Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Maendeleo

Malawi:Kinachobaki ni kupanga yaliyopo na siyo endelevu

Takwimu hizo zinaonesha kwamba familia yenye watu 6, ili waweze kufikia angalau mwisho wa mwezi wanahitaji kuwa na kwacha za Malawi 170,000, wakati kiwango cha chini cha mshahara wa mwezi ni kwacha 18,000. - REUTERS

17/03/2017 16:01

Ni nchi ambayo kwa sasa unafikiria namna ya kukidhi haja kwa siku, kwasababu huwezi kupanga ya wakati ujao.Ni nchi ya Malawi ambayo kwa kipindi sasa wanaongelea juu ya kipeo cha uchumi, siasa na chakula. Ni maneno yaliyosemwa na  Padre .Piergiorgio Gamba alipohojiwa na vyombo vya habari Fides.“Nchini Malawi kipindi cha Kwaresima ni muhimu hata kama hali inabaki katika mtazamo wa hali ngumu kwasababu ya rushwa nchi nzima ambapo haupungui kamwe bali ni kuzidi kuongezeka kila kona.Kwa mfano inabidi kutoa malipo kwa ajili ya kupata huduma fulani, kwa mfano kufunga nyaya za umeme, ni siku 15 hivi hakuna umeme, au badala ya adhabu, wanalipa hongo  wasikamatwe kwa ajili mwendo kasi, yote kulipa tu.Zaidi ya rushwa ,bado kuta tatizo la kuendela kutafutwa watu walemavu wa ngozi kwa kuamini kwamba wakipata viungo vyao watakuwa matajiri”.Anasema Padre Gamba.

Kituo cha utume wa kijamii cha wamisionari wa Afrika huko Lilongwe kila mwezi wanajaribu kuorodhesha takwimu za uchumi.Takwimu hizo zinaonesha kwamba familia yenye  watu 6, ili waweze kufikia angalau mwisho wa mwezi wanahitaji kuwa na kwacha za Malawi 170,000, wakati huo huo kiwango cha chini cha mshahara wa mwezi  nchini Malawi ni kwacha 18,000. Kiasi hicho ni kidogo sana ambacho hakifiki hata moja ya kumi ya kuweza hata kukidhi mahitaji madogo ya familia.Pamoja na hayo taarifa zinasema, matumainimakubwa ni wakati wa mavuno.Kwani Waziri wa Kilimo amesema kutakuwa na ongezeo la asilimia 34% ya mahindi katika masoko ukilinganisha na mwaka uliopita. Lakini takwimu za hatari zinabaki kuwa tishio la wadudu walio shamabaulia mashamaba na kuharibu maeneo ya hekari za ngano bila uwezekano wa kupata dawa yoyote inayouzwa .

Anamaliza Padre Piergiorgio akisema pamoja na hayo ni nchi inayobaki katika mzani wa njaa leo hii na hata siku zijazo. Labda ndiyo maana nchi ya Malawi inashindwa kufikiria  yaliyopita na hata yale endelevu.Kinacho hesabika ni leo hii kama umeweza kuwapo.

 Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

17/03/2017 16:01