2017-03-02 14:15:00

Maisha ni matakatifu, yalindwe na kuhesimiwa kwa gharama zote


Maaskofu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wana wasiwasi mkubwa kutokana na hali halisi  ya nchi yao kwa ngazi ya kisiasa katika jamii.Hiyo ni kutokana na ukosefu wa kutimiza makubaliano yalitolewa mwaka jana pia matukio ya vurugu yanayo endelea katika nchi hiyo na kusababisha ulinzi na usalama wa raia kuwa mashakani.Wasiwasi huo unasomeka katika ujumbe uliotiwa saini  mara baada ya Mkutano wao wa mwaka huko Kinshasa kuanzia 20 hadi 25 Februari 2017. Ujumbe wao wa mwisho unayo kauli mbiu “Hakuna vizuizi mbele ya masumbuko ya sasa: kuweni wajasiri kwa sababu Kristo ameushinda ulimwengu.”

Katika ujumbe huo Maaskofu wanaonesha wazi hali halisi ilivyo katika ngazi za kisiasa, nakuweka bayana kile ambacho kinaweza kutojitokeza katika kuendeleza ghasia na vurugu.Hali kadhalika wanaelezea juu ya makubaliano ya kisiasa pamoja na mchakato wa uchaguzi unaosisitizia juu ya kumpata waziri mkuu .Kutokana na hilo wanazitaka sehemu zote mbili wawe na mazungumzo wazi, ambayo yafanyike kwa uamanifu na matumaini ya kila mmoja kati ya wagombea urais na wapinzani.

Ukosefu wa mchakato wa uchaguzi mkuu nchini humo unazidi kuleta hali tete  wakati, ghasia zinaendelea kuongezeka hadi kufikia kupinga Kanisa Katoliki bila sababu zisizoeleweka, wanasema. Lengo kuu la Baraza la Maaskofu katoliki DRC ni kwamba, utume wao katika kipeo cha uchaguzi , unahusu kuwapatia wadau wa kisaisa na kijamiii, picha kamili na mwelekeo wa uhakika, kutoa ushauri kwa ajili ya mafao yao wenyewe.Pia ujumbe unasema, hiyo ni kazi ya kuunganisha ambayo siyo mchezo na ambayo haiwezekani kuwekewa vikwazo.Utume huo ni wa uaminifu na utume wa utabiri.Kwa njia hiyo, Maaskofu wanasisitiza kwamba nia ni kusindikiza jamii ya Congo katika kufikia makubaliano yaliyo kuwa yametolewa mwishoni mwa mwaka 2016.

Hali kadhalika maaskofu wana laani vikali vitendo vya wanamgambo na polisi kwa uharibifu mkubwa wa miji kadhaa ikiwemo unyonyaji wa watoto wadogo kufanywa maaskari, na hivyo wanaendelea kusema, “ Tunakemea  na kulaani vikali kila vurugu” wanasisitiza  “maisha ni matakatifu na yanahitaji kulindwa.Ni lazima kuyalinda na kuyaheshimu kwa gharama zote.Tunalaani  na hasa mashambulizi ya mfululizo dhidi ya miundo mbinu ya majengo ya Kanisa Katoliki”. Kwa upande wa wito wao, Baraza la Maaskofu katoliki nchini Congo, yana mwendea  hata Rais Kabila kwa sabababu aweze kutekeleza makubaliano yaliyo fanyika mwishoni mwa mwaka 2016.Kwa njia hiyo pia ni kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa eneo zima la Taifa,kwa watu wengi wanaotaka kufanya uchaguzi wa Rais, kwa wapinzani na si kuzuia utekelezaji wa Mkataba .

Ujumbe pia unaelezea kwamba wanapaswa  kuandaa uchaguzi ndani ya kipindi kilichokubaliwa.Kwa upande wa vyombo vya habari waweze kuchangia katika mshikamano wa kitaifa kwa kuwajuza kinachoendelea kwa usahihi. Maaskofu hawakosi kuwageukia vijana wakitoa mwaliko kujihusisha na makubaliano ya mkataba wa mwisho wa mwaka 2016 na kuwajibika katika matumizi ya mitandao ya kijamii.Kwa upande wa Jumuiya ya Kimataifa wanaomba wasaidie mchakato wa uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Na mwishowe,  kwa waamini wote wanao omba wasali kwa ajili ya amani ya nchi na kutimizia ishara za huruma katika kipindi  cha uchaguzi.

 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.