2017-03-21 16:15:00

Mons. DE WIT GUZMÁN ateuliwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Santiago DE WIT GUZMÁN kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini  Jamhuri ya Watu wa Afrika ya kati. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amempendisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu.Kabla ya uteuzi wake alikuwa mshauri wa ofisi ya ubalozi wa Vatican kwenye makao ya ubalozi  huko Gabala nchini Jamhuri ya Afrika ya kati. Askofu mkuu mteule Santiago De Wit Guzman alizaliwa tarehe 5 Septemba 1964 huko Valencia, nchini Hispania. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi kunako tarehe 27 Mei 1989 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Alianza huduma ya kidipomasia mjini Vatican kunako tarehe 13 Juni 1998. Tangu wakati huo, ametoa huduma yake huko Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati, Netherland, Paraguay, Misri, DRC na Hispania.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.