2017-03-24 16:41:00

Katika ubatizo tunashiriki kifo na ufufuko wa Yesu Kristo!


Padre Raniero Cantalamessa mhubiri wa nyumba ya Kipapa wakati wa Kipindi cha Kwaresima kwa mwaka 2017 ameendelea na tafakari za Ijumaa baada ya tafakari yake ya kwanza ya  tarehe 17 Machi 2017.NaKauli mbiu inayoongoza tafakari za Kipindi cha Kwaresima ni “Wala hawezi mtu kusema, “Yesu ni Bwana” Isipokuwa katika Roho Mtakatifu”.(1Kor. 12:3). Padre Cantalamessa Ijumaa 24 Machi 2017 amesema ; katika utanguliza wa tafakari mbili zilizopita , tumejaribu kuonesha jinsi gani roho Mtakatifu anatuelekeza uhalisia wa ukweli juu ya Kristo, kwa kuonesha kwamba yeye ni Bwana na kama Mungu kweli kwa Mungu kweli. Tafakari zinazobaki , ni kwenda moja kwa moja katika wajibu wa Kristo.Tutaonesha jinsi gani Roho Mtakatifu anaangaza fumbo la Pasaka na hawali ya yote kuanzia  katika tafakari ya fumbo la kifo chake.

Kuna umuhimu  gani wa sasa kwa mwaamini au kila binadamu kutambua juu ya maana, au kifo kina mwisho wake ?, badala yake ni kinyume kwasababu huo  ni mwanzo wa maisha.Kwa kuelezea ukweli wake, fumbo la pasaka ya kifo na ufufuko wa Kristo ndilo jibu peke yake kwa kujibu  maswali kama hayo.Padre Cantalamesaa anasema ; kwa utambuzi huo tutafakari fumbo la Pasaka ya Kristo kuanzia kifo msalabani .Katika barua ya wahebrania inasema, Kristo kwa njia ya Roho Mtakatifu alijitoa mwenyewe bila kuwa na madoa kwa  Mungu” (Wab 9,14). Roho milele kwa maana nyingine ni kusema Roho Mtakatifu maana ya kusema  ubinadamu wa Yesu  alipokea Roho Mtakatifu aliyekuwa ndani yake na kutoa sadaka kwa Baba yake , ni nguvu ya roho inayo mwimarisha wakati wa mateso.Katika liturujia  inayo tanguliwa Komunio ,Padre anasali “ Bwana wetu Yesu kristo, Mwana wa Mungu aliye hai, kwa mapenzi ya Baba na kwa nguvu ya Roho Mtakatifu aliye maisha ya ulimwengu....

Hiyo inajitokeza kama sadaka kama vile sala ya Yesu,”siku ile Yesu akafurahi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu akasema nakushukuru ee Baba , Bwana wa Mbingu na dunia” (Lk 10, 21). Ni roho Mtakatifu ndani mwake iliyo mfanya kusali, ni roho Mtakatifu iliyo msukuma kujitoa sadaka ya kuteketezwa kwa Baba. Roho Mtakatifu ambaye ni zawadi ya milele ambayo ni mwana wake Baba milele, ni roho mwenyewe anaye msukuma kutoa sadaka ya kuteketezwa kwa baba kwa ajili yetu wakati ule. Uhusiano kati ya Roho Mtakatifu na kifo cha Yesu, vimeoneshwa hasa zaidi katika Injili ya Yohane: aliyasema hayo kumhusu  Roho ambaye wale walio mwamini yeye watampokea.Wakati huo Roho alikuwa hajafikia kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa bado" (Yh 7,39). Kwa upande wa Yohane ,maneno hayo yalitamkwa kabla Yesu kutundikwa msalabani.Yesu Msalabani anatoa roho yake,inaonekana katika maji na damu,kama anavyo andika Yohane katika barua yake ya kwamba ,”basi wako mashahidi watatu:roho maji na damu , na ushaidi wa hawa watatu waafikiana. ” (1 Yh 5, 7-8).

Roho mtakatifu anampeleka Yesu msalabani, na katika msalaba Yesu anatoa zawadi ya Roho Mtakatifu.Roho Mtakatifu alikuwapo katika maisha ya Yesu tangu kuzaliwa kwake, kuanza maisha ya utume,na katika ubatizo. Na wakati wa kifo chake Yesu msalabani, Yesu anatoa zawadi ya Roho mtakatifu, ambayo inajionesha kwa mtume Petro siku ya Petekoste akisema; baada ya kupokea roho Mtakatifu ndani mwetu kama vile mnavyo ona na kusikia (Md 2,23).Kwa namna hiyo nini maana yake kwetu sisi kifo cha Kristo?. Hawali ya yote ni kwa ajili yetu, kwani katika sala ya nasadiki tunamalizia na maneno ya "nangojea ufufuko wa miili na uzima wa milele ijayo". Sala hiyo haisemi ufufuko ulio tangulia na maisha ya milele, hasa ya kifo. Kwasababu kifo siyo kitu cha imani bali ni uzoefu.Kwa maana  hiyo kifo ni karibu na sisi linachopitia kwetu kwa ukimya.

Pamoja na historia ya kifo, binadamu wa nyakati zote ametafuta namna ya kupambana na kifo, na hata leo hii, binadamu huyo anajaribu kujituliza. Tunaweza kusema kwamba kifo ni matatizo ya binadamu kwa namna moja.Hata Mtakatifu Agostini katika tafakari yake ya kitaalimungu ya sasa juu ya kifo anasema; Binadamu anapo zaliwa, watu wengi wanakuwa na mawazo tofauti ya kumfikiria atakuwaje, wanafikiri ya kwamba mtoto huyo anatakuwa mzuri, au mbaye, atakuwa tajiri, au masikini, ataishi maisha marefu au hapana. Lakini hakuna yoyote asemaye labda atakufa.Padre Cantalamessa anasema lakini kifo  ndiyo uhakika wa maisha.Tukisikia mtu kaugua ugonjwa usio tibika , mara moja tunasema ,masikini lazima afe, amehukumiwa kufa na hakuna la kufanya.Lakini kwa nini tusisema maneno kama yaliyosemwa kwa yule aliyezaliwa?.badala yake ni masikini, lazima afe na hakuna cha kufanya . Kuna tofauti gani kati ya muda mfupi na muda mrefu. Kifo na ugonjwa wa kufa inatofautaiana katika kuzaliwa.

Kwa mtazamo huo  tunaweza kufikiria juu ya mauti ya maisha , Kama vile mwana filosofia mwingine  Martin Heidegger anayesema “kuishi katika kufa. Kuishi ni kufa. Kila dakika tunayoishi ni jambo linalo ungua, tunaelekea katika kifo.Kuishi kaitka mauti haina maana ya kwamba kifo ndiyo mwisho wa yote bali ni mwisho wa maisha .Tunazaliwa pia kwajili ya kufa, hakuna jambo jingine.Tumetokana na utupu na tutarudi katika utupu na hakuna njia nyingine kwa binadamu. Padre anasema, lakini katika tafakari ya kikristo kuna mabadiliko ambapo ubinadamu ni wa umilele.TaaliMungu ya kikristo inatoa utofauti kwasababu ya imani katika Kristo. Kwa kuwaacha wanataalimungu, Padrei Cantalamessa anasema tuwatazame watunzi wa mashairi wenye kuwa na maneno ya hekima na rahisi kuelezea  ukweli juu ya kifo. Kwa mfano wa Giuseppe Ungaretti  akiandika kuhusu mwanajeshi katika makambi ya mapambano ya vita anafananisha na  hali ya kila binadamu mbele ya fumbo la kifo akisema , kifo ni kama majani ya mti yanapo pukutika yote wakati wa kipindi cha baridi.

Hali kadhalila vitabu vya Biblia katika Agano la kale hawana majibu ya dhati juu ya kifo.Kwa upande wa vitabu vya hekima vinagusia, lakini kwa namna ya ufunguo wa maswali badala ya majibu. Mfano wa vitabu hivyo ni Ayubu, Zaburi Muhubiri na Hekima .Vitabu hivi viyo vinagusia kwa makini mada ya kifo. Mfano Zaburi inasema “nifundishe kuhesbu siku za maisha yangu ili tuweze kuwa na hekima  ya moyo.(Zb 9,12).Lakini kwanini kuzaliwa , kwanini kufa ? baada ya kifo tunakwenda wapi?. Maswali hayo katika vitabu vya hekima yanabaki bila kuwa na jibu. Mungu anataka hivyo na juu ya hayo yote yataoneka katika hukumu ya mwisho. Anasema Padre Catalamessa.Katika Biblia tunakutana na maaandishi mengine kama vile  maisha yetu  ni mafupi na yenye huzuni , hakuna cha kufanya mtu anapokufa lakini maandishi mengine yanasema : "katika upotofu wao uambiana: Maisha yetu ni mafupi na yenye taabu. Kifo kinapowasili hakuna dawa ya kuepuka nacho.Hakuna mtu aliye wahi kumtoa ahera.Padre anasema ni katika kitabu hicho cha Hekima ya Solomoni, mawazo ya kifo yanaanza kuwa wazi kwa mfano," lakini wanyofu wako mikononi mwa Mungu mateso yote hayatawapata kamwe".Lakini pia ni kweli kwamba haijulikani anataka kusema nini , pamoja na kwamba kweli  katika Zaburi maneno mengine yanasomeka “kifo cha waamini wake Mwenyezi Mungu si jambo dogo mbele yake”(Zab 116,15). Pamoja na kwamba hatuwezi kusimama katika sentensi hiyo kwasababu inaleta  maana nyingine ya kuwa Mungu anafanya walipe  zaidi waamini wake kwa maana  ya kuulizwa matendo yao.

Katika nyakati zote kuna vyama vingi  kwa ngazi za kidunia vinavyotaka kuonesha kwaaba hakuna kifo bali maisha ni ya milele . Kwa upande waamini kama vile Mkriso na myahudi anaweza kufikiria kwa haraka maneno ya Nyoka aliyo mwambia binadamu wa kwanza ya kwamba "hamtakufa kamwe bali mtakuwa kama Mungu (Mw3,4-5),lakini badaye  tunajua mwisho wa historia hiyo ilivyoendelea.
Kwa wakristo tunatambua ya kwamba ipo njia moja tu ya kubadili kifo , ambayo mtaktuf Paulo anasema ; kwa njia ya mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni nayo ikasababisha kifo .Hivyo kifo kimeenea katika jumuiya yote ya binadamu, kwa maana wote wametenda dhambi .Ingawa dhambi ya mtu mmoja ilisababisha kifo kwa wote , kwa fadhili ya mtu mmoja yaani Yesu Kriso . Mungu amewasaidia  watu wote neema na zawadi zake.
Na wote wanaopokea neema na zawadi hiyo ya kufanywa kuwa waadilifu , watatawala katika uhai kwa njia ya huyo mmoja yaani Yesu Kristo (Rm 12-17).

Pia kwa ushindi wa Kiroho juu ya kifo umeandikwa kutoka katika Barua ya kwanza ya Mtakatifu Paulo kwa Wakorinzi ,kuwa "kifo, ushindi wako uko wapi?Uwepo wako wa kuumiza uko wapi? (1Kor 15,54-57); na pia anasema, Yeye alikufa kwa ajili ya wote.  2Kor 5,15). Kwa njia hiyo tunaweza kusema kwamba yeye ni mtoto wa Mungu aliyeshuka chini katika kaburi, kama mfungwa , lakini akatokea katika ukuta mwingine.Yeye hakurudi nyuma mahali aliponingilia kama Lazaro, ambaye baada ya kufufuka alikufa tena .Yeye alifungua njia nyingine ya kwamba yoyote anaye mwamini aweze kumfuata yeye.
Je kifo cha Yesu kimebadilisha nini?, Mantiki ya kifo  cha Yesu ni kwamba kifo kinabaki pale pale kwenda katika kaburi, lakini pakiwa na uwezekano wa kutoka katika kaburi hilo,kwa kila anaye amini.Katika kupata maelezo zaidi kuhusu hilo Mtakatifu Paulo kwa watesalonike anaandika “ ndugu  twataka mjue ukweli kuhusu ambao wamekwisha fariki dunia, ili msipatwe na huzuni kama watu wengine wasio kuwa na matumaini.Sisi tunaamini ya kwamba Yesu alikufa , akafufuka, na hivyo sisi tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja na Yesu wale wote waliofariki wakiwa wana mwamini.( 1Tes4,13-14).

Kwa maana hiyo siyo kwamba hakuna huzuni bali wasiwe kama wasio amini kwasababu kifo kwa waamini ni mwanzo wa maisha mapya, kwa njia hiyo siyo kuruka katika utupu bali ni kuruka katika umilele.Ni kuzaliwa upya ni katika ubatizo mpya na kuanza maisha mapya yasiyo na mwisho.Kanisa linapo adhimisha sikukuu ya watakatifu,siyo kwamba inaadhimisha siku ya kifo chao, bali kwa alili ya kuzaliwa upya mbinguni.;Mwandishi mmoja  wa kitabu akigusia juu ya maisha anasema, kati ya maisha ya imani ya wakati  na maisha ya milele kuna uhusiano mkubwa unao fafana uwepo wa maisha ya umbu la mama na mtoto baada ya kuzaliwa. Kwa hiyo kifo ni kama ubatizo, ambao unajionesha kwa upande wa Yesu aliposema !nina ubatizo ambao inanipasa niupokee" (Lk 12,50).Na Mtakatifu Paulo anasema ubatizo ni kama  kubatizwa katika kifo cha Yesu (Rm 6,4).Ndiyo maana zamani wakati wa kubatiza mtu alikuwa akiingia ndani na kufunikwa na maji kabisa,akiwa amevaa nguo nyeupe kwa maana ya kwamba dhambi zote zilikuwa zinabaki zimefunikwa na maji na anatoka akiwa kiumbe mpya. Ni mfano wa  kifo cha mdudu,anazaliwa kipepeo.Kwani  "Yeye atayafuta machozi yao yote, maana kifo hakitakuwako tena, wala uchungu , wala kilio, wala maumivu maana ile hali ya kale imepitwa"

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.