2017-03-09 16:13:00

Hata sisi tunamsaliti Yesu kama Yuda kwa njia ya matendo yetu maovu!


Mafungo ya kiroho ya Baba Mtakatifu Francisko na wenzake, huko Ariccia bado yanaendelea kwa tafakari ya nne na ya tano kufikia Jumenne jione na Jumatano asubuhi ya 8 Machi 2017, Padre Michelini, anawatafakarisha juu ya Sura ya Yuda Iskarioti baada ya kumsaliti Yesuanapoteza imani kwa Bwana hadi kufikia kujiua. Anasema ni tukio la aibu ambalo lakini hakuna woga kwa Kanisa kushindwa kukabiliana nalo kwa njia ya matendo ya huruma. Aidha Anakumbusha historia ya Yuda alipokimbia kurudisha vipande 30 vya sarafu kwa watesi wa Yesu wakakataa ndipo zikaishia  kujenga makuburi ya watu wageni huko Yerusalem.

Katika habari za kila siku kwenye mitandao zinaonesha kesi nyingi za mauaji na kujiua,akitoa mfano wa hivi karibuni wa kijana wa miaka 16 aliyejiua kwasababu ya kushitakiwa na mama yake kwa polisi kwasabubu ya tatizo la kutumia madawa ya kulevya.Lakini kifo cha Yuda kinagusa moja kwa moja wote, anasema Padre Michelini kwa tafakari ya Injili ya Matayo 27,1-10. Kama injili isingetupatia nyenzo za kutosha kujua sababu ya uamuzi huo, tungefikiri  kwamba amepoteza imani kwa Bwana .Vile vile anatoa mfano wa mwandishi wa kifaransa Emmanuel Carriere  katika kitabu chake  (Royaume 2014) ambaye hakuweza kujisifia  uzoefu wake wa kupotea bali nasema wazi kuwa kwa kipindi fulani katika maisha yake , alikuwa mkristo, lakini kwa miaka mitatu tu na sasa siyo tena mkristo.anaongeza, ninakuachilia mbali Bwana , lakini wewe huniachi.

Padre Milcheli anataka kusema kwamba yeye ameweza kucha imani katika Kristo baada ya kumpenda bila kumuona. Lakini kwa upande wa Yuda ni tofauti kwani yeye alikuwa karibu na Yesu, alimjua kama nyama na mfupa wake. Licha ya hayo Yuda alikuwa mfuasi wake mkerereketwa, aliyesikia maneno yake , aliona miujiza yake.Anaendelea Padre Michelini akitumia mwandishi mwingine wa kitabu kwamba Yusa alikuwa tayari kumfuasa Yesu, lakini kuna jamba fula ni likamwingilia kwa ghafla na kumfanya apoteze imani kwa Yesu na asimwamini tena. Pamoja na hayo Padre Michelini anasema  sababu hizo hazikuandikwa katika injili , ambapo hata Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto wa kumi na sita aliwahi kusema kuwa kile kilichojitokeza kwa Yuda ni zaidi ya saikolojia isiyoelezeka.Kwa upande wa wa Padre Michelini anafikiria kwamba Yuda alifikira kumkabidhi Yesu kwa wenye madaraka ya dini ili aweza kuwaonesha jinsi alivyo masiha wa Israeli. Kwa njia hiyo Yuda hakuweza kugeuza uso wa Yesu kama sura ya masiha wa kufikirika,y aani mkombozi , mpiganaji na mwanasiasa.Kwa kuonesha hiyo Injili ya Matayo  inasema mitume wake wanamwita Yesu Bwana: ni Yuda peke yake anamwita mara mbili Rabbi maana yake mwalimu, kwasababu yeye anamwona Yesu tu  kama mwalimu na wakati wa kumkabidhi anataka kutumia nguvu afanya kile anachotamani.

Padre Michellini anatoa swali la kujiuliza, ilitokea vipi mtu aliyechaguliwa na Yesu afikie hatua ya kupoteza imani hadi hasimtambue kabisa?ni swali ambalo hatuwezi baki tofauti. Mwandishi wa Kitabu Guardini anafikiria kuwa mchakato huo ulitokana na kushimana na fedha .Pamoja na  haya anaelezea kuwa wote tunamwacha Yesu , kwasababu hata Petro alimkana.Kwa njia hiyo  anawaalika wote kujiuliza kila siku katika maisha yetu kuna hali ya kumwacha Yesu , hali ya kujifanya tunajua zaidi, hali ya kujifanya watakatifu, katika wajibu wetu, namna ya kupenda ubatili , kwenye anasa, kutafuta fedha , kutafuta ulinzi , katika chuki  na kulipiza visasi. Kutokana na mambo hayo hatuwezi kujitetea na kukasirikia usaliti, kwababu hata Yuda yupo ndani ya maisha yetu wenyewe.

Kwa kurudi katika tendo la Yuda kujiua mwenyewe   ni mojawapo ya mambo matano yanao ongelewa katika Biblia bila kutaja msukumo wa kujiua , ambao unawakabili wanaume na wanawake kwa sasa. Msukumo huo ni zaidi ya kukata tamaa , tendo hili la kutisha linaelezea , sikitiko, majuto, ufahamu na kutubu dhambi zilizofanyika, anasema Padre Michelini. 
Lakini Padre Michelini anabainisha jambo jingine akitazama Riwaya moja ya mtunzi Alesandro Manzoni, anamtolea sifa kwa utunzi wake. Kwani katika Injili haijulikani ni nani alikwenda kumafuta Yuda baada ya makuhani kumfukuza vibaya wakisahu jinsi walivyokuwa wachungaji.Lakini katika sura ya 21 ya Riwaya ya Manzoni inaonesha juu ya mtu mmoja anayelipa kwasababu ya makosa yake.Hadi kufikia tendo la kukutana na Kardinali Federico Borromeo anaye muomba msamaha kwa ajili ya kuotkwenda yeye kukutana kwanza.Anaongeza hiyo ni pamoja na wito wa Baba Mtakatifu Francisko anavyo toa wito ya kwamba, Kanisal inapaswa kwenda kukutana na wenye dhambi anasema Padre Michelini. Kwa upande wa Yuda muda huo alikabiliana na ugumu,makosa yake,hata watesi sasa wanageuka kuwa maaduni wake, hadi kufikia hatua ya kukimbia na kujiua.

Kwa njia hiyo Padre Michelini anadhibitisha kwamba ni muhimu Kanisa kutoka nje , kutelemka njiani ili kukutana na wenye  dhambi kwa sasa, katika jela na hata mahali ambapo wengine hawapendi kutama;kama  vile kwenye virabu, na maeneo ya mzuki, akitoa mfano dhati juu ya ndugu  zake wa shrika la ndugu wadogo wanavyo fanya  uzoefu wa kwenda kucheza muziki kwa ajili ya kuinjilisha , na yeye kama profesa anasema ninawatania.
Lakini hali halisi ni kwamba  katika Injili ya Matayo inatoa ushauri wa kwenda hata sehemu zenye kuleta kashfa , zenye kuleta matatizo , bila kuficha chochote , kwani anadhibitisha hili kwa kusema kuwa hata Injili inaleza wazi ya kwamba kati ya ndugu wa Yesu yupo hata Kahaba.


Wakati huo huo Tafakari ya nne ya mchana wa Jumanne tarehe 7 machi 2017 Padre Michlini aligusia sala ya Yesu wakati yuko Getsemani (Matteo 26, 36-56) ,anawashauri waende kwa moyo wote katika bustani ya Getseman , kwa uvumilivu  juu ya huzuni wa Yesu; kuomba jinsi gani ya kukabiliana na huzuni na mateso ya wengine,au  kama wako tayari kukesha kwenye sala , au ndiyo wanaanguka kishawishi cha usingizi.Suala jingine ni la tafakari ya mchana ni kuweza kutambua utashi wa Bwana.Kwa namna hiyo Padre Michelini anasisitiza kuwa ni muhimu kabisa kutambua utashi wa ukombozi na hasa namna ukamilifu kwasababu Mwenyezi Mungu anaalika  wote kwa huru kwasababu ni viumbe vyake ,pamoja na kwamba yeye baadaye Mungu anaweza hata kubadilisha mawazo  kwa kutazama historia ya Yona (3, 10).Anasema unaweza kutubu, au kuongoka  kama vile walivyo ongoka  wakazi wa Ninawi . Iwapo Mungu anabadilisha, Padre Michelini anasisitiza ni jinsi gani Kanisa lake lisibadilike tunawezaje kubaki tumemama na ugumu wetu.Padre Michelini ameanza na jinsi ya kukabiliana na sala ya Yesu alipokuwa mlima wa Mizeituni huko Tabor.

Kuna hali mbili zinazojitokeza katika mlina na zinafanan na kustaajabisha, hali ya kwanza inaonesha ule  uvumilivu, maana Yesu amejaribiwa kutokana na kwamba  hata Petro na wenzake hawakutambua maana ya tangazo la mateso na kifo chake huko Yerusalem, pili amewatangazia mara ya mmoja yule atakaye msaliti .Lakini pamoja na hayo matukio mawili aliyo watangazia, bado mitume hawajatambua kitu gani kinatukia.Katika tukio la kwanza mlimani Tabor sauti ya Baba yake inamtuliza mwanae.Tukio la sauti ya Baba lipo katika Injili zote ispokuwa ni Luka anaelezea juu ya nguvu na mapambano ya malaika, lakini auti haiskiki. Yesu ndiye anaye toa sauti akikubali kwamba itimizwe mapenzi ya Baba yake.Lakini mapenzi haya haina maana ya kifo cha mwanae , bali ukombozi wake, kama alivyo andika mwandishi wa kitabu Guardini akieleza Bwana; Yesu alikuja kwaajili ya ukombozi  watu wake, kwa ajili ya ulimwengu .Kwa namna hiyo alikuwa atimize imani na upendo ambao ulikuwa umepungua .

Halikadahalika Padre Michelini anaeleza hata msemo wa Yesu juu ya mauaji katika shamba la mizabibu. Ni Baba anaye mtuma mwanaye akifikiria ataheshiwa .Lakini habari njema na Yesu mwenyewe hawa kupokelewa , hivyo ufalme utapita kwa namna nyingine ya Yesu kwenye bustani ya Geseman, anaitwa na kukubali.Aidha Padre Michelini anatafakari juu ya Teolojia ya  aina nyingine akisema tuite aina ya B, ya kwamba hata mbele ya Yeu kukataliwa na watu wake,yeye hasimami bali anakubali hatua nyingine yaani kupokea sadaka yake.Kwa maana hiyo Yesu anawaonesha mitume wake wafanye hivyo alivyo fanya Getsemani kwa matendo ya  maombi ya Israeli, kusikiliza na kupenda Mungu kwa moyo wote , kwa nguvu zote hadi kutoa maisha . Anasisitiza siyo tendo la nadharia bali ni hali halisi yak ila siku.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.