2017-03-14 15:57:00

Tangu mwaka 2017 uanze,watu 140 Iran wamehukumiwa adhabu ya kifo!


Katika ripoti ya tisa ya mwaka,juu ya hukumu ya kifo nchini Iran iliyotolewa na Shirika la Haki za Binadamu (IHR) nchini Iran kwa mwaka 2016 linasema watu 530 wamehukumiwa kifo Jamhuri ya kikiislam ya Iran.
Kama takwimu ya ripoti inaonesha idadi ndogo kulinganisha na idadi ya mwaka  juu ya hukumu za vifo zilizotolewa kwa miaka mitano iliyo pita huko Iran,lakini bado ni kuonesha jinsi idadi ilivyo kubwa ya hukumu za vifo katika nchi hiyo.Hata hivyo anaeleza  Mahmood Amiry-Moghaddam,Mkuruguenzi wa Shirika la haki za Binadamu nchini Irani kuwa lipokelewe kwa hali ya uchanya ikiwa na maana ya pungufu ya adhabu ya kifo :lakini pamoja na hayo hakuna vielelezo vya kutosha vya kuelezea mabadiliko ya kisiasa katika Jamhuri ya Kiislam ya Iran ya kuonesha upungufu huo.Kulingana na taarifa , zinazoonesha kwamba kwa miezi miwili ya mwaka 2017 , watu 140 wamehukumiwa adhabu ya kifo.

Katika tukio la kuwakilisha ripoti ya mwaka juu ya adhabu ya hukumu ya kifo nchini Iran kwa mwaka 2016, Mashirika ya Iran juu ya haki za Binadamu(IHR)  na Shirikisho la kupinga adhabu ya kifo (ECPM) walikuwa wametoa ombi kwa nchi za Ulaya ambao walianzisha mazungumzo ya Iran, ili kudai shinikizo la kusitisha adhabu ya kifo nchini humo,na uwepo wa mageuzi zaidi ndani ya mahakama kwa kufuata  viwango vya kimataifa.
Ripoti hiyo pia inalenga kwa umakini juu ya jukumu la mahakama ya mapinduzi , kama vyanzo vikuu vya ujeuri na ukiukwaji wa kesi za mahakama.Ni ndani ya mahakama hasa ya mapinduzi walio husika kwa idadi kubwa ya hukumu za vifo zilizotolewa na kutekelezwa katika kipindi cha miaka 37 nchini Iran.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka wa haki za Binadamu nchini Irani , ni karibu asilimia 64% za watu walionyongwa kwa kipindi cha mwaka 2016 na zaidi ya watu 3,200 katika kumbukumbu ya mwaka 2010 zilizotolewa na mahakama ya mapinduzi.Mahakama ya mapinduzi haina uwazi zaidi kuliko ile ya umma , na waamuzi  wao wanajulikana  kuwa na matumizi mabaya ya madaraka kisheria  kwa hukumu wanazotoa. Kwa mfano mchakato wao ni mfupi kwani unadumu  si  chini ya dakika 15 tu , ukosefu wa upatikanaji wa misaada  ya kutosha kisheria ,kutumia ushahidi wa kulazimishwa na kutumia hukumu kwa njia ya mateso;hizo ndizo baadhi ya tabia na vielelezo vinavyotumiwa na mahakama ya mapinduzi nchini Iran.

Juu ya hukosefu wa mchakato wa haki, Mahmood Amiry-Moghaddam anasema kupunguza adhabu ya kifo ambayo ni endelevu , kwa bahati mbaya haiwezekani mbele ya kesi za  haki mahakamani.Hiyo ni kwasababu mahakama ya mapinduzi ambayo ina wahukumu mamia ya watu wafe kila mwaka , ni miongoni mwa taasisi kuu zinazo wajibika katika ukiukwaji mkubwa nchini Iran ambapo ni lazima kusimamishwa.
Halikadhali Mkurugenzi mwandamizi wa Shirikisho la kupinga adhabu ya kifo Iran , Raphaël Chenuil-Hazana anatoa wito kwa mataifa yote ya kidemokrasia na wadau  kutoka Jamhuri ya Iran walioko Ulaya, ili kufanyike juhudi kubwa ya kupunguza adhabu ya kifo nchini , kwa njia hiyo haki za binadamu ziweza kuwa moja ya mazungumzo baina ya nchi.Kwa kutilia mkazo pamoja na mazungumzo na Iran inawezekana kuifikia mapatano na matoke mazuri.

 Hata hivyo mashirika hayo mawili ya haki za binadamu Iran na (IHR) Shirikisho la kupinga adhabu ya kifo (CPM) wanaungana pamoja kutoa ombi kwa mamlaka ya Iran kumwaachia huru mwana harakati na mtetezi Narges Mohammadi  kuhumiwa miak 16 gerezani  kutokana na kufanya kampeni ya kukomesha hukumu ya kifo. Vikundi na vyama vya Haki za Binadamu wanaunga mkono pamoja tamko hili pawepo na kusitisha ukandamizaji wa vyama vya raia na kesi za jinai dhidi ya wanaharakai wa amani.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.