2017-03-07 13:10:00

Kuna watu wanakufa kwa baa la njaa nchini Somalia!


Waziri mkuu wa Somalia Bwana Ali Khaire anasema, kuna watu wanaendelea kufariki kutokana na baa la njaa nchini Somalia! Katika kipindi cha siku chache zilizopita, watu zaidi 110 wamepoteza maisha kutokana na njaa kali hasa katika mkoa wa Bay, Kusini Magharibi mwa Somalia. Ukame wa muda mrefu unatishia usalama na maisha ya mamilioni ya wananchi wa Somalia.  Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba, zaidi ya watu milioni tano kwenye Ncho ziliko kwenye Pembe ya Afrika wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula unaotishia usalama na maisha yao na kwamba, wanahitaji chakula cha msaada wa dharura. Hivi karibuni, umati mkubwa wa wananchi ulivamia mjini Mogadisho ili kutafuta chakula. Takwimu zinaonesha kwamba, watoto wanaokabiliwa na utapiamlo mkali kwa sasa wamefikia zaidi ya watoto 360, 000 na kati yao 71, 000 wanaendelea kupoteza maisha pole pole kila sikui!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.