2017-02-23 16:53:00

Tukumbuke kutoa shukrani kwa wale walio tusaidia kufikia lengo


"Soka kama michezo mingine ni mfano wa maisha binafsi na ya jamii", ni maneno aliyo tamka na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa kukutana na wanasoka na viongozi wao kutoka timu ya Villareal nchini Huispania, tarehe 23 Februari 2017 mjini Vatican."Kama ukicheza unafikiria juu ya mema ya kikundi , basi ni rahisi kupata ushindi" anasema Baba Mtakatifu. "Na hii inawezakana kama sisi tunatenda kwa moyo wa umoja na kuachilia kando ubinafsi  au matarajio binafsi kwani ki ukweli soka ni kama michezo mingine yaani ni mfano wa maisha binafsi  na ya jamii"


Kwa upande mwingine wachezaji wakiwa wanacheza,Baba Mtakatifu anaongeza "wakati huo huo wanaelimisha na kusambaza maadili,ili watu wengi na hasa vijana waweza kustaajabia na kuwachunguza . Wachezaji hutoa mfano kwa namna ya kuweza kuigwa na kufuatwa kwa wale wanao watazama, na hivyo hii ni wajibu ambao unapaswa kuhamasishwa na kutoa ubora wao wenyewe kwa kuhakikisha kwamba yale maadili ambayo soka inawakilisha inatazamwa na kope za macho kama vile umoja, juhudi binafsi ,uzuri wa mchezo na timu ya kucheza vinatekelezwa.

Kipengele  kingine anachotilia mkazo Baba Mtakatifu Francisko kwa wachezaji hao  anasema ni "kuhusu mchezo mzuri , na kutoa shukrani , ambayo pia inaongoza maisha yetu kuelekea wale wote walio tusaidia , kwa maana bila wao tusingefikia mahali hapo.Anasema."Kwa kujisikia njia hii inatusaidia kukua kama watu na  kwa sababu 'ya mchezo wetu? Hapana siyo kwaajili yetu tu bali pia kwa ajili ya watu wengine ambao ni sehemu yetu ya maisha. 

Anahitimisha akiuliza ni kwanini wanaweka mlinzi wa kuzuia mpira, ni kwasababu hujui atakaye piga teke mpira huo utaelekea sehemu ipi, na hiyo ndivyo maisha yalivyo.

 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.