2017-03-27 14:48:00

Katika mageuzi tushinde vishawishi kusema tumezoea kufanya hivi


Kipimo cha utume wa kimisionaria, ni mojawapo ya sera za mageuzi ya vyo vya habari vya Vatican.Ni moja ya maneno yaliyotamkwa na Monsinyo Dario Edoardo Viganò, Katibu mkuu wa Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican,hivi karibuni katika tamasha moja kwenye Chuo Kikuu cha Kipapa Laterano Monsinyo Vigano, amesema kuwa katika mawasiliano ya jamii ni lazima kushinda vishawishi vya kusema “tumezoea kufanya namna hii”na kwamba kama wewe ni mwaminifu wa Injili unaweza kweli kuwa mbunifu na wazi katika kubadilika kulingana na Baba Mtakatifu Francisko asemavyo.
Pamoja na hayo amesema kuwa masafa ya Radio Vatican hayakuzimwa na kwamba usikivu na umakini kwa idara za afrika ni msingi. Ni mtu mwenye nguvu na mwaminifu wa Injili ya Kristo ,mbunifu na wazi katika mabadiliko, badala ya kujitenga na kubaki na mazoea ya kusema daima tumekuwa tukifanya hivi. Monsinyo Dario Vigano ameyasisitiza katika tamasha la ubunifu lililo andaliwa na Chuo Kikuu cha Laterano, na kuweka mkazo katika roho ya Baba Mtakatifu Francisko katika hatua ya mchakato wa mageuzi ya vyombo vya habari  Vatican.

Kwa kufafanua anasema mchakato huo siyo kwamba ni kuunda upya au wa kutengeneza zaidi, ni mabadiliko katika mtazamo kwa vile unapita. Vilevile anasema siyo rahisi sana kuratibu vyombo vya habari vinavyogawanyika katika miundo ambayo inatunza huduma ndani bila  kutazama upeo wa juu.Maana mantiki ya upeo wa juu ni yenye nia ya kuhifadhi lakiniwakati huo huo unaendeleza ili kufikia malengo.Ameongeza Monsinyo Vigano, kwa njia hiyo ni muhimu kuwekeza katika mafunzo ya wafanyakazi ambao wanatekeleza huduma ya mawasilino Vatican. Vilevile amefafanua juu ya kigezo cha utume wa kimisionari kwamba, kuna taadhari kubwa katika hali ngumu ya maisha kwenye umasikini na matatizo. hata hivyo kutokana na kutambua hali hizo za kutokuweza kutatuliwa kwasababu ya  kutamfuta mitindo iliyopita, inabidi kutafuta ufumbuzi sahihi.Halikadhalika Monsinyo Vigano ameongeza juu ya mtazamo huo wa  kupata ufumbuzi   sahihi unaoweza kupata katika taadhari ya gharama na hasa kwa kubadili gharama hizi zikawa uwekezaji , kwa njia hiyo yeye anabainisha kufanya masafa mafupi ya Vatican na hasa kuwa makini kuzingatia bara la Afrika.

Kuhusu suala hili la masafa anasema kwamba, kufikia hadi sasa masafa mafupi ya Radio Vatican hayakuzimwa kamwe, kwa maana hiyo masafa waliyo kuwa nayo Afrika yanaendelea kufika na hiyo inapaswa kuwa wazi;masafa mafupi , hayakufungwa, kwasababu umakini kwa Afrika ni msingi kiasi kwamba wako  katika machakato wa kutekeleza mradi wa Radio Fm 240 Afrika, kupitia njia ya satellite, na pia kubuni hata miradi mingine ya kuendeleza kutoa maneno ya Baba Mtakatifu Francisko. Katika suala hilo si  kutazama  masafa mafupi leo hii, bali ni kutafuta ni kwa jinsi gani tunaweza kuhakikisha ujumbe wa Baba Mtakatifu unafika barani Afrika na katika nchi zote katika maeneo mengi ambayo bado kuenea teknolojia.Akiendelea kuongea juu ya Afrika , ameongeza kwamba katika  mwelekeo huo inabidi kuwa na makubaliano na Facebook, ambapo nchi 44 zinaweza kupata kwa namna nyepesi ujumbe mfupi wa Baba Mtakatifu.

Monsinyo Vigano pia amezungumzia juu ya mwelekeo wa mawasiliano ya Baba Mtakatifu Francisko , akibainisha kuwa hakika yeye siyo mtu wa kufanya masoko na hata mtu wa kufanya mikakati ya mawasiliano, bali yeye anatoa mawasiliano kama tunavyo muona . Baba Mtakatifu Francisko kwa hakika yeye ni mtu wa watu na mtu wa watu kwa kawaidia anajua namna ya kusimamia mahusino na watu. Kwa njia  hiyo ndiyo mawasiliano ndiyo nguvu ya Baba Mtakatifu Francisko ,ni yeye mwenye anaamua ni aina gani  ya mahusiamo na mawasiliano, wala hatawaliwi na uamuzi wa sheria za itifaki. Yeye siyo picha ya mtu tu, bali ni mtu anayefanya mambo kana kwamba daima anaongozwa na Roho Mtakatifu.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.