Jinsi gani ya kutambua wito wa Kristo kwenye zama za mitandao ya kijamii? Jinsi
gani ya kuwaongoza kwenye utambuzi wa miito , na namna ya kutofautisha , sauti za“uvumi
mwanana wa upepo miongoni mwa sauti nyingi zitolewazo na makampuni ya vyombo vya
habari . Hayo ndiyo masuala ya mkutano juu ya vijana utakao fanyika Barcelona kuanzia
tarehe 28-31 Machi 2017 kwa mada “ kutembea pamoja nao” kutoka katika Injili ya
Mtakatifu Lk 24, 15.
Mkutano kuhusu namna ya kuwasindikiza vijana ili waweze kujibu wito wao kwa kristo
katika uhuru umeandaliwa na Baraza la Maaskofu wa Ulaya , kwa ushirikiano wa Baraza
la maaskofu wa Huspania na Jimbo Kuu la Barcelona.
Washiriki 200 na kati yako wapo maaskofu , wahusika wa masuala ya kichungaji kwa
vijana shuleni , vyuo vikuu, miito katekesi ,hata mashirika mengine ya utume wa Kanisa
kama vile chama cha Emaus, ambapo wataongozwa na tafakari ya Injili .Pia miongoni
mwa wengi ni Makardinali Angelo Bagnasco na Vincent Nicholas Rais wa Baraza la Maaskofu
Ulaya na makamu wake, Pia Askofu Mkuu wa Jimbo la Barcelona Juan José Omella Omella.
Taarifa zinasema kuwa mada inayohusiana na vijana na changamoto ya kuwasindikiza kwenye
mantiki ya sasa ya kijamii ndiyo zitakuwa mada motomoto kwa siku nne katika kubadilishana
mawazo na hasa njia bora na uzoefu miongoni mwa washiriki.Pamoja na hayo, maadhimisho
ya ibada za misa , sala na kuabudu vitawaongoza kwa siku hizo nne . Ili kutoa maana
zaidi kwa mfano muhimu wa mapendekezo ya kutangaza Injili washiriki hao pia watafanya
ziara katika familia takatifu.
Mtazamo wa Mkutano huo ni wazi unaakisi tayari maandalizi ya Sinodi ijayo kuhusu Vijana iliyotangazwana na Baba Mtakatifu Francisko kufanyika Vatican Oktoba 2018 ikiwa ni mada juu ya vijana na wito.Matunda ya kazi ya mkutano wa Barcellona yatapelekwa moja kwa moja kwa Mababa wa Sinodi.Halikadhalika inaleta maana kubwa suala la ushiriki wa Kardinali Lorenzo Baldisseri, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu , ambaye atapata fursa ya kutoa machache ya kusema wakati wa kubadilishana mawazo na wahudumu wa kichungaji kwa vijana wakati wa Mkutano huo.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican.
All the contents on this site are copyrighted ©. |