2017-02-25 17:37:00

Jumuiya ya Capodarco kujikita zaidi katika wanyonge na walemavu


Ninafurahi kuwapokea katika mkutano na kumshukuru Padre Franco Monterubbianesi , mwanzilishi wa Jumuiya na Padre Vicinio Albanesi Rais wa Jumuiya yenu kwa sasa , kwaajili ya maneno yake na pia wote kwa ushuhuda.
Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi 25 Februari alipokutana na wawakilishi wa Jumuiya ya Capodarco. Baba Mtakatifu anasema Jumuiya ya Capodarco imegawanyika katika sekta mbalimbali katika hali halisi za maeneo na mitaa, ambapo mwaka jana imeadhimisha miaka 50 tangu kuanza kwakwe. Kwenu ninyi ninawashukuru kwa huduma nyingi mlizo fanya kwa ajili ya watu walemavu , watoto, watu wanaoishi katika hali tegemezi na usumbufu , na pia familia zao.Ninyi mmechagua kuwa upande wa hawa kwa ajili ya kuwalinda na kutoa msaada wenu, kutoa matumaini katika na katika kushirikishana ,kwa njia hii  mmechangia na kuendelea kuchangia ili jamii iweze kuwa bora.

Ubora wa maisha ya ndani ya jamii unapimwa kwa kiasi kikubwa kutokana na uwezo waowa pamoja kuwajali wale ambao ni wadhaifu na wanahitaji msaada,kwa kuheshi kwa upendo hali yao na utu wao wote bila ubaguzi.Ukomavu huo unatambulika wazi katika kuona kwamba kutokubagua ni jamabo ambalo ni kawada. Hata watu wenye ulemavu wa kimwili , akiliki na kimaadili, lazima waweze kushirikia maisha ya jamii na kusidiwa ili waweze kutekeleza ukubwa wa uwezo wao.Ni kwa njia tu ya utambuzi wa haki ya wanyonge , jamii inaweza kusema imejengwa juu ya sheria na haki.Jamii ambayo inatoa nafasi kwa watu wakamilifu, wanao jitegemea, siyo jamii inayostahili kuitwa ya kibinadamu.kwasababu ubaguzi na kuona msingi ya ufanisi haikubaliki na hata ile jamii inayotazama rangi au dini.


Kwa upande wa Jumuiya yenu imeweza daima kujiweka katika hali ya kukisikiliza kwa makini na kwa upendo, imejitahidi kukabiliana na mahitaji ya kila mmoja kwa kuzingatia uwezo wao na mapangufu yao.Hiyo mbinu yenu kwa upande wa wadhaifu , inazidi upeo wa juu wa huruma na kutoa huduma katika ustawi wa jamii , wakati huo inafungua nafasi ndani ya jamii. Baba Mtakatifu anawatia moyo wa kuendelea na safari hiyo , inayotazama hawali yote moja kwa moja ngazi ya walemavu.Mbele ya matatizo ya uchumi kutokana na matokeo hasi ya utandawazi , ya kwamba jumuiya inatafuta kuwasaidia wale wanao jikuta katika majaribu, wasiweze kujisikia kubaguliwa na kutupwa pembeni bali kutembea  mstari wa kwanza, wakitoa ushuhuda wa uzoefu binafsi.Hiyo ndiyo inayo takiwa kuhamasisha utu na heshima ya kila mtu , ili aweza kujisikia ameshinda maisha , na huruma ya Mungu Baba mwenye upendo wa kila kiumbe.


Baba Mtakatifu Francisko anawashukuru kwa mara nyingine tena kwa ushuhuda wao katka jamii ,ya kwamba wanasaidia watu ili waweza kugundua heshima na utu wa kila mtiu, kuanzia wa walio wa mwisho.Kwa njia hiyo Taasisi, mashirika na vyama mbalimbali vya kijamii katika kuhamsisha wanaalikwa kudumisha na kuwasaidia hawa watu.
Ni kufanya kazi kwa ajili yao ,kwa upendo na utaalam katika kusaidia pia familia na wanao jitolea ,ambao wanakumbusha maana na thamani ya kusaidia.Ushiriki wa walio wadogo katika Jumuiya ya Kanisa ni kufungua njia ya mahusiano rahisi ya kindugu , na sala zao rahisi kumwelekea Baba yetu aliye mbinguni.

 

Aidha anakumbusha kwamba asili ya chama hiki ni kutokana na hija katika madhabahu ya Mama Maria  ya huko Lourdes Ufaransa na Loreto nchini Italia ambapo Padre Franco alihisi namna ya kumsaidia, kumpa thamani  binadamu, kiroho na kimwili kwa kila mtu na hasa aliye na matatizo. Kutokana na huduma yenu ya jumuiya na yenye thamani katika Kanisa na Jamii, Bikira Maria awasindikiza na kuendelea kuwasaidia kupata nguvu mpya kila mtu katika kutunza daima mtindo wa Injili ambao ni huruma , ukarimu, ukaribu na hata ujasiri , roho ya sadaka kwasababu siyo rahisi kufanya kazi katika sekta ya wenye matatizo binafsi na katika jamii.








All the contents on this site are copyrighted ©.