Unjilishaji,ushemasi na pembezoni.Ni mambo muhimu ambayo Baba Mtaaktifu Francisko ameweza kuzungumza kwenye Kanisa Kuu la Jimbo kuu la Milano, Jumamosi tarehe 25 Machi 2017 wakati, akijibu maswali ya padre, shemasi na mtawa mmoja. Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa Kanisa halipaswi kuogopeshwa na changamoto hizo,kuona kwamba ni fursa za kuanza upya kutangaza Injili kwa watu wote.Anasematunarusha nyavu katika uinjilishaji ,tunapaswa kukumbuka kwamba siyo sisi tunao chukua samaki, bali ni Bwana nayevua samaki hizo.Baba Mtakatifu Francisko ametumia mfano huo kuanza kujibu maswali hayo, na hasa akimjibu Padre Gabriel Gioia juu ya changamoto za jamii iliyopanuka kwa Kanisa. Anasisitiza hawali ya yote ya kwamba changamoto kwa Kanisa daima ni chachu, kwasababu hatupaswi maana zinafanya Kanisa likue.
Hiyo ni ishara ya imani hai ya jumuiya inayoishi, ambayo inamtafuta Bwana, pia
kufanya macho yabaki wazi.Tunapaswa kuogopa hawali ya yote imani isiyo na changamoto,
ambayo ni kujisiki kwamba umetosheka,kutokuhitaji lolote ,kila kitu kimefanyika, Hiyo
siyo imani na haitajiki bali tunapaswa kuiogopa. Baba Mtakatifu Francisko ameonya
juu ya baadhi ya itikadi, kwasababu anasema itikadi hizo zinatokana na mtu kujiona
kwamba anayo imani iliyokamilika. Lakini Changamoto zinatuokoa kutoka katika mawazo
yetu finyu na kutufungua upeo wetu kuwa mpana.
Kujuhusu kuwa na tamaduni nyingi katika jamii zetu, Baba Mtakatifu anatoa onyo kwamba
hatupaswi kuogopa utofauti ,kwa utambuzi ya kwamba Kanisa ni moja,bali katika uzoefu
wa aina mbalimbali na ndiyo utajiri wa Kanisa."Kanisa ni moja katika utofauti lakini
ni kanisa moja". Na utofauti huo unaunganishwa kuwa katika umoja. Lakini je ni nani
anayefanya tafauti? Ni roho Mtakatifu , ambaye ni mwalimu wa utofauti.Ni nani anayefanya
umoja? Ni Roho Mtakatifu Mwenyewe,akiwa mwalimu wa umoja. Ndiye msanii mkubwa, ndiye
Mwalimu wa Umoja na katika utofauti ni Roho Mtakatifu.Anasisitiza kwamba hilo tunapaswa
kulitambua vema.
Aidha Baba Mtakatifu Francisko anatoa mfano kwamba ulinganifu na wingi zaidi haviendani na siyo mambo yatokanayo na Roho Mtakatifu, bali wengi zaidi na umoja vinatokana na Roho Mtakatifu na kwa njia hiyo anasisitiza juu ya kufanya uamuzi. Kwa kuwasaidia vijana waweza kuamua yaliyo mema katoka katika utamaduni ulio saza. Kwa mfano anasema vijana wetu wako tayari kuchat kila wakati .Wanauwezo kuchat kwa kutumia aina mbili ua tatu za skrin kwa wakati mmoja, na wanawaza kuingiliana kwa wakati mmoja katika matukio mbambali yanayoendelea.Hivyo anasema tupende tusipende ndiyo namna walivyo jikita ndani yake, na kwa njia hiyo sisi kama wachungaji tunao wajibu wa kuwasaidia katika ulimwengu huu.Anaongeza,"nadhani ni vizuri kuwafundisha kupembua ,kwasababu tunazo zana na vifaa vya kuweza kuwasaidia kutembea njia ya maisha bila kuzima Roho Mtakatifu aliye ndani yao".
Shemasi awe mlinzi wa huduma ya Kanisa.Baba Mtakatifu amemjibu Shemasi Roberto Crespi ambaye ni shemasi wa kudumu na kwa namna ya pekee katika huduma yake ya ushemasi.Ameonesha mara moja kuelezea juu ya umuhimu na mchango mkubwa wa maisha ya Kanisa.Lakini pamoja na hayo ametoa onyo mara moja juu ya hatari mbili za huduma ya shemasi, ya kwanza ile ya kiulimwengu na pili ya kufanya kazi zaidi. Baba Mtakatifu anasema Shemasi ni mlinzi wa huduma ya Kanisa. Akichambua maana ya huduma anasema ni ufunguo unaolezea jukumu ya huduma yao, wito wao na wao wenyewe kuwa Kanisa.Wito ndani ya wito kama miito mingine na siyo ya kibinafsi, bali inapaswa kuishi ndani ya familia na familia. Ndiyo ya watu na watu wa Mungu. Maana yake ni kwamaba hakuna huduma altare na hakuna liturujia ambayo aijifungui katika huduma ya masikini , na hakuna huduma ya masikini ambayo haifungujki katika liturujia.Hakuna jamii ya kazi ambayo siyo ya kifamilia.Hiyo inatusaidia kupembua ushamasi kama wito wa Kanisa.Amesisitiza Baba Mtakatifu.
Akijibu swali la mtawa Paola Paganono juu ya changamoto za kikrsto ya kuwa ni wachache
ndani ya jamii ya sasa. Baba Mtakatifu amesema kitendo cha uchache kisiwe kisingizio
cha kutokuwajibika ,kwani tukumbuke daima kwamba ni kiasi kidogo cha chachu kinachohitaji
kufanya unga ukue. Ni bora kuanza mchakato badala ya kujaza nafasi.Leo hii tunapaswa
kuanza michakato badala ya kujaza nasasi , kupambana kwa ajili ya umoja badala ya
kusimamia migongano iliyopita, kusikiliza hali halisi,kujifunua katika wengi kwa watu
wa Mungu na wote wa Kanisa,maana yake kujifungua kikanisa.
Baba Mtakatifu pia amezungumzia juu ya ushuhuda wa watawa wawili Shrika la watawa
wa dada wa Yesu huko Afghanstan, na kusema inabidi kwenda katika maeneo ya pembezoni
na kuwa wamisionari, kwenda kukutana na watu , kukutana na Bwana katika miisho ya
dunia.Na hiyo ndiyo manaa ya kwenda.Kuchangua sehemu za pembezoni,na hivyo amesema
"amkeni na kuanza mchakato, washeni matumani mahali ambapo yamezimika, katika jamii
iliyogeuka na kutokuona uchungu wa wengine. Katika udhaifu wetu, kama vile shirika
linaweza kuwa makini kwa wote walio dhaifu, na baadaye wakageuka sehemu yenye kuwa
na baraka".
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.
All the contents on this site are copyrighted ©. |