2017-03-11 16:18:00

Tutakuwa na ushindi iwapo vijana wote watarudi majumbani kwao


Maaskofu Katoliki wa Nigeria wametoa ujumbe wa kichungaji  unaohusu kukabiliana changamoto za sasa zinazoathiri nchi yao.Hizi ni pamoja na masuala ya dhana ya uraia, utakatifu wa maisha ya binadamu, masuala ya usalama kwa ujumla kuongezeka kwa makundi ya wanamgambo na misingi ya kikabila, pamoja na changamoto za demokrasia.Masuala mengine ni kuhusiana na haja ya haraka ya kutoa ufumbuzi wa vijana walio kata tamaa na pia mapambano ya kitaifa dhidi ya rushwa.Ujumbe huo ulitiwa na saini na Askofu Mkuu Jos ambaye ni Rais wa Baraza la maaskofu Katoliki wa Nigeria (CBCN), Ignatius Ayau Kaigama pamoja na Askofu William Avenya, wa jimbo la Gboko na  Katibu wa CBCN na aliye toa habari hizi katika vyombo vya habari ijumaa 10 Machi 2017.Ujumbe huo unasema kwamba:

Tangu mwisho wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kutisha nchini Nigeria, ambavyo vimekuwa vya kihistoria katika nchi yetu, suala la uraia limekabiliwa na matatizo zaidi.Tumeshuhudia kuona wanamgambo wa makabila  wanachomoza kila eneo na kueneza vurugu zao na uharibifu dhidi ya jamii ya nchi.Tumeshuhudia kuongezeka kwa sera za utambulisho kisiasa kwa madai ya tumbo la ukabila.Hivyo badala ya kupumua hewa tuliyopewa bure ya demokrasia tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi, mapafu yetu yanavuta hewa ya vurugu.Ukosefu wa usalama katika nchi umegeuka uwanja wa michezo ya vita.Kukabiliwa na ukosefu wa ardhi, ukosefu wa makazi na wagonjwa ni wengi, watu wengi kwa sasa  hawajisikii kuwa ni raia wan nchi ya Nigeria.

 
Maaskofu  hao wanatoa wito wa maneno na hisia zao kwa waandaaji wa katiba ambao walikuwa wametoa ahadi ya kuhakikisha kwamba uhuru utadumu kwa watu kutokana na serikali kuwa na uhalali wake.Pamoja na hayo Katiba hiyo inaweka wazi usalama na ustawi wa jamii ya watu kuwa ni madhumuni msingi ya serikali.Katika katiba hiyo inaonesha dhana ya raia wa nchi  ni kuhakikisha wanapata haki ya utu , uhuru wa kujieleza, uhuru wa dini na dhamiri.Hali kadahalika wanasema “Tunatambua uhakika wa uhuru wa kutembea , lakini raia wa kawaida sasa anajua kwamba huru huo badala yake ni kesi.Kwa suala la maisha wanasema” tumegundua kabisa utakatifu wa maisha ya binadamu umekuwa kinyume na kanuni mbili tulizo nazo ya utamaduni wa jadi na hisia za kidini.Haijawahi kuonekana maisha ya namna hii.Vurugu za kila siku na zaidi watoto na vijana wanapoteza maisha bila kuwa na hatia au kwa kutazama wazazi wao wanachinjwa na mali zao kuharibiwa.Chanzo cha vurugu hizi zilianzishwa na mlipuko wa Boko Haram.Tunakumbuka kwamba hasa mauaji ya mamia ya watu huko Zaria Desemba 2015, mauaji ya watu kusini mwa Kaduna na kuwakuta wafugaji na wakulima wanaoishi katika nyika, maelfu ya watu wameuwawa. Tunaomba pumziko la roho za wafu kwa Mungu na pia kuwafariji wafiwa na kuponya waliojeruhiwa.

Tunatambua mafanikio yaliyopatikana chini ya utawala wa sasa katika udhalilishaji na uasi wa Boko Haram. Ingawa serikali ya shirikisho imetangaza kushindwa kiufundi kwa jeshi la Boko Haram, hatuna sababu ya kuamini kwamba hawawezi kutrudisha upnga upya na hasa  tunapoendelea kushuhudia ukatili wao na kuchinjwa wananchi wasio na hatia.Tunawapongeza serikali ya shirikisho kwa ajili ya mafanikio yaliyokwishapatikana, ikiwa ni pamoja dharura kwa baadhi ya wasichana Chibok.Lakini tutakuwa na  ushindi kamili  iwapo tutaona mabinti wote wamerudi nyumbani.Zaidi nikuhamasisha serikali ya shirikisho ili kuharakisha mchakato wa kuwarejesha watu wetu.Zaidi ya miaka, tumeshuhudia kutishwa na kutendewa vitendo vya kinyama watu wetu na wasomi nguvu ambayo imeendelea kutojali usafi na heshima ya kila raia wa Nigeria. Kwa hiyo sasa tunajua kuwa kizazi kipya cha vijana wanakabiliwa na maisha ya kutokuwa na uhakika, hofu na ukiwa.

Wahitimu hawawezi kupata ajira,wazazi hawana kazi, hawana pensheni na wanakabiliwa na hali ya kudhoofika  kuchumi.Halikadhalika wanasikitishwa na vijana kukabiliwa na hatari nyingi. "Tumepoteza watoto wetu mitaani, kujiingiza katika makundi na madawa ya kulevya. Muda mrefu  vijana hawa wana zurura mitaani na kuwa tegemezi sana kwa wazazi wao, kutokana na kubaki muda mrefu bila ajira, wanajiunga  na vikundi  vya kiuhuni, kubaka, madawa ya kulevya na magenge ya biashara haramu ya binadamu,au kujiunga na Boko Haram.

Maaskofu wanasema  taifa letu ni  lazima kubadili mwelekeo huu mbaya katika jamii yetu, na  wanatoa maombi kwa kusema: Wakati tukiendelea kuomba kwa ajili ya kupona haraka kwa  Rais wetu kwa umoja wa taifa letu, ni lazima kutambua kwamba kuna changamoto ya kuweka rasilimali yetu kubwa katika huduma ya watu wetu. Hakuna tena kuhairishwa kwa muda usiojulikana,mgawanyo sawa wa rasilimali zetu kwa manufaa ya lazima kwa  lengo la uhakika kwa wale ambao wanamiliki imani hii. Hii itasaidia kurejesha utu wetu kama binadamu na uadilifu wetu kama taifa na uaminifu wetu kama raia. Mungu abariki Nigeria.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.