2017-03-23 16:25:00

Wenye heri wapya ni ushuhuda wa uaminifu wa ahadi ya ubatizo!


Jumamosi 25 Machi 2017 Kanisa litawapata wenye heri, wafia dini wa Almeria Padre Álvarez Benavides y de la Torre aliye kuwa dekano wa Kanisa kuu na wenzake wafia dini 114 katika miaka ya 1936-1938. Kuhusiana na wenye heri wapya , Kardinali Angelo Amato  Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya mchakato wa kutangaza wenyeheri na watakatifu akihojiwa na Radio Vatican amesema;katika miaka hiyo nchini Hispania kulikuwa na vita na mashambulizi dhidi ya Kanisa na waamini wake.Kwa njia hiyo maelfu ya waamini wakiwemo waamini walei, mapadre,watawa waliuwawa kinyama kwasababu walikuwa wakatoliki.Katika majimbo yote, yamepata mchango wa wafiadini, kwa maana ya kwamba  leo hii Baba Mtakatifu Francisko amepokea ombi la wengine 115 wafiadini wa Almeria walio uwawa kwa sababu ya chuki katika kutetea imani yao.Inabidi kuwa na kumbukumbu zaidi ili tusiweze kamwe kupoteza urithi huo usio weza kulinganishwa kwa utii wa Mungu katika maisha na katika kijitoa kwa neno la upendo.Tuwakumbuke kwa sababu tunataka kurudia kusema kwamba ukristo ni dini ya upendo na maisha ambayo yanapinga aina zote za nguvu na vurugu.

Kuhusu Padre José Álvarez- Benavides de la Torre,anasema, shuhuda nyingi zinasema alikuwa mchungaji mwema , mwemye hekima na karama nyingi. Siku za mwisho wa maisha yake Julai 1938 kifungo chao kilikuwa kwenye mtumbwi wa kubeba vyuma, kwani yeye na wenzake nguo zao ziligeuka kuwa nyeusi kama mkaa .Lakini pamoja na mateso hayo Padre Jose aliweza kuwatuliza wenzake katika sala.Na alipo ombwa kukana imani yake kwa mateso makali yeye hakuweza kufanya hivyo na ndipo alipigwa risasi. Wakati akikata roho alitamka maneno kama ya Kristo mfalme ya kuwasamehe watesi wake. Na kwa upande wa walei, kati yao Bwana Luis Belda Y Soriano de Montoya,mwenye umri wa miaka 34 akijishughulisha katika chama cha vijana katoliki na wakili wa Taifa.Alikuwa mtu mnyenyekevu , akijibidisha katika kuwasaidia wenye matazo, hakukosa ibada ya misa ya kila siku. Alikuwa na moyo wa kitume kwasababu aliwatembelea wagonjwa ,alifanya mikutano ya wanafamilia, mafunzo ya watoto, na hasa kwa ajili ya utetezi wa watoto wa kutokutoa mimba. Aliwafundisha wote juu ya heshima kwa kila mtu. Alikuwa na ibada maalumu kwa Bikira Maria kwa kusali Rosari kila siku, alipenda Kanisa kuwa mwaminfu wa Baba Mtakatifu pamoja na utii wa Askofu.Ni yeye mwenyewe aliyejikabidhi kwa maaskari ili aweza kusalimisha familia yake, na sababu yake ya kuwawa, ni kwasababu alikuwa mkatoliki.Kabla ya kifo chake ,akiwa kwenye mtumbwi alipiga kelele kwa mke wake akisema maneno ya kuwasamehe wote watakao fanya vibaya.

Katika orodha ya wenye heri wapya wapo wanawake walio uwawa kwa chuki za kidini kwa mfano Mama Carmen Godoy Calvache mwenye umri wa miaka 49. Alikuwa mwenye upendo mkubwa,alitumia fedha zake kuwasaidia wengine wenye matatizo ya afya na watoto, kwasababu aliwatuma kwa daktari na aliwalipia fedha za madawa. Kabla ya kuuwawa, kwanza alitolewa mali zake zote hata fedha kwenye benki na pia walichukua nyumba . Alifungwa na kupata matatizo makubwa, hadi kuhukumiwa kifo cha njaa na kiu, mara baada ya kumtesa sana, waliamua kimzika akiwa bado hai.

Kardinali Amato anasema pamoja na kuongelea juu ya watu watatu, lakini ni vema kutambua kwamba wote hawa wafiadini walikuwa ni wema, na hawana hatia , walikuwa kama kondoo walio kutana na mbwamwitu na kuwaondolea adhi yao ya kibinadamu. Kwa namna  hiyo tupo mbele pande mbili mmoja wa kuonesha  adhi yao na kwa upande mwingine unaonesha ubaya walio tendewa. Leo tunatoa shukrani kwa wenye heri wapya kwa ushuhuda wa uaminifu katika Kristo na uthabiti wa ahadi za  ubatizo. Tuna waheshimu kwa heshima yao kama mifano ya msamaha na kutuongoza kupendelea yaliyo mema.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.