2017-03-21 15:30:00

Mama Maria kijana kama ninyi hakubaki amekaa katika sofa nzuri !


Katika kufanya maandalizi ya siku ya vijana Duniani kuanzia  mwaka 2017 hadi kufikia kilele chake 2019 huko Panama, maandalizi hayo yameanza kupamba  moto, tukumbuke kwamba kauli mbiu itakayoongoza siku ya Vijana inatokana na utenzi wa Bikira Maria yaani Magnificat, hivyo  kwa mwaka 2017 itakuwa  sehemu ya “Mwenye nguvu amenitendea makuu, na jina lake ni takatifu”(Lk 1,19. Mwaka 2018 itakuwa sehemu ya “Usiogope Mariam kwa maana umepata neema kwa Mungu” (Lk1:30). Na mwaka 2019 ambayo ndiyo kilele chake itahusu “Tazama mimi ni mjakazi wa Bwana na iwe kwangu kama ulivyosema Lk.1,38).Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko ametoa ujumbe kwa njia ya video kwa vijana kwa ajili ya maandalizi hayo na kusema kwamba :Ninakumbuka kwa uhai kabisa katika makutano ya Siku ya Vijana 2016 huko Krakow , ambapo tulianza safari kuelekea katika mkutano mwingine Mungu akipenda huko Panama mnamo mwaka 2019.

Kwa upande wangu ni wakati muhimu sana wa  kukutana na kuzungumza na nyinyi.Nilitaka safari hiyo iwe sambamba na maandalizi ya Sinodi ya Maaskofu , ambayo imewekwa kwa ajili ya vijana.Katika safari hiyo, anatusindikiza Mama yetu Maria ,ambaye anatupenda na imani yake; ni imani yake anayo jieleza  katika wimbo wake wa shukrani ya kwamba Bwana amenitenda makuu (Lk 1,49).Yeye anamshukuru Mungu kwa kumtazama udogo wake. Na katika kutambua makuu aliyo mtendea maishani mwake  anaanza safari kwa ajili ya kukutana na Elizabet, mzee na mwenye kuhitaji msaada wa ukaribu. Maria hakubaki nyumbani amefunga mlango, hiyo ni kwa sababui yeye hakuwa  kijana wa kupenda sofa , anayetaka kubaki katika raha, kujisikia salama bila kusumbuliwa na lolote. Ametikiswa na imani, kwasababu imani ni moyo wa historia yote ya mama yetu.Anasema Baba Mtakatifu Francisko.

Vijana wapendwa hata Mungu anawatazama na kuwaita, anapofanya hivyo anaona upendo mlio nao na kwamba mnao uwezo wa kuutoa.Kama alivyo fanya kijana wa Nazareth, na nyinyi mnaweza kufanya dunia iwe bora,na kuacha alama ya historia , yaani historia yenu na  ya wengine wengi.Kanisa na.Kanisa na jamii wanahitaji ninyi,kwa mbinu zenu, ujasiri wenu mlio nao, ndoto zenu na mawazo yenu,vinaweza kuangusha kuta zilizo simikwa katikati na kufungua njia ambazo zitawapeleka katika ulimwengu ulio bora,wa haki na usio kuwa na ukatili bali wa ubinadamu zaidi.

Kwa kipindi chote cha safari hii, ninawatia moyo wa kuhamasisha mahusiano ya kifamilia , urafiki na Bikira Mtakatifu, ambaye ni mama yetu. Ongeeni naye kama Mama.Na kwa njia yake toeni sifa kwa zawadi yenye thamani ya imani , ambayo mmepokea toka kwa mababu zenu, na mwaminishe maisha yenu yote.Kama mama mwema yeye anawasikiliza, anawakumbatia, anawatakia mema na kutembea nanyi. Mkifanya hivyo, ninawakikishia hamtajuta kamwe! .Ninawatakia hija njema ya siku ya vijana  Duniani 2019!.Na Mungu awabariki.
Hayo ndiyo matashi mema ya Baba Mtakatifu Francisko kwa njia ya video amewatakia vijana wote katika maandalizi ya safari kuelekea Panama katika Siku ya Vijana duniani mwaka 2019.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.