2017-03-28 15:13:00

Wafanyakazi 6 wa Umoja wa Mataifa huko Juba kuuwawa


Janga jipya katika nchi  ya Sudan ya Kusini limetokea kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambapo kwa miaka hii ya karibuni wameshambulia na njaa kali.Wafanyakazi 6 wa Umoja wa mataifa wakiwemo wakenya 3 na raia mahalia 3 waliuawa katika shambulizi wakiwa safari ya kutoka mji mji Mkuu Juba kuelekea mji wa wa Pibor mashariki wakipeleka msaada .Gari walio kuwa wakisafiria la Umoja wa Mataifa  lilisimamishwa na kuzingirwa na kundi la watu wenye silaha .Watu hao 6 walilazimishwa kutoka ndani ya gari na kuuwawa papo hapo.Nchi ya Sudan ya Kusini ni moja ya nchi changa katika dunia ambapo imeundwa tangu tarehe 9 Julai 2011, na yenye utajiri wa mafuta ,lakini ikiwa na ukosefu wa bahari ya kuweza kuweka bandari , kwa miaka hii imekuwa ni uwanja wa migogoro ya makabila kati ya makundi hasimu ambayo inawazuia watu wa kujitolea kuingia katika maeneo yaliyo athirika na njaa na kuiba misaada ya raia hao.

Katika nchi kuna watu milioni 2.5 waliyo songamana kutokana na kukimbia makazi yao kwasababu ya vita na ukame. Hadi sasa walio athirika ni watu 100.000 na milioni moja ya watu wako  katika hatari ya njaa.Nchi ya Sudani ya Kusini  ilipambana kwa miaka mingi ili kuweza kupata uhuru, lakini baada ya kufikia lengo , taifa imejikuta kwa upya na mgawanyiko wa vita vya kikabila kati ya wafuasi wa Rais Kiir na wale wa  rais aliyepita Machar.
Hata hivyo habari kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibindamu, OCHA imekaribisha hatua ya serikali ya Sudan ya kufungua njia mpya na salama kwa ajili ya kupitisha misaada ya kibinadamu, hatua ambayo itaokoa maisha ya watu hao  wanaokumbwa na njaa kali nchini Sudan Kusini.

Barabara hiyo ya urefu wa kilometa 500 yenye kuanzia El Obeid katikati mwa Sudan hadi Bentiu,Sudan Kusini itawezesha Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP kufikisha tani 11,000 ya chakula wiki hii, kiasi ambacho kitatosheleza lishe ya miezi mitatu kwa watu 300,000 nchini humo.
Shirika hilo limesema hatua hiyo ni muhimu wakati huu kabla mvua hazijaanza mwezi Mei na inadhihirisha ushirikiano wa Sudan na nchi hiyo pamoja na jumuiya ya kimataifa katika kuzuia janga la njaa ambalo linaweza kuathiri watu wengine milioni moja.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.