2017-03-23 13:53:00

Siku ya leo sikilizeni sauti ya Bwana msifanye migumu mioyo yenu!


Inabidi kusikiliza neno la Mungu, ili mioyo yetu isiwe migumu, ni maneno yanayoonekana katika uchambuzi wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa misa ya asubuhi Alhamisi 23 Machi 2017 katika Kikanisa cha Mtakatifu  Marta mjini Vatican, akisisitiza kwamba iwapo tunakwenda mbali na Mungu kuna hatari ya kugeuka viziwi  wa Neno, pia kuwa wakatoliki wasio imani na mwishowe kugeuka wakatoliki wasio mjua Mungu. 
Baba Mtakatifu anasema iwapo watu hawasikilizi neno la Mungu na kugeuzia mabega , mwisho wake wanakwenda mbali na yeye.Hayo anayasema akichambua maneno kutoka katika somo la siku katika kitabu cha Yeremia,ili kupanua zaidi tafakari na umuhimu wa usikivu wa Neno la Mungu.Kama husikilizi sauti ya Bwana ,unasikiliza sauti nyinginezo.Kama usikilizi Neno la Mungu,mwishowe unasikiliza mihhungu ya dunia.

Baba Mtakatifu anasema, iwapo leo hii kila mmoja anabaki kimya na kutafakari binafsi na kujiuliza ndani ya moyo , anaweza kuona ni mara ngapi mioyo imefungwa na masikio yamekuwa kiziwi. Hiyo ni kusema watu, jumuiya, tukiwa na maana ya jumuiya ya kikristo, parokia na jimbo kifunga masikio na kuwa viziwi mbele ya Neno la Mungu na kutafuta sauti nyingine au mabwana wengine, na mwisho kwenda kuishia katika kutafuta mihungu. Ni mihungu ya dunia hii ambayo jamii inatoa , hiyo ni kwenda mbali na Mungu aliye hai.Tunapokwenda mbali na Mungu anaendelea na tafakari, mioyo yetu inakuwa migumu, imefungwa yenyewe, na ambayo haina hata uwezo wa kupokea jambo lolote, siyo tu kufungwa bali ni ugumu wa moyo,wa kumfanya mtu aishi maisha yasiyo stahili na kufanya uendelee kuwa mbali kila siku.

Maneno haya mawili ya  kusikiliza Neno la Mungu na moyo kuwa mgumu, uliofungwa wenyewe, unasababisha ukosefu wa uaminifu.Unapoteza maana ya uaminifu.Katika somo la kwanza, limesema juu ya waamini walivyo poteza uaminifu,  kwa njia hiyo ,ni kama  wamegeuka wakatoliki wasiyo na imani ni wapagani,mbaya zaidi ni wasio mjua Mungu.Hawa ni kwasababu wamekosa mwelekeo wa upendo wa Mungu aliye hai. Na hiyo ni matokeo ya kuwa na mioyo migumu au  kupigia kisogo neno la Mungu ambapo imefikia kuwapelekea  katika njia ya ukosefu wa uaminifu.
Je ukosefu wa uamanifu unatokana na nini? Baba Mtakatifu Francisko anauliza swali,umejazwa kwa njia ya kuchanganyikiwa , kwasababu hawajuhi Mungu yuko wapi, wana muona Mungu mahali ambapo siyo kwasababu kwao Mungu amejichanganya na shetani. Ni tafakari ya maneno kutoka  Injili ya Siku ambapo.Baba Mtakatifu anafafanua kuwa ,watu walimwona Yesu akifanya miujiza  na mambo mengi, kwa ajili ya uokovu wao, kwa furaha watu wakasema, anafanya hivyo kwasababu yeye ni mtoto wa shetani.Ana uwezo wa Beelzebuli. Neno hilo kwa hakika ni kashfa Baba Mtakatifu Francisko anasisitiza.

Kashfa ni neno la mwisho katika hatua ya yule asiye sikia Neno na kujifanya mgumu wa moyo. Anaye leta mchanganyiko  kutokuwa mwaminifu, mwishowe anatoa  kashfa. Anaongeza , ole wao watu wale wanao sahau mshangao wa kwanza wa kukutana na Yesu.Amemalizia akisema,leo hii kila mmoja ajiulize; je ninasimama na kusikiliza Neno la Mungu, ninachukua Biblia mikononi na kuona kwamba inaongea na mimi?.Moyo wangu ni mgumu?. Nimekwenda mbali na Mungu?.Nimepoteza matumaini na Bwana na kuishi na mihungu itokanayo na malimwengu?. Nimepoteza furaha na mshangao wa makutano ya kwanza na Yesu?.Anaongeza leo hii iwe siku ya kusikiliza sauti ya Bwana,kwa njia ya sala iliyoskika  msifanye migumu mioyo yenu na tuombe neema hii , neema ya kusikiliza ili mioyo yetu isiwe migumu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.