2017-03-25 17:22:00

Ni Mungu kwanza anaye kuja kukutana na binadamu mahali alipo!


Tumemaliza kusikiliza habari njema na muhimu ya historia, yaani kupashwa habari mama Maria kwamba atakuwa ni Mama wa Mungu ( Lk 1,26-38). Ni sehemu ninayopenda kuisoma pia katika mwanga wa habari nyingine ya kuzaliwa na Mtakatifu Yohane Mtabatizaji (Lk 1,5-20). Ni habari mbili zinalinganshwa kwa kuonesha kile Mungu anachojalia mwana wake.Ni maneno ameanza nayo Baba Mtakatifu Francisko wakati wa mahubiri yake kwenye uwanja wa Monza huko Milan akiwa katika ziara ya kitume tarehe 25 machi 2017, wakati Mama Kanisa anaadhimisha sikukuu ya kupashwa habari Mama Maria. Habari  ya kuzaliwa kwa Yohane mbatizaji ilitolewa wakati baba yake Zakaria anaandaa liturujia ndani ya Hekalu, na wakati huo waamini wote wanamsubiri nje .Lakini habari ya Yesu ilitokea nje ya mji  huko Galiya, mji ulio kuwa pembezoni, kwa maana nyingine mji ambao haukujulikana katika nyumba ya kijana aliyeitwa Maria.

Ishara hii katika Ekalu la Mungu na makutano ya Mungu na watu, yanatokea katika sehemu ambazo hakuna aliye dhania, yaani pembezoni. Lakini hapo ni mahali pa ahadi,ni mahali pa makutano ambapo Mungu anatoa nyama yake ili kutembea naye hadi kutufikia kwa njia ya Mama yake. Eneo hilo siyo tena kutengwa kwa ajili ya watu walio wachache, walio baki wakisubiri nje. Kwa maana hiyo hakuna atakaye baki tofauti au kukaa katika hali ya binafsi bila uwepo wake, bali furaha ya ukombozi ndiyo inaanza katika maisha yak ila siku katika nyumba ya kijana wa Nazareth.
Ni Mungu mwenyewe anayeanza kuachagua , kama alivyo fanya kwake Maria, na katika nyumba zetu, katika mahangaiko yetu ya kila siku, wasiwasi na shahuku.Na ni pale katika miji yetu, shule zetu vyuo vikuu, katika viwanja na katika mahospitali ni hapo hapo habari njema inakamilisha. Ndipo tunamuona vema na kusikiliza neno “furahi kwa maana Bwana yu pamoja nawe”

Ni furaha inayotoa maisha, inayotoa matumaini ,inayofanyika mwili ili kuweza kutazama  ya kesho na pia kwa kuwatazama  wengine .Ni furaha inayo geuka kuwa mshikamano,makaribisho na huruma  kwa ajili ya wengine.Katika kulinganisha na mama Maria, hata sisi tunaweza kuwa na wasiwasi, wa kujiuliza je ni kwa njia gani hayo yanatokea, kwenye kipindi cha kubahatisha?.Baba Mtakatifu anatoa mifano ya halisi ya maisha ya wasiwasi wa jamii akisema, kubahatisha kuhusu maisha, kuhusu kazi, na kuhusu familia. Ni kubahatisha kuhusu masikini na wahamiaji, kuhusu vijana na maisha yao endelevu. Yote hayo utafikiria kwa mtazamo ni juu ya fedha tu. Pamoja na hayo maisha ya kila siku ya familia nyingi wanajikuta na wasiwasi wa hali ya ukosefu wa usalama na wakati huo uchungu unabisha mlango kila kona, vijana wengi wanakuwa na wasiwasi wa usalama kwa ajili ya ukosefu wa fursa , hali ya kubahatisha inazidi kuongezeka kila sehemu.

Katika hali tunayo ishi, utafikiri kweli tunataka kuibiwa matumani na furaha. Mbele ya matatizo kama hayo utafikiri yanatufanya kutokuweza kukabiilana na changamoto kama hizo, kwa sababu kwamba kila tunapotaka kuelekea katika ujenzi wa kuelekea nadharia ya jamii iliyo bora, matokeo yake hakuna muda wa chochote na hata kwa yoyote yule.Tunapoteza muda kwa ajili ya familia, kwa akili jumuiya kwa ajili ya urafiki, Mshikamano  na kwa ajili ya kumbukumbu.Je Injili ya leo inaweza kutafakarisha namna gani ya kuiishi ndani ya mji wetu? , kuna uwezekano wa kuishi kwa  matumaini ya kikristo kwa hali ya leo hii?. Baba Mtakatifu anatoa maswali hayo, na kuyajibu akisema; maswali haya mawili yanaugusa uzalendo wetu ,maisha ya familia zetu, katika nchi zetu na katika mji. Yanagusia miji yetu, vijana na ambayo yanatufanya tutazame namna gani ya kuwapo na kuendelea  katika historia. Iwapo tunataka kuwa watu wenye furaha na matumaini haiwezekani kubaki tunatazama hali hii ya uchungu kama vile watazamaji wanao angalia juu ya anga wakisubiri mvua ikatishe kunyesha.

Kila kinachotukia hatuna budi kukitazama kwa furaha ya ukombozi ambayo unatengeneza maisha ya kila siku katika nyumba ya kijana wa Nazareth. Mbele ya wasiwasi wa Maria na katika wasiwasi wetu ,tunaweza kupata majibu kwa funguo za aina tatu ambazo malaika anatuzawadia kukubali utume tulio kabidhiwa. Kwanza Malaika anatukumbusha kuwa na kumbukumbu, iliyo fungua uwepo wa Maria katika historia ya wokovu. Ahadi iliyofanya na David, kama tunda la agano na Yakobo na hivyo Maria ni mwana wa Agano; kwa njia hiyo hata sisi le hii tunaalikwa kufanya kumbukumbu kutazama wakati wetu ulio pita ili tusisahau tulikotoka.Tusisahau viota vya mababu zetu ,kwa yote waliyo pitia hadi kufikia mahali sisi tulipo. Ardhi hii na watu wake walikabiliana na uchungu wakati wa vita mara mbili: kwa njia hiyo  kufanya kumbukumbu inatusaidia kutobaki tumefungwa ndani ya mawazo yanayopanda magugu mbaya , au kufanya mipasuko na magawanyiko kana kwamba ndiyo mojawapo ya kutatua vikwazo.Kufanya kumbukumbu inasaidia kujiweka tayari mbele ya kutatua matatizo yanayoweza kujitokeza kama vile mgawanyiko.

Pili kuwa mshiriki wa watu wa Mungu kwa maana ya kufanya kumbukumbuni kukuwezesha  kuwa mmojawapo  watu wa mungu. Inasaidi kukumbuka ya kwamba sisi ni sehemu ya watu wa Mungu wa Milan na ndiyo wa Ambrosi,lakini zaidi wewe ni sehemu ya kubwa ya watu wote wa Mungu. Watu walio undwa na maelfu ya sura, na historia kutoka tamaduni, kabila mbalimbali. Na hii ndiyo utajiri tuli nao.Watu wanao karibisha wangine kuwashirikisha kwa heshima na katika shughuli ili kuadhimisha habari mpya kutoka kwa wengine. Ni watu wasio ogopa kuwakumbatia watu wengine,ni watu wasio kuwa na hofu ya kuwapatia wengine mahali pa kukaa wenye kuhitaji, maana wanatambua kwamba pale yupo Bwana.

Tatu ni kwamba hakuna lisilo wezekana kwa Mungu (Lk 1,37): kwasababu Malaika alimalizia kutoa jibu lake kwa Maria maneno hayo . Tunapofikiria ya kwamba kila kitu kinatokana na sisi,nguvu zetu uwezo wetu , mategemeo yetu tunaishia kubaki  wafungwa. Lakini tunapokubali kusaidiwa na kushauriwa,tunapojifungua katika neema,ndipo kile kisichowezekana kinapata fursa ya uwezekano. Baba Mtakatifu Francisko anasema kwamba uwezekano huo kwa  hayo yote yanatambuliwa na ardhi ya Milan kwasababu katika historia, karama nyingi zimeonekana za kimisionari, na utajiri mkubwa wa Maisha ya Kanisa. Ni ardhi ambayo haikujifungia yenyewa binafsi na mawazo yake , bali ikawa na uwezo wa kujifungua kwa wengine.
Jana kama leo Mungu anaendelea kuwatafuta wafuasi  wake , wanawake na waume wenye uwezo wa kuamini,wenye uwezo wa   kufanya kumbukumbu na kuwa sehemu ya watu wake katika kushirikiana kwa njia ya roho. Mungu anaendelea kupita katika mitaa na barabara zetu. Na pia anaendelea kupita katika mioyo ya yenye uwezo wa kusikiliza na kuwa mwili mmoja hapa .Kwa kulinganisha na maneno ya Mtakatifi Ambrosi katika tafakari yake, tunaweza kusema “ Mungu anaendelea kutafuta mioyo kama ile ya Maria, yenye uwezo wa kuamini na zaidi katika hali  isiyo ya kawaida. Hivyo Bwana Atufanye kukuza imani na matumaini katika maisha yetu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.