2017-03-09 16:53:00

Uhuru wa dini ni haki kwa kila binadamu kuabudu bila vikwazo!


Hotuba ya Askofu Mkuu Jurkovic Ivan mwakilishi wa Baraza la Kudumu la Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko Gineva kuhusu kuheshimiana na  amani kama hali ya amani na utulivu kati ya madhebu ya dini na imara.
Pamoja na jitihada nyingi ili kukuza na kuimarisha haki ya msingi ya binadamu ya uhuru wa dini kweli tunashuhudia kuendelea kuzorota kwa sababu ni wazi kwamba upo ukosefu wa kuhamasha haki katika maeneo mengi duniani.Suala la dini kwasasa limekuwa jambo nyeti la kufikiria .Hii udhibiti katika mifumo wa  ndani na nje ya nchi  kimataifa katika sheria kama vile kwenye maslahi mchanganyiko ambayo utata umeibuka ndani ya taasisi za jumuiya ya kimataifa.Askofu Mkuu Ivan katika hotuba yake anasema,suala la uchaguzi wa Imani na matokeo yake ni mali za madhehebu ya dini kwa kila ngazi ya maisha, mazingira ya kijamii na katika mzunguko kisiasa.Kwa njia hiyo ni  jukumu la wote  katika kukabiliana na changamoto za jamii yetu kwa njia msingi kila siku.Leo zaidi dini imechukua jukumu muhimu kutokana na uhusiano mgumu uliopo kati ya uchaguzi binafsi na imani pia namna ya kujieleza kwa umma.Askofu Mkuu Ivan anasema, kutokana na athari hizo, uchaguzi na mazoezi ya imani ya mtu lazima iwe huru bila vikwazo au kutumia nguvu.


Wakati hali ya uhuru wa dini katika dunia inaendelea kuwa tishio ,hasa wakati huu ambapo kesi nyingi za unyanyasaji dhidi ya wakristo na jumuiya nyingine za kidini, bado lakini kuna juhudi na nguvu ya kuashilia uangalizi juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu na wahusika wa unyanyasaji.Juhudi hizi zinawakilisha matumaini kwamba jumuiya ya kimataifa itaguswa na kuingilia kati ambapo kwamba hajapoteza dhamiri yake.
Katika kipindi cha miaka iliyopita, mamilioni ya watu wamelazimika kuacha  makazi yao au kulazimishwa kuondoka katika ardhi za mababu zao. Wale ambao wanakaa katika maeneo yenye vita au maeneo yanayodhibitiwa na makundi ya kigaidi wanaishi chini ya tishio la kudumu la ukiukwaji wa haki za binadamu, kama vile  ukandamizaji na kwa walio wengi ni wakristoHali ya Wakristo katika nchi za Mashariki ya Kati, Makanisa na makaburi ya kale ya dini zote vimeharibiwa ni  nchi ambayo watu wameishi kwa miongo na wana haki ya kubaki,kwa namna hiyo inafufua wasiwasi mkubwa anasema askofu Mkuu Ivan.Kuna sababu zaidi na zaidi za hofu na umakini kwa mustakabali wa jamii ya Kikristo kwaba ni zaidi ya miaka elfu mbili ya uwepo wao katika kanda hizo, ambapo Ukristo umekuwa na nafasi yake kamili ya historia yake ya muda mrefu.Kwa njia hiyo mateso dhidi ya Wakristo leo hii kweli ni mbaya zaidi kuliko ya miongo  ya kwanza ya Kanisa, na kuna mashahidi wengi zaidi wakristo leo kuliko enzi za zamani.

Hali kadhalika hotuba inaeleza kuwa ulinzi ni moja ya mambo muhimu yanayotuzunguka na mjadala wowote juu ya uhuru wa dini kama haki za msingi za binadamu kwa sababu ni asili ya binadamu. Kwa njia inabidi kutumia jukumu la kimkakati katika kutathmini na kuhakikisha tahadhari sahihi hasa katika kuhakikisha unatolewa na mamlaka ya umma. Tafsiri hii ni kuonesha mchakato wa uthibitisho wa haki za binadamu ambao umekuwa na sifa ya historia ya miongo michache ambayo imewekwa kwa ajili ya binadamu mwenyewe/ haki zake ziwe kitovu cha hatua za kisheria, kisiasa, kitamaduni na kidini. Kwa hakika, uhuru wa dini inatoa changamoto la kujiuliza swali juu ya haki za binadamu, ambayo ina ongoza kanuni na msingi wa dhana ya sheria za kimataifa za haki za binadamu.Uhuru wa kidini ni haki ya kibinadamu ambayo huonyesha mwelekeo juu ya hadhi ya binadamu, uwezo wa kutafuta ukweli unaoendana na hilo kwa kutambua hali ambayo ni muhimu kwa uwezo wa kuwapeleka wote wa kwa nguvu ya mtu mwenyewe.Zaidi itambuliek kuwa uhuru wa kidini siyo  tu  imani binafsi au kuabudu,bali ni uhuru wa kuishi, wote faragha na hata hadharani, kwa mujibu wa kanuni za maadili kutokana na kanuni za dini. Hii ni changamoto kubwa katika dunia ya utandawazi ambapo imani dhaifu pia imepunguza kiwango kwa maadili na kwa jina la dhana potofu ya kuvumiliana napia kusababisha wale wanaotetea imani yao kuishia kuteswa.

Uhuru wa dini kwa hakika una maana haki ya kuabudu Mungu, peke yake na katika jamii, kama dhamiri zetu zinavyotushauri. Lakini uhuru wa dini pia ni asili yake,inapitia katika maeneo ya ibada na nyanja binafsi ya watu na familia. Mila zetu mbalimbali ya kidini zinatumikia jamii hasa kwa kutoa zaidi ujumbe kwa kuinjilisha.Uhuru wa dini unawaalika watu na jamii kuabudu Mungu, asili ya maisha yote, uhuru na furaha. Unatukumbusha kipengele madhubuti cha uwepo wa binadamu na uhuru wake usio punguzwa katika uso wa kila mtu anaye dai kwa nguvu. Mila zetu tajiri za kidini zinatafuta kutoa maana na mwelekeo,yaani kutokana na nguvu ya kudumu katika  kufungua upeo mpya, ili kuchochea mawazo, na kupanua akili na moyo.Halikdahali unatoa wito kwa ajili ya uongofu, maridhiano, wasiwasi kwa mustakabali wa jamii, kwa kujitoa sadaka  katika huduma kwa  manufaa ya wote, na kuwa na huruma kwa wale wanaohitaji. Katika moyo wa kazi ya kiroho ni kutangaza  ukweli na hadhi ya binadamu na haki za binadamu. Katika dunia ambapo kuna aina mbalimbali ya dhuluma, kutafuta kukandamiza uhuru wa dini, au kujaribu kupunguza thamani ya tamaduni bila haki ya sauti katika umma, au kutumia dini kama kisingizio cha chuki na ukatili. Ushauri wa Askofu Mkuu Ivan kwamba ni muhimu wafuasi wa dini mbalimbali kuungana sauti zao kwa kutoa wito wa amani, uvumilivu na kuheshimu hadhi na haki za wengine.

Aidha anasema Askofu Mkuu Ivan kuwa mwelekeo wa utandawazi ni mzuri, unatuunganisha, unaweza kuwa na sifa. Lakini kama unataka kujifanya kwamba wote tuwe sawa, ni kuharibu ule upekee wa kila mtu na kila watu. Tunaishi wote duniani kwa kile kinachoitwa "utandawazi wa dhana ya teknolojia ambayo kwa uangalifu wake inalenga juu ya mshikamano au mwelekeo mmoja na inataka kuondokana na tofauti zote za mila na desturi katika jitihada za umoja wa juu juu tu. Kwa njia hiyo dini zina  haki na wajibu wa kuweka wazi kwamba inawezekana kujenga jamii ambayo hali nzuri ya vyama vingi vikaheshimu tofauti na maadili yao kama vile "thamani ya kushiriki  katika kutetea heshima ya binadamu kwa njia  amani katika dunia yetu yenye wasiwasi








All the contents on this site are copyrighted ©.