2017-02-25 18:05:00

Wasaidieni hata wale wanao ishi uchumba sugu bila kufunga ndoa


Ni furaha kukutana nanyi baada ya semina yenu wa mafunzo iliyo andaliwa na maakama ya Kanisa la Roma kuhusu mchakato wa talaka za ndoa.Namshukuru Decano na msaidizi kwa shughuli juu ya semina ya mafunzo haya.Kama ilivyo kuwa imejadiliwa na mapendekezo ya Sinodi ya Maaskofu juu ya mada ya Ndoa na Familia imeeleweka na kuanza kutekelezwa na pia kujumuishwa kwa njia ya hai kupitia wosia wa kitume upendo wa furaha,na pia kwa kutafsisiriwa katika sheria sahii za kisheria zilizomo katika hatua mbili yaani ya hiari yake mwenyewe na hiari ya huruma ya Yesu mwenyewe.Ni utangulizi wa Baba Mtakatifu katika hotuba yake mjini Vatican tarehe 25Februari 2017, kwa maparoko kutoka nje na ndani ya Italia kuudhulia semina ya mafunzo kuhusu talaka ya ndoa na familia .Baba Mtakatifu Francisko anasema ni jambo jema ya kwamba ninyi maparoko, kwa kupitia juhudi hizi za utafiti,mnaweza kufanya utafiti katika suala hili kwa kina kwa sababu ni nyinyi wahusika wa kuthibiti kwa hakika kila siku mnawasiliana na familia hizo.Sehemu kubwa ya kesi ni nyinyi wa kwanza kuulizwa na vijana ambao wanataka kuunda familia mpya kwa kuoa na kuolewa katika sakramenti ya ndoa.

 
Ni ninyi mnao kimbiliwa na wana ndoa kutokana na matatizo yao makubwa katika uhusiano wao, katika migogoro hiyo wanataka kufufua imani na kugundua njia,ya Sakaramenti ,na katika kesi kama hizi mara nyinyi wanataka maelekezo ya kuanza mchakato wa talaka.Hakuna mtu yoyote zaidi kuliko ninyi anaye  wajua hao na ambaye anawasiliana na kukabiliana hali hali ya masuala ya kijami katika eneo hilo.Ni kwa uzoefu mbalimbali kama vile sherehe za ndoa katika Kristo,ndoa sugu, ndoa za kiserikali,au kushindwa kwa ndoa, familia na vijana wenye furaha na wasio na furaha.Kila mmoja katika hali hii ninyi mnaitwa kuwasindikiza katika safari kwa kuhudumia na  kuwapa msaada.
Awali ya yote katika kutoa ushuhuda wenu na neema ya Sakramenti ya ndoa ,na kuweka kipaumbele wema wa familia,ambayo ni kiini muhimu cha Kanisa na jamii wakati wa kutangaza kwamba ndoa kati ya mume na mke ni ishara ya umoja na utashi kati ya Kristo na Kanisa.Ushuhuda huu unakamilika kutokana na maandalizi ya wachumba kwa ajili ya ndoa waweze kutambua maana na kwa kina hatua ambazo wanatarajia katika safari yao ya maisha.Hali kadhalika wakati mkiwasindikiza vijana , wasaidieni waishi katika mwanga na hata katika vivuli ,wakati wa furaha na hata katika majaribu , katika nguvu ya Mungu na  uzuri wa ndoa yao.

 

Msisahau daima kuwakumbusha wana ndoa wakristo ya kwamba  katika ndoa Mungu anaangaza na kujionesha sura yake , tabia yake isiyo futika ya upendo wake. Ndoa ni picha ya Mungu,aliyo umba kwaajili yetu, na ambayo inaungana kwa dhati katika utatu mtakatifu wa Baba Mwana na Roho Mtakatifu. Upendo wa Mungu katika utatu , upendo kati ya kristo na Kanisa lake mchumba wake , unapaswa kuwa kiini msingi cha katekisimu na katika unjilishaji wa ndoa.Kwa njia ya mikutano binafsi na katika jumuiya , katika mipango na bila mipango, msichoke kuonesha kwa watu wote , hasa wana ndoa ,mafumbo haya makubwa. (Taz. Ef 5,32).
Mkiwa mnatoa ushuhuda huo , ni wajibu wenu kuwasaidia hata wale wale ambao wamebaini ya kwamba muungano wao siyo sakramenti ya kweli ya ndoa na wanataka kubadilika kutoka katika hali hii.Katika kazi hii nyeti ni muhimu kuifanya kwa makini kwa namna ya kwamba waamini wenu wawatambue siyo kwamba ninyi ni wataalamu katika vitendo vya urasimu au kanuni za sheria , bali kuifanya kama ndugu wanaojiweka katika hali ya mtazamo wa  kusikiliza na uelewa.


Wakati huo huo , mfanye kwa  njia ya Injili yenyewe , katka kukutana , kuwakaribisha hata  wale vijana ambao wanataka kuishi uchumba sugu bila kufumga ndoa. Wao katika nazi ya kiroho na kimaadili ni miongoni mwa masikini na wadogo , ambao Kanisa katika nyayo za Mwalimu na Bwana , Kanisa linataka kuwa mama ambaye hawezi kumtupa bali ni kutafuta mbinu za kumkaribia na  kumtunza .
 Hata watu hawa wako rohoni mwake Yesu Kristo. Waangalieni kwa macho ya huruma , ni huduma ya wali wanyonge na ni wa mwsho ambao Yesu anataja katika Injili , ni sehemu muhimu ya huduma yenu kwa ajili ya kukuza na kulinda Sakramenti ya ndoa.
Mwenye heri Paulo wa VI alikuwa akifundisha ya kwamba Parokia ni uwepo wa Kristo katika ukamilifu wa kuokoa kazi yake, ni nyumba ya Injili , ni nyumba ya ukweli , ni shule ya Bwana wetu. (mafundisho ya Papa Paulo VI ”8 Machi 1964)


Baba Mtakatifu anaongeza ,nikiongea hivi karibuni na mahakimu wa Kanisa wa Roma , nilitoa pendekezo ya kuanzisha kweli njia ya ukatekumeni endelevu wa ndoa , ambao unafunika hatua zote za kisakramenti kama vile kipindi cha mandalizi ya ndoa, maadhimisho ya ndoa , na hata miaka itakayofuata,na hasa ninyi Maparoko ni wajibu kwa kushirikiana na maaskofu , ambao wamewakabidhi kazi ya ukatekumeni .Ninawatia moyo japokuwa ni ngumu ambayo mnakutana nayo.
Namshukuru kwa uwajibikaji wenu kwa ajili ya ya kutangaza Injili ya familia. Roho Mtakatifu hawasaidie kuwa wahudumu wa amani na furaha  katikati ya watu watakatifu waaminifu wa Mungu, hasa kwa watu wanaoishi katika mazingira magumu na masikini katika huduma yenu ya kichungaji.
Wakati huo naomba sala kwajili yangu na ninawapatia baraka kila mmoja wenu na jumuiya zenu za kiparokia.

 

Sr Angela Rwezaual

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.