Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

Nafasi ya mwanamke katika ulimwengu wa kazi ni nguzo isiyoonekana!

Askofu Mkuu Auza anasema,ni jambo linalopaswa kuwa muhimu hasa la kazi ya mwanamke katika kutunza familia,ni zawadi,ni asili ya mwanamke kuwasaidia wengine - RV

18/03/2017 14:57

Jumuiya ya kimataifa , inalinda kwa nguvu na kuthibitisha hadhi ya wanawake katika sehemu ya kazi.Ni msisistizo wa wito ulitolea hivi karibu katika Umoja wa Mataifa mjini New York na mwakilishi wa kudumu wa Vatican Askofu Mkuu Bernardito Auza.Askofu Mkuu alitoa hotuba yake katika kikao juu ya Tume kuhusu hali ya Wanawake kikao kinacho endelea hadi tarehe 24 Machi 2017 kuhusu mandhari ya kazi za wanawake katika ulimwengu unao badilika.Askofu Mkuu Auza anasema wanawake ni nguzo lakini hazionekana, ambapo wanafanya kazi na kukuleta faida katika nchi, lakini kazi yao na hata katika mfumo wa uchumi , hauwafikiri, na wala kuwaangalia.Hawapo hata katika orodho ya sekta ya kazi na wanabaguliwa, na mbaya zaidi ni kama kazi hiyo inategemea  uwezekano wa kushirikiana  na nchi nyingine.

Anatumia mfano kwamba wanawake wengi ni kama sanaa nzuri ya mawe yaliyojipanga, katika ulimwengu unao badilika.Kulingana na mada inayo jikita ya masuala ya wanawake kwa siku hizi, ukitazama hali ya sasa  kwa upande wa ajira ya wanawake , hakuna mfumo wa kijamii wa kuwalinda wanawake hata kuhamasisha kwasababu wengi ni waathirika wa kukosa usawa na wanaume hata kama wote wanafanya kazi katika sehemu moja inayofanana.Kuna hata kubaguliwa katika mchakato wa kupata ajira, kwa mfano anapokuwa mjamzito na kujifungua,au anapaswa asaidie watoto wake, au kuwasaidia wazazi au wazee.Ni jambo linalopaswa kuwa muhimu hasa la kazi ya mwanamke katika  kutunza familia,ni zawadi,ni asili ya mwanamke kuwasaidia wengine, kwa njia anasema,ni  changamoto katika mioyo ya waajiri wa kazi binafsi , kutafuta njia za kuwawezesha wanawake wanao fanya kazi wasijisikie kubaguliwa, au kujikuta wanajitoa sadaka kuacha kazi kwa ajili ya uwezo wao wa kuwa mama.Askofu Mkuu anongeza, hata kama kazi yenyewe haiwezi kuwalipa wanawake, kutokana na kutokujulikana katika mfumo wa uchumi, lakini inachangia, siyo tu katika maendeleo kiuchumi kwa kila nchi  bali inasimamia hata nguzo msingi ambayo serikali katika jamii na nchi haina budi kuwasikiliza na kuwafikiria , maana pasipo wao serikali hizo zingekuwa zinatumia huduma za kijamii.

Akitazama juu hadhi ya wanawake, anaschukua mfano wa mwanamke anayepewa ruhusa ya kifamilia, katika kumkuza mtoto wake, au kusaidia mgonjwa na mzee wa familia.Anasema  kutoa ruhusa kwa wanawake ni moja wa jibu ambay inaweza kuwa mwafaka muhimu na hasa kama itasindikizwa na siasa kìjamii, na katika vitengo ambavyo vina msaidia mwanamke anaye jishughulisha katika familia au akiwa nyumbani, kwa namna ya pekee hata katika kuwangaliwa wale wanawake walio zaa nje ya ndoa vilevile wanawake wakimbizi na wahamiaji ambao pia ndiyo miongoni mwa waathirika zaidi na nimasikini.Anaongeza hawa wa mwisho kati yao ndiyo wanapaswa kuheshimiwa hadhi yao na utu wao kwa  kulindwa na kuwawezesha wapete furza bora za kazi yenye adhi.Kwa namna hiyo Askofu Mkuu Auza anasema Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanapaswa kutoa kipumbele zaidi kuwalinda na kuthibitisha hadhi ya wanawake katika nafasi ya kazi, katika familia na mahali pengine, ili waweze kuwa na uwezo , na hasa katika mafunzo, uzalishaji , utunzaji binafsi na uthibiti wa mali wanazozalisha na wakati huo huo  kuwekwa pamoja kwa  kuepuka aina ya unyanyasaji na kunyonywa au biashara ya wanawake na watoto.

 Hali kadhalika Askofu Mkuu Auza agusia suala la uwajibikaji wa wanaume ndani ya nyumba  akikumbusha jukumu la wanaume juu ya mabadiliko ya hali ya kazi ya wanaume . Anakumbusha moja ya maneno ya Baba Mtakatifu Francisko juu ya wosia wa Furaha ya Upendo kwamba katika nyakati ambazo wanawake  wanazidi kushiriki katika shughuli za kitalaam,inawezekana kwa mfano 
Mwanaume akawa mwepesi na kukubaliana na hali ya ajira ya mwanamke.Hiyo ni kwasababu anasema, kwa kawaida wanaume uona vigumu kuchukua wajibu wa kuwahudumia watoto katika shughuli za ndani ya nyumba, na kufikiria kwamba kazi hiyo siyo ya mwanaumea  na  kwamba  kushindwa au kuona aibu. Askofu Mkuu anasisitiza kuwa tunapaswa kuwasaidia pia  watoto kukubali na kuona kwamba ni kama kawaida ya wazazi na hasa kwa wanaume  'kubadilishana',kwa kusaidiana kwa maana shughuli za ndani ya nyumba hazimtolei heshima yoyote kuendela kuwa  baba ndani ya familia na kuwa msingi wa nyumba. Kwa maana nyingine ni kazi za kushirikishana ni wajibu kwa wote wawili ndani ya familia kusaidiana

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

18/03/2017 14:57