2017-03-27 15:34:00

Maaskofu wa Peru kutoa wito wa msaada wa waathirika wa mafuriko


Hivi karibuni Baraza la maaskofu nchini Peru (CEP)wametoa wito kwa watu wote kujibidisha zaidi katika kufanya matendo ya upendo hai kwa ajili ya wale ambao wamepoteza kila kitu kutokana na mvua kubwailiyosababisha  maporomoko ya ardhi na mafuriko nchini.Ni karibia mia ya watu wamepoteza maisha yao na zaidi ya maelfu kubaki wameathirika kulingana na ripoti ya karibuni ya uendeshaji wa dharura kitaifa.
Maaskofu wa Peru wanasema kwamba hata kama wanaishi masaa ya mateso wasiwasi na maumivu , lakini kuna mshikamo . Siyo kipindi cha kuwa na hofu ni muda wa kuwa na imani katika Mungu mpaji ambaye anawajali kila mmoja kama vile Baba mwenye upendo.Ni kipindi cha kufanya maombi , ni kipindi cha kufanya mshikamano kama wanavyo onesha watu  na siyo muda wa kutafuta makosa , bali ni wakati wa kuunganisha nguvu za pamoja.

Maaskofu pia wanawaalika waathirika wasadiane wao kwa wao kwa  kutoa kipaumbele kwa wote na zaidi walio katika mazingira magumu, kama vile watoto ,wazee na wanawake wajawazito wakati wa usambazaji wa misaada.Halikadhalika wanaalika wale ambao wanaendelea kuteseka na gadhabu ya asili , kuendelea na ujasiri , kama vile Mama Maria mbele ya Msalaba wa Yesu kwani wanasema hali ya kipindi kama hiki kitapita na kurudia hali iliyo bora.Wamesisitiza kuwa wataendelea kuwa karibu nao kwa maombi , upendo na msaada kwa kupitia parokia na Caritas Jimbo. Wanatoa wito kwa wot e ambao hawakuathirika moja kwa moja na nguvu ya sili wawe wakarimu, na kutoa msaada wao, hata kama upendo huo ni matokeo ya kujitoa sadaka kuu. Na mwisho Maaskofu wanasema  hata hivyo nchi ya Peru imekuwa na mwamko wa kusaidiana  kwa sababu ni watu jasiri, na ujasiri huo unatokana na imani yao.Na Mungu Baba wa huruma awabariki na kuwapa nguvu na kuwalinda.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.