2017-03-28 14:23:00

WHO:Kampeni ya chanjo ya Polio kwa watoto katika nchi 13 za Afrika


Ni zaidi ya watu wa kujitolea 190,000 watatoa chanjo ya polie kwa  watoto milioni 116 katika nchi 13 za Afrika kwa wakati mmoja. Lengo ni kujaribu kuzuia ugonjwa huo unaozidi kuzuka katika bara hilo. Kampeni hii imetangazwa na Shirika la Afya Dunia WHO . Chanjo hiyo itatolewa kwa watoto chini ya miaka 5 katika nchi za Benin, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Ivory Coast, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Guinea, Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Nigeria na Sierra Leone.

Zoezi la kutoa chanjo litafanyika kwa kutembelea nyumba kwa nyumba katika miji yote na vijiji kwa kufanya kazi masaa 12 kila siku. Watu hao wa kujitolea watasafiri kwa miguu , au baiskeri , wakiwa na mifuko maalum ya kutunza chanjo ikiwa na baridi ya nyuzi 8. Taarifa inasema mwisho wa mwezi Agosti mwaka jana watoto wanne wamepooza na polio katoka katika maeneo yote yenye matatizo ya usalama , kama vile Borno nchini Nigeria. Ingawa eneo  hilo liko mipakani lakini virusi vinaweza kuenea kwa urahisi katika maeneo yasiyo ya ulinzi kama vile nchi za jirani,na hivyo ni onyo kutoka kwa wataalam.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.