2017-03-07 17:03:00

Mabadiliko ni lazima katika shughuli za kichungaji nchi Takatifu


Kweli kwaresima ni safari ya uongofu kwetu sisi maaskofu , mapadre wa Kipatriaki sisi ni miongoni mwa wenye dhambi ambao tunaomba huruma ya Mungu , na kuomba neema ya kubadilika.Makosa yetu na imani yetu potofu ziko wazi mbele ya  macho yetu .Haya ni maandishi ya Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa msimamizi wa Kitume katika nchi Takatifu katika barua yake kwa Jimbo akiwambia waamini wake ambapo ametimiza miezi 7 tangu achukue madaraka ya utume wake na matatizo ambayo wanakabiliana nayo.Anasema kwa miaka 170 ya Kipatriaki imekuwa na jukumu muhimu na bado upo umuhimu katika maisha ya Wakristo wa nchi takatifu.Parokia zetu , shule zetu na taasisi nyingine zimechangia sana katika maisha ya Wakristo katika nchi hii na kuhimarisha ushuhuda wetu kwa Kristo aliekufa na kufufuka .Pamoja na hayo kumekuwa na makosa ambayo yanaumiza maisha ya Kipatriaki kwa upande wa kifedha na kiutawala hasa kuhusu Chuo Kikuu .

Tumekosea katika baadhi ya maeneo muhimu labda ni kutokana na kutoelekeza nguvu ya kutosha juu ya dhamira yetu msingi. Kuhubiri Injili na kujitolea zaidi wenyewe katika masuala ya kichungaji, anadhibitisha Askofu Mkuu Pizzaballa ambaye pia kwa siku za hivi karibuni alikutana  na mapadre, watawa na walei alipokuwa katika matembezi ya kichungaji katika sehemu nyinyi za Jimbo.Kwa hakika alikuta hali ambayo inapaswa kushughulikiwa kwa uaminifu , ujasiri ,uamuzi  na upendo wa kindugu. Wiki iliyopita katika kushughulikia suala hilo kikamilifu , Askofu Mkuu Pizzaballa alikutana na makasisi wote wa Kiaptriakia kutafakari juu ya wito na utume wa makasisi na pia kutafakari juu ya makosa ambayo yamesababisha hali mbaya na zaidi hasa kiuchumi.

 Kuna mambo mengi ya kufanya anasema Askofu Mkuu Piazzaballa , ni wakati wa kuanza kazi ya mageuzi, ukarabati wa baadhi ya sekta za utawala wetu na siyo hayo tu.Miongoni mwa mengi yaliyojitokeza, tumeamua kuzingatia zaidi katika shughuli zetu za kuchungaji na kufungua kwa mfano ofisi mpya za jimbo kwaajili ya shughuli za kichungaji na kuratibu kwa kuunganisha huduma zetu katika uchungaji wa jumuiya ndani ya jamii.Njia tuliyo nayo mbele yetu itakuwa ngumu bila shaka kwa sababu ya vikwazo na changamoto.Lakini kama tunafanya kazi pamoja , na kulenga dhamira yetu ya kumtumikia Kristo katika Kanisa lake , tutaweza kushinda hata kipindi hiki kigumu, anasema. Anahisi kwamba mapadre wake wako tayari kpambana vita hivi kwenda mbele kwa ujasiri hata katika vipingamizi vilivyopo katika njia hiyo.
Na mwisho Askofu Pizzaballa anawaalikwa waamimi wote  kusali kwaajili ya maaskofu makasisi , watawa wote , walei, vijana , wazee ili kuweza kufanya kazi pamoja kwa ajili ya nchi takatifu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.