2017-03-18 15:47:00

Ziara ya Papa Francisko Barani Afrika, 28 - 29 Aprili 2017


Dr. Greg Burke msemaji mkuu wa Vatican anasema, Baba Mtakatifu Francisko amekubali mwaliko uliotolewa na Rais wa Misri, Baraza la Maaskofu Katoliki Misri , Mheshimiwa Sana Papa Tawadros II pamoja na Sheikh Ahmed Mohamed El Tayyib wa Msikiti Mkuu wa Al Azhar, mjini Cairo, ili kutembelea Misri kuanzia tarehe 28- 29 Aprili 2017. Kwa namna ya pekee kabisa, Baba Mtakatifu Francisko atatembelea mji wa Cairo. Taarifa zinabainisha kwamba, wakati wowote kuanzia sasa ratiba elekezi ya ziara ya kitume ya Baba Mtakatifu Barani Afrika itatolewa na Vatican.

 

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.