2017-02-25 17:49:00

Kwa matendo yenu onesheni Kanisa masikini na kwa ajili ya masikini


Kwa furaha ninawapokea mkiwa katika hija kwaajili ya maadhimisho ya miaka 50 chama chenu cha washiriki Katoliki wa  Mshikamano .Kwa kupitia kwenu ninatoa salam pia kwa watu wote  ambao wamejitolea kwa zaidi ya miaka 50 katika nchi  hata kwa wale ambao leo na hata jana wameweza kujitoa katika uwepo wao na uwezo wao.Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliyo aliyo anza nayo, alipokutana na Washiriki Katoliki wa Mshikano wa Baraza  la maaskofu wa Ufaransa mjini Vatican 25 Februari 2017 wakiwa katika hija ya madhimisho ya miaka 50 ya chama chao. Baba Mtakatifu anawambia, kama alivyo andika Mwenye heri Papa Paulo wa VI katika hati “maendeleo ya watu” ya kwamba, maendeleo hayawezi kuja  kiurahisi bila kukua kwa uchumi. kwa njia hiyo ili maendeleo yaweze  kuwa yauhakika yanapaswa kushirikisha ,kwa maana ya  kuhamasisha kila mtu na watu kwa ujumla.Ili mshikamano wa ulimwengu uweze kuwa dhahiri unapaswa ujikite kwa watu wote na kujikimu katika mahitaji yao (nn. 14 na 65)


Uhakika huo umepelekea Kanisa la Ufarasa kuunda kwa miaka 50 ,Washiriki Katoliki wa Mshikamano, kwa uamnifu katika mtazamo wa kimisionari ambao walitambua namna ya kujitoa kwa ukarimu kuchangia kwa kipindi chote cha miongo.Baba Mtakatifu Francisko anasema kwenu ninyi ninatoa shukrani kwa Bwana kwa ajili ya roho Mtakatifu ulio jionesha katika safari ya binadamu na kiroho kwa wote hasa wanao jitolea, na katika kazi ya kuwasindikiza kwenye mipango na miradi kati ya Kanisa mahalia na watu kwa kutazama umasikini kwa matendo ya  usawa na zaidi kindugu.
Neno mshikamano, limeondolewa maana yake ya kweli, kwani mara nyingi inatafsiriwa vibaya , lakini inaelekeza zaidi jambo moja kubwa la ukarimu.Ibidi kuunda kwa upya zile hisia za kufikiria namna ya kijumuiya, kutoa kipaumbele maisha ,katika  heshimu mali za watu wengine.(Furaha ya Injili 188)

Ni kwa mtazamo huo ambapo chama cha (Délégation Catholique pour la Coopération)Washirki Katoliki wa Mshikamano wame jikita katika matendo , na kutimiza ile sehemu ya Kanisa , na pia wadau wote mahalia katika nchi ,mahali ambapo shughuli ya kujitolea imeanzia  kufanya kazi kwa kushirikiana na viogozi  wa nchi na wote wenye mapenzi mema.
Hiyo inachangia hatua ya  uongofu wa kweli katika mazingira ya kutambua utu wa kila binadamu , thamani yake binafsii na hata katika shughuli na uwezo wake katka kuunda na kuhamasisha wema wa pamoja.(wosia, mazingira nyumba ya wote 216-221).Baba mtakatifu  anawatia moyo wahusika wa chama hicho cha washiriki Katoliki wa mshikamno ya kwamba wawe na utamaduni wa huruma , unaotafuta njia za kugundua makutano ya watu wengine, yaani utamaduni ambao hautazami mtu yoyote kwa utofauti , au kugeukia pembeni baada ya kuomuona ndugu ananayeteseka. (Barua, Misericordia et misera, 20).

Msiwe na hofu katika kukimbilia  njia ya undugu , na kujenga madaraja kati ya mtu na watu  katika ulimwengu unaoendelea kujenga kuta kwasababu ya kuogopa wengine.Kwa mtazamo wa shuguli zenu , mipango na matendo yenu , yaoneshe Kanisa lilivyo masikini na kwa ajili ya masikini, onesheni Kanisa linalo taka kutoka nje  kuwa karibu na watu wengine wanao teseka , wanao baguliwa na walio na pweke.

Endeleeni  kuwa jasiri katika kutoa huduma ya Kanisa linalo ruhusu kila mmoja ajitambue na kuwa karibu na Mungu wa huruma na upendo wake, ambaye anapokea na kutoa nguvu kwa njia ya Yesu kristo , aliye neno hai. Jibidisheni kuonesha talanta zenu za wema kwa watu wote , na kuwa makini katika kulinda nyumba yetu ya pamoja.Alimaliza Baba Mtakatifu Francisko akisema, nikiwa na Muomba Bwana kuwasaidia ili mpate  kutoa huduma ya utamaduni wa makutano katika muungano wa familia ya kibinadamu , ninatoa baraka ya kitume ninyi nyote sehemu ya Washiriki Katoliki wa Mshikamano.








All the contents on this site are copyrighted ©.