2017-03-26 12:11:00

Baba Mtakatifu:Babu zetu wana hekima na uzoefu wa maisha ongeeni nao!


Katika kurithisha imani kwa watoto na vijana kunahitajika ushuhuda, kwa njia ya kuwaonesha imani,inasaidia kwaenda mbele. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi jioni tarehe 25 Machi 2017 katika mkutano wake wa mwisho wa kichungaji huko Milano. Mkutano huo wa vijana walio pata kipaimara Jimbo Kuu Milan ulifanyika katika uwanja mkubwa wa Mpira Meazza-Mtakatifu Siro.Vijana hao waliambatana makatekista wao,wazazi wao nawatu mia 400 wakujitolea.Taarifa zinasema ni zaidi ya vijana 1000 na zaidi ya watu 78,000 katika uwanja huo walio udhulia.Ulikuwa ni muda mzuri wa furaha na vichekesho kwa vijana kuongea na Baba Mtakatifu.Uwanja ulio zoea kuwapokea vikosi vya wana michezo wa mpira, uligeuka  kuwa wa furaha nyingi kwa mtazamo wa rangi za kila aina halikadhalika ulivyopambwa rangi,na katika sala  nyimbo, muziki, ngoma na shuhuda mbalimbali.Yote hayo yameweza kufanikisha kwa njia ya maandalizi ya Chama cha vijana katoliki Jimbo Kuu Milano.

Na katika kujibu maswali ya vijana waliyo muulizia kuhusiana na uzoefu wake alipokuwa kijana kama wao ,Baba Mtakatifu Francisko anasema babu, bibi , marafiki na parokia walimsaidia Papa akue katika imani,Babu na bibi wana hekima na uzoefu wa maisha na hivyo amewashauri waongee na babu zao, na pia kucheza na marafiki vilevile huko parokiani, kwani  ndiyo anasema mambo matatu yaliyo kama uzi wa sala. Swali la pili aliulizwa na familia moja yawazazi, kwa jinsi gani waweze kurithisha imani kwa watoto wao.Baba Mtakatifu Francisko, kwa kuwataka wawelewe zadi  anasema, ni kuonesha  ushuhda hawali ya yote kwa watoto.Kwa njia ya swali hilo amewaomba wote wabaki kidogo kimya kwa kufikiria, ni nani amewasaidia;yeye binafsi amesema alisaidiwa na Padre mmoja aliye mbatiza, na kumsindikiza hadi kuingia unovizi.Aidha ametoa mifano mingi inayo husu ushuhuda na zaidi amesema, ni jinsi gani watoto wanajisikia, wakiona wazazi wao wanagombana au wanaachana . Kwasababu wanao umia ni watoto, na hivyo Baba Mtakatifu Francisko anawaalika kwa namna ya pekee wazazi kusoma vizuri wosia wake wa Furaha ya Upendo, na hasa katika haya za kwanza. Anaongeza macho yao madogo ya watoto wanawatazama bila kuchoka.

Halikadhalika anasema, kuwaonesha ushuhuda wa imani  ni kama kupiga hatua kwenda mbele na kukabiliana uso kwa uso majanga mengi tulio nayo. Na hiyo siyo katika mtazamo usio jasiri, bali ni katika mtazamo wenye matumaini na huo ndio ushuhuda uli bora ambao tunaweza kuwapatia. Baba Mtakatifu anatoa methali moja isemayo "maneno matupu upeperushwa na upepo, lakini yale yanayo pandwa katika kumbukumbu  na katika moyo ubaki daima".
Kutokana na hili, amewaalika kila jumapili kwenda kusali kanisani kwanza na baadye kwenye michezo, au kwenye viwanja ili kuunganika kwa pamoja.Anaongeza kuiishi Jumapili maana yake ni kutumia muda wako kukaa na watoto, kama wasemavyo Buenos Aires. Lakini katika nyakati zetu, wazazi wengi wamepoteza kasumba hii kwani hawachezi na watoto wao.Wito mkubwa kwa wazazi ni kwamba wawafundishe watoto wao, mshikamano na hasa katika matendo ya huruma.

Na mwisho Baba Mtakatifu Francisko amejibu swali la katekista, juu ya umuhimu wa kushirikiana katika kuelimisha, na hivyo anatoa ushauri wa kutumia aina tatu za lugha, ya kwanza ni ile ya akili,ya moyo na mikono. Anasema mwalimu mwema ,au mkufunzi  anajua kuongeza ubora wa wanafunzi wake, bila kusahau yale mengine.Kwa ushauri wake wa mwisho kwa vijana amewaomba watoe ahadi kwa Yesu kwamba kamwe hakuna ruhusa ya kufanya uonevu.Amesema kwa ukimya nisikilizeni,”Ni katika kimya, je katika shule yako, kwa jirani yako, kuna mtu ambaye anatoa matusi hovyo ,na nyinyi mnakuja juu kwasabu anayo kasoro hiyo na kasoro hiyo ni kubwa , kwani inawezekana ni mwembamba na mambo mengine? Fikirieni. Je mnapendelea aendelea kuwa na aibu ,na wakati mwingine kupigwa kwa ajili hiyo?.Fikirieni hali hiyo  inaitwa uonevu!.Tafadhali nyinyi mlio katika maandalizi ya kupokea Sakramenti ya kipaimara fanyeni ahadi kwa Bwana ya kwamba kamwe hatutaruhusu mambo hayo yafanyike shuleni kwenu, katika vyuo vyenu , na katika mitaa yenu, Je, mmeelewa?”Amemaliza na swali hilo Baba Mtakatifu Francisko kwa vijana.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.