2017-02-28 14:31:00

Jamii haiwezi kujichukulia hatua za kisheria mikononi mwao A.Kusini


Hakuna kinacho halalisha ukatili dhidi ya wageni ,ni maneno ambayo yametamkwa  na Askofu Abel Gabuza  wa Jimbo la  Kimberly na Rais wa Kamati ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu wa Afrika ya Kusini (SACBC) wakati wa mkesha wa siku ya maandamo dhidi ya uwepo wa wageni nchini Afrika ya Kusini ,maandamano yaliyofanyika Pretoria tarehe 24 Februari 2017. 
Askofu Gabuza aliwataka waandamanaji wawe na utulivu na kujizuia , lakini ombi lake halikusikilizwa kwasababu kumetokea mashambulizi ya wafanya biashara na wahamiaji kwa mapigano na polisi ambao waliwatìa mbaroni watu zaidi ya 130.

Wahamiaji halali na wasio kuwa na vibali vya kukaa wanatuhumumiwa kuhusika na vitendo vya uhalifu vinavyo kithiri na pia watu mahalia kulalamika kwamba ukosefu mkubwa wa ajira nchini Afrika unasabaishwa na wageni hao.
Kwa njia hiyo Askofu Gabuza anasema"hatuwezi kukubali kesi za namna hiyo pamoja na kusema eti kuna wageni wahalifu,jamii haiwezekani  kujichukulia hatua za kisheria mikononi mwao wenyewe, hivyo Askofu ameomba mashirika ya diaspora ya Afrika na polisi kubaini wanao fanya  vitendo vya jinai na uhalifu miongoni mwa wahamiaji waliopo na hasa wale wanaoshiriki kuuza dawa za kulevya na ukahaba.Ameitka vilevile Serikali kuimarisha uthibiti katika mipaka.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.