2017-03-03 14:52:00

Uvunaji duniani ni mzuri lakini kuna njaa katika nchi zenye vurugu


Ni kwa mujibu wa ripoti  ya FAO liyotolewa Alhamisi 2 Machi 2017 ya matarajio ya mazao na hali ya chakula inasema,makusanyo ya vyakula kwa kwa ujumla duniani ni mazuri bali tatizo ni hupatikanaji na mgawanyiko katika maeneo yenye vurugu za wao wenyewe, wakati huo  na ukame unazidi kuongezeka katika usalama wa vyakula kwenye maeneo ya nchi ya Afrika ya Mashariki.
Ni karibu nchi 37 zinaomba msaada wa chakula , na kati ya hizi  28 ni nchi za Afrika , ambazo ukame unazidi kudumu kwa muda mrefu, ulio sababishwa na mvua za Elnino na kusababisha uvunaji mdogo kwa kwa mwaka 2016.Pamoja na hayo, hata kama kuna matokeo mazuri ya uvunaji kwa upandea wa kilimo cha Afrika ya Kusini , bado kuna vurugu na ghasaia zinazo sababisha kuoengeza idadi kubwa ya wengi kuwa na baa la njaa duniani.Kwa sasa nchi ya Sudan ya Kusini inaongoza kuwa na dharura ya usalama na pia vyakula ,ikiwa pamoja na nchi ya Nigeria ya kaskazini , Somalia na Yemen.
Hali hii haijawhi kutokea naana hii ya kuweza kukakabiliana na hali ngumu ya njaa na hasa kwa matukio yote mawili kufuatana.Ni maneno ya Kostas Stamoulis muhusika katika Ofisi ya Mkuruguenzi Mkuu na Mkuu wa ofisi ya Uchumi na maendeleo ya jamii wa FAO.Anaongeza,  hii ni hali ambayo inahitaji matendo ya haraka ili kuweza kutoa huduma ya vyakula , na hata zana za kuweza kuwasaidia kwa kuzuia aina nyingine inayoweza kujitokeza katika maisha endelevu.


Nchi ya Sudan, watu 100,000 wanakabiliwa na njaa  katika mikoa ya Leer na Mayendit.Kwa ujumla ni karibu watu milioni 4,9 na ambao  wanakumbwa na hali ya kipeo cha njaa na ukame, wakati huo namba inakaribia kufika milion 5.5 kwa namna hiyo ni kusema nusu ya watu wa nchi hiyo kufikia mwishoni mwa mwezi Julai wote watakuwa wamekonda kwa njaa.Kwa upande wa Nigeria milioni 8,1 ya watu wako mashakani nao kwaajili ya ukosefu wa vyakula, nao wanahitaji kwa haraka chakula  na zana za kuwalinda.Hali hiyo inajitokeza kutokana hukusanyaji mdogo wa vyakula mwaka jana kwasabau ya vurugu na kuanguka kwa uchumi katika nchi hiyo.Nchini Yemen milioni 17 ya watu,ni maana ya kusema robo tatu ya watu wote wa nchini humo nao wako katika hali mbaya ukosefu wa chakula.Nchini Somalia, vurugu , ghasia na pia ongezeko la njaa vimeongezeka mara dufu kwa miezi sita , kwa sasa ni takribani ya watu milioni 2,9 wenye kusadikika katika hali mbaya ya ukosefu wa vyakula.

Ukame umeharibu mashamba ya ulizi ,wachungaji , kwa mara tatu wamekosa vipindi vya mvua ambavyo vimesababisha kupungua kwa mazao ya kilimo hasa maeneo ya kusini na kati kwa asilimia 70 %ukilinganisha na hali halisi.Migogoro na machafuko ya kiraia katika nchi ya Afghanistan, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Iraq, Myanmar na Syria imesababisha ukosefu wa chakula kwa mamilioni ya watu na pia kuleta madhara kwa nchi jirani wanao karibisha wakimbizi.Licha ya ukame katika Afrika ya mashariki mwishoni mwa 2016 imeongeza uhaba wa chakula katika nchi mbalimbali za kanda ya kusini.

Ripoti ya FAO inaeleza kuwa uzalishaji wa nafaka duniani kwa ujumla imepiga hatua kubwa kwa mwaka 2016,hasa kwa ahueni ya nchi  za Marekani ya Kati, wakulima wakubwa wa Asia,Ulaya na Amerika ya Kaskazini.Kwa mtazamo wa mbele , kwanza FAO inatabiri uzalishaji wa ngano kimataifa kwa mwaka 2017  ya kwamba unaonesha upungufu wa asilimia 1.8% kulinganisha na rekodi ya mwaka jana hasa kutokana na matarajio ya asilimia 20% ya kushuka kwa uzalishaji nchini Marekani ambapo maeneo yanayo panda ngano wakati wa baridi inaonesha kuwa ya chini kabisa kwa kipindi cha miaka zaidi ya 100 iliyopita.

Nchi ya Brazil na Argentina kwa mwaka 2017 matarajio ya zao la mahidi ni chanya kwa ujumla katika eneo lote la kusini mwa dunia.Kwa upande wa mpunga , hali ni mchannyiko , lakini bado ni mapema mno kufanya utabiri sahihi kwa ajili ya wingi wa mazao muhimu zaidi duniani.
Uzalishaji wa mahidi nchi za kusini mwa Afrika umepunguzwa kutokana na mavua za El Nino, wataweza kupona kidogo mwaka huu kutokana na nchi ya Kusini mwa Afrika ambayo inarajiwa kuongezeka kwa zaidi ya asilimia 50% ukilinganishwa na mwaka 2016,  na uwezekano wa mwendo chanya katika nchi za kusini .Hata hivyo kuna kuna hali inyaoonekana ya wadudu na michanga  pamoja na mafuriko nchini Msumbiji, Zambia , na Zimbabwe , ambavyo vinaweza kuzuia faida za uzalishaji kwa mwaka 2017.

Nchi 37 kwa sasa zenye kuhitaji msaadawa chakula kutoka nchi ni Afghanistan, Burkina Faso, Burundi, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Congo, Korea ya Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Djibouti, 'Eritrea, Ethiopia, Guinea, Haiti, Iraq, Kenya, Lesotho, Liberia, Libya, Madagascar, Malawi, Mali, Mauritania, Msumbiji, Myanmar, Niger, Nigeria, Pakistan, Sierra Leone, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Swaziland, Syria, Uganda, Yemen na Zimbabwe.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.