2017-03-13 17:00:00

Askofu mkuu Lokudu:Uende Chumbani kwako na usali kwa ajili ya amani!


Kama maombi haya yamefanyika kwa dhati, mambo mengi yataweza kujitokeza katika nchi kama vile amani,haki, upendo na mazungumzo ya dhati.Hayo ni maneno yaliyo tamkwa na Askofu Mkuu wa Juba Sudan ya Kusini Paulino Lokudu Loro, wakati wa maombi kitaifa kwa ajili ya kuombea amani nchini Sudan Kusini. Maombi hayo yameagizwa na Rais wa nchi Salva Kiir na kufanyika tarehe 10 Machi 2017 katika maeneo mengi ya nchi.Askofu Mkuu Lokudu anaongeza, kutokana na sala mambo  mengi yanaweza kutokea kama vile uwepo wa Serikali nzuri, usalama na uchumi mzuri kwa wote .
Kardinali akimgeukia Rais wa nchi ;amesema, “uende katika chumba chako na kusali kwa ajili ya amani”, vilevile na kuwataka wote kwamba;  iwapo nchini humo watapuuzia maombi , nchi itaendelea kujikunyata katika mateso, rushwa , kuwakamata watu wasio na hatia , na ukabila. Kwa ishara ya kuonesha maridhiano, Rais Salva Kiir amewaachia viongozi wa Serikali ya Wau Elias Way na msaidizi wake Andrea Dominic , walio kuwa wametuhumiwa usaliti.

Maombi hayo yaliyofanyika huko Juba , yameudhuliwa na maelfu ya watu ,wakiwepo  viongozi mbalimbali wa madhehebu ya wakristo, na waislam,hali kadhalika makutano ya sala ya namna hiyo yameonekana katika maeneo mengi ya nchi hiyo. Hata hivyo hivi karibuni mmoja wa Kanisa Katoliki alikuwa ameonesha mshangao wake juu ya Ras wa nchi kuanzisha suala hili la sala , lakini Maaskofu Katoliki wametumia fursa hiyo kuwataka viongozi wawajibike ,na hasa  viongozi wa kisiasa, kwa namna ya pekee Rais  wa nchi. Askofu Erkolano Lodu Tombe wa Jimbo la Yei , aliwataka viongozi wa Serikali ya  Rais waachilie mbali shauku  ya kupenda mali na  madaraka tu ili utajiri uwe ni kwa ajili ya huduma ya wazalendo.Na Askofu Baran Eduardo Hiiboro Kussala, wa Jimbo la Tombura/Yambio , alimtaka Rais Salva Kiir awe na mwendendo wa Baba wa Taifa , ambaye anawatunza wazalendo wake, kwa kuhakikisha kwamba wote wanashiriki mazungumzo ya kitaifa.

Vita vya wenyewe kati ya Rais Kiir na Makamu wa Rais mstaafu Riek Machar vimeipigisha magoti  Sudan ya Kusini. Ni nchi ambayo Umoja wa Mataifa ulitoa tamko la dharura  tangu mwaka 1945 hadi leo hii.Vita na ukame vimeharibu kilimo na kuwaweka watu katika hali mbaya ya maisha  ya mamilioni ya watu wa Sudan. Hali kama hiyo pia inafanana na nchi nyingine za dharura zilizo kwenye orodha ya umoja wa mataifa kama vile Yemen , Somalia , Nigeria ya Kaskazini mashariki.Katika nchi hizi nne ni zaidi ya milioni 20 ya watu wako hatari ya kufa kwa njaa, iwapo msaada wa dharura hautatolewa.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili a radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.