2017-03-20 13:31:00

Tukutane na Yesu katika sala na hasa katika uso wa yule anayehitaji


Katika Injili ya Domenika ya Tatu ya kwaresima, Iinatuonesha , mazungumzo ya Yesu na mwanamke msamaria (Taz Yh 4,5-42). Mazungmzo hayo yalitokea wakati Yesu anakatisha mjia katika mji wa Samaria , Mji ulioko kati ya Mikoa ya Uyahudi na Galilaya , Samaria ni mji ambao ulikuwa na mafarakano na kudharauliwa. Lakini ni ukawa mji wa kwanza kukubali mahubiri ya Yesu katika kwa mitume wake. Mitume walikuwa wamekwenda kutafuta chakula,  wakati Yesu alibaki kisimani,  na kuomba maji mwanamke aliye kuwa amekuja kuchota maji kisimani. Kwa njia ya kuomba maji, ndipo yakaanza mazungumzo.Ni jinsi gani myahudi kudiriki kuomba jambo lolote kwa msamaria?. Yesu akamjibu, kama ungejua mimi ni nani na ni zawadi gani niliyo nayo kwako ,ni wewe ungeniomba ukiwa wa kwanza maji ya uzima. Maji yanayotoa  kila aina ya kiu  na kugeuza chemichemi katika mioyo kwa wale wanao kunywa maji hayo.

Baba Mtakatifu Francisko anasema, kwenda katika kisima kuchota maji ni kazi ngumu na inaudhi; Ni vizuri kuwa na maji tayari yanayotirirka!.Lakini Yesu alikuwa akizungumzo juu ya maji tofauti. Mwanamke alipogundua ya kwamba anaongea na nabii akaamua kumweleza ukweli wa maisha yake kwa mantiki ya dini. Kwasababu kiu yake ya kutafuta upendo haikuweza kuisha kutokana na wanaume watano alio olewa nao, zaidi ya hayo alipata uzoefu wa kukata tama na pia katika uongo. Kwa njia hiyo mwanamke anashangazwa na ukarimu na heshima kwa ajili yake na hasa anapoongea na Yesu anaonekana kumuonesha imani ya mwamba kuma uhusiano wake  na baba katika Roho na Kweli.Mwanamke anatambua ya kwamba mwanaume huyo anaweza kuwa ndiye Masiha. Kitu cha kushangaza,Yesu ndiyo mimi ninaye ongea na  wewe. Yesusa anajitambulisha kuwa masiha kwa mwanamke ambaye alikuwa na maisha mchanganyo.

Maji anayo yatoa ni ya  uzima wa milele, Baba Mtakatifu Francisiko anafafanua kwamba maji hayo  yametawanyika katika mioyo yetu tangu siku ile ya ubatizo, Mungu anatubadili na kutujaza neema yake. Lakini inawezakana kwamba zawadi hii tumeisahau ,na kubaki katika orodha ya vyetu tu vya ubatizo; na labda tunakwenda kutafuta visima vya maji yasiyo toa kiu. Hiyo ni kwasababu tunaposahau maji ya kweli tunakwenda kutafuta visima visivyo na maji safi. Kwa maana hiyo Injili hii inatuhusu sisi!. Siyo kwa ajili ya wale wasamaria , bali ni kwa ajili yetu, Baba  Mtakatifu anasisitiza!.
Yesu anazungumza kwetu kama vile Msamaria,sisi tayari tunamtambua , ila labda hatujakutana naye binafsi. Tanatambua Yesu ni nani lakini kwa bahati mbaya hatujakutana naye binafsi, kuongea naye, na hatujamtambua kama kwamba yeye ni mkombozi wetu. Katika kipindi hiki cha kwaresima , ni fursa nzuri ya kumkaribia , kukutana naye katika sala na kufanya mazungumzo ya moyo, kuzungumza naye , kumsikiliza yeye. Ni fursa njema ya kumtazama uso wake na kwa njia ya  uso wa ndugu anayeteseka.
Kwa njia hiyo tunaweza kubadilika kwa upya katika  neema ya ubatizo tuliyo ipokeana tukatulizwa kiu katika chemichemi ya Neno la Mungu na katika Roho Mtakatifu kwa kugundua furaha ya kuwa na mapatano  na kuwa chombo cha amani katika maisha yetu ya kila siku.

Baba Mtakatifu Francisko amemalizia akisema; Mama maria autusaidie kuchota neema hii kila wakati , maji yatokayo mwambani ,ambaye ni Kristo mwokozi ili sisi tuwezea kukiri kwa hakika imani yetu na kutangaza kwa furaha maajabu ya upendo wa Mungu, na huruma ya chemichemi ya kila jema.
Baada ya Angelus
Mara baada ya mahubiri yake , amewatolea salam mahujaji wote takribani  40,000 katika viwanja vya Mtakatifu Petro;akiwawakumbuka wakazi wa nchi ya Peru walio kubwa na mafuriko na kusasabisha vifo vya watu wengi na wengine kukosa mahali pa kukaa.
Aidha akikumbuka sikukuu ya Mtakatifu Yosefu ambayo Kanisa limeiadhimisha tarehe 20 kutokana na kufikia kilele chake siku ya Jumapili  amewatakiwa matashi mema mababa wote wa familia .

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.