya wakristo wa kihindi pamoja na kwamba ni wachache katika eneo hilo na wakati mwingine wanabaguliwa, kama vilehata  wabatizwa wanaoishi nchini India. 

Kituo cha kiekumeni cha Wakristo wanalazimika kufanya kazi katika Jamii ya india ili kuonesha njia ya kuheshimu maisha ya viumbe, kwa kufikiria kwamba ni zawadi ambayo imekabidhiwa dunia iitunze na kuilinda na siyo mali ya kutumiwa bila kifikiria ya kesho. Kwa njia hiyo mjini Bangalore katika mkutano wa siku tatu, umewapa fursa ya kubadilishana uzoefu wa hali halisi ya  wakristo wa India wanavyoishi ,na kujaribu  kutafu mbinu za kuweza kusaidia ili kuondokana na umasikini, ukosefu wa haki ambao unasababisha hali ya kubaguliwa kwa watu na hasa kwa upande wa wanawake .
Kutokana na kushirikisha na uzoefu wa mateso ya kubaguliwa kwa wanawake, imebainika ni jinsi gani wanatumika  katika sehemu kadhaa za kazi bila malipo na mara nyingi wanaishi katika umasikini ulio kithiri kiasi cha kutokuona hata ufinyu wa   kuondokana na hali hii, pamoja na kwamba ipo mipango na miradi iliyo anzishwa na Makanisa.

Aidha katika Mkutano huo Bangalore wamezungumzia na kuhimiza zaidi juhudi hizi zilizoanzishwa kwa ushirikiano wa kiekumeni  pia mpendekezo ya kuwa na mahusiano ya moja kwa moja na taasisi za kisiasa na kuwahusisha hata dini nyingine. Aidha katika siku tatu, wameweza kunukuu dhamira kuu ya Baba Mtakatifu Francisko kwenye  Waraka wake wa Sifa kwa Mungu wakisisitiza zaidi ya kujibidisha katika kazi ya ulizni wa mazingira ambayo ni kazi ya uumbaji , ikiwa na maana ya kuhamasisha na kukuza mipango ya mafunzo yaliyo wazi kwa wato wote , bila kuwa na utofauti wa jinsia, tabaka. Kwa Wakristo wamewahimiza kwamba ni  lazima kutoa mchango wao halisi wa ujenzi wa  jammi yenye ujasiri na uwezo wa kukemea umasikini na kubaguliwa,kwa kujaribu kukuza maendeleo ya kiuchumi ambayo uhusisha kila mtu.
Na mwisho wa mkutano  katika Kituo cha Kiekumeni cha Kikristo, wameamua kutoa wito kwamba wakristo wote wanapaswa kuwa mashuhuda wa misingi ya kiekumeni, ambayo inasizingatia haki, ujenzi wa amani na kufundisha uadilifu wa viumbe .

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.