2017-02-22 13:32:00

Binadamu akiingiliwa na ubinafsi maisha yake yanaharibika


Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko imetokana na Waraka wa Mtakatifu Paulo kwa Warumi usemao kwa maana tunajua mpaka sasa viumbe vyote vinalia kwa maumivu kama ya kujifungua mtoto .wala si hivyo viumbe peke yake bali hata sisi tulio na roho aliye wa kwanza wa zawadi za Mungu : sisi pia tunalalamika  ndani yetu tukingojea tufanywe watoto wa Mungu , nazo nafasi zenu zikombolewe. Maana kwa matumaini  hayo sisi tumekombolewa. Lakini tumaini halina maana ikiwa tunakiona kile tunacho tumainia.Maana ni nani anayetumani kile anachokiona? Kama tunakitumaini kile ambacho hatujakiona bado ,basi tunakingojea kwa uvumilivu.Hali kadhalika naye  roho anatusaidia katika udhaifu wetu , maana hatujuhi tunavyo paswa kuomba, lakini roho mwenyewe anatuombea kwa Mungu kwa mlio na huzuni usio elezeka. Naye Mungu aoneaye mpaka ndani ya mioyo ya watu anajua fikira ya huyo roho, kwani huyo roho huwaombea watu wa Mungu kufuatana na mapenzi ya Mungu. (Rm 8, 22-26).

Baba Mtakatifu katika Katekesi yake ya Jumatano, tarehe 22 Februari 2017 kwa mara nyingine tena kurudi katika Viwanja vya Mtakatifu Petro, anasema mara nyingi tuna shawishika kumuona Muumba ni wa binafsi ambapo tunajidai kufanya chochote utakacho , na kwamba hakuna anaye weza kuuliza juu yake.Katika barua ya Mtakatifu Paulo kwa warumi anatukumbusha jinsi  kazi ya uumbaji ilivyo zawadi na maajabu ambayo Mungu ametukabidhi mikononi mwetu , ili tupate kuwa na mahusiano na yeye , na kutambua uhuru wa ishara ya upendo ambapo sisi wote tunaalikwa kukamilisha na kushikamana siku hadi siku.

Lakini binadamu anapoingiliwa na ubinafsi , basi maisha yake yameharibika   hata mambo yake yale mazuri aliyokabidhiwa.Ni kama yalivyojitokeza hata katika kazi ya uumbaji.Huo ni uzoefu wa dhambi ,uliovunja mahusiano ya Mungu yaani asili ya muungano iliharibika hata kwa kile chote kinachotuzunguka kikaishia kuharibu kazi ya uumbaji kwasababu ya kuanguka chini katika dhambi. Muungano na Mungu unapovunjika Baba Mtakatifu Francisko anasema binadamu anapoteza uzuri wake na kubadilika  kila kitu , ambacho tangu mwanzo kilikuwa kinatoa sura na mfano wa Baba muumbaji na upendo usio na mwisho , na kwa namna hiyo sasa ni kutoa ishara ya huzuni, upweke wa kiburi na ukatili wa binadamu.

Lakini Bwana hawezi kuacha upweke katika sura hiyo kwasababu anatoa fursa ya matumaini mapya ya uhuru na  ukombozi wa ulimwengu.Huo ndiyo Mtakatifu Paulo anaonesha kwa furaha , akiwaalika watu wawe makini katika kusikiliza kilio cha uumbaji.Baba Mtakatifu Francisko anasema,tunapokuwa makini kwa dhati kila kitu kinacholia hata kazi ya uumbaji  ni sisi wenyewe tunalia kama binadamu na hata roho aliye ndani mwetu, katika mioyo yetu.Kwa njia hiyo machozi haya siyo kwamba  hayazai na siyo kwamba hakuna kitulizo bali Mtakatifu Paulo anabainisha vizuri ya kuwa  hayo ni kama  machozi mama anaye jifungua mtoto , ni machozi ya mtu anaye teseka , lakini akiwa na utambuzi wa kupata kiumbe mpya.

Kwa upande wetu ndiyo ilivyo , kwani tunakabiliwa na matokeo ya dhambi na kila kitu kinachotuzunguka  ni alama ya jitihada zetu za mapungufu na hata kufungwa kwetu.Wakati huo huo lakini tunatambua ya kwamba tayari  tumekombolewa na Bwana na tayari tumepewa kutafakari na kuonja ndani mwetu kile kinachotuzunguka kama ishara ya ufufuko, au pasaka ambayo inafanya viumbe kuwa vipya. Kwa Matumaini tunajua kwamba Bwana anataka kutuponya moja kwa moja kwa huruma yake wote walio jeruhiwa mioyo na unyonge kwa yote yale mabaya waliyopitia na kwamba kwa njia hiyo yeye anageuka kuwa kiumbe mpya katika ulimwengu mpya na ubinadamu mpya ambapo hatimaye, binadamu anarudia upatanisho katika upendo wake na hayo ndiyo lengo la matumaini yetu.

Mkristo haishi nje ya ulimwengu , yeye ana uwezo wa kutambua ndani ya maisha yake mwenyewe ni kitu gani kinamzunguka katika mazingira, yaani dalili za uovu, ubinafsi na dhambi.Yeye ana mshikamano na wale ambao wanateseka , wanaolia na wale ambao wandelea kubaguliwa. Pamoja na hayo mkristo amejifunza kutambua hayo kupitia mwanga wa Pasaka, kwa macho ya Kristo mfufuka .Kwa namna hiyo anajua kwamba anaishi kwa subira , kipindi cha hamu ya kuelekea upeo wa juu zaidi ya wakati  uliopo na katika wakati wa utimilifu.

Baba Mtakatifu Francisko anasema ni mara ngapi hata sisi wakristo tunajaribiwa kutaka kukata tamaa au kuona kila kitu ni kibaya, na mara nyingine tunapoteza muda , na kubaki bila kuwa na maneno , wala hatujuhi ni kitu gani cha kuomba , hata cha kutegemea.Lakini kwa mara nyingine tena , Baba mtakatifu anasema ndipo anakuja Roho Mtakatifu , anatutia nguvu na matumaini yetu ambayo  yanaendelea kuwa hai katika machozi yetu,kuwa na matumaini ndani ya mioyo yetu . Anamalizia akisema ni Roho mwenyewe anaona zaidi ya kile kionekanacho wazi na kutufunulia tayari mbingu mpya na nchi mpya ambayo Bwana anaendelea kufanya maadalizi ya binadamu.

Mara baada ya katekesi yake , Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 22 Februari 2017 kama kawaida yake aliwasalimia mahujaji wote kutoka pande zote dunia waliofika kwenye viwanja vya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro kumsikiliza,pamoja na salam hizo bado ametoa wito wa nguvu kwa nchi ya Sudan ya Kusini inayokabiliwa na migogoro ya kivita  na kusababisha watu wengi waendelee kuteseka na baa la njaa. Kwa mujibu wa habari za Umoja wa Mataifa zinasema ni mamilioni ya wameathirika kwa ukosefu wa chakula katika ukanda wa pembe ya Afrika, kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anataka utolewe msaada wa dhati kwa ajili ya watu hao.

"Ni wasi wasi na uchungu wa kusikia habari kutoka katika nchi Sudan ya kusini , ambako kumekuwa na migogoro ya kivita, na kuongezeka pia ukosefu mkubwa wa chakula, na kusababisha vifo vya mamilioni ya watu, ikiwa ni pamoja na watoto wengi. Kwa wakati huu ni muhimu zaidi  kuwajibika wote bila kusimama mbele ya kauli tu , kwa njia ya matendo ya dhati ili kutoa misaada ya chakula na kufanya kwamba hiyo misaada inawafikia watu wanaoteseka. Bwana awadumishe ndugu zetu na wale ambao wanafanya kazi kuwasaidia.

 

Akiwasalimia vijana wote, wagonjwa na wana ndoa wapya , anawakumbusha juu ya sikukuu ya Ukulu wa Petro mtume , ambayo imeangukia siku ya katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko siku ya Jumatano 22 Februari 2017, anasema ni siku ya pekee kwa waamini wote wakiwa na Khalifa wa Mtakatifu Petro kwenye Makao yake makuu. Na hivyo, anawatia moyo vijana kujikita kwa kina katika sala zao kwa ajili ya utume wake .Na Wagonjwa anawashukuru kwa ushuhuda wa maisha yao wanayo toa katika mateso kwaajili ya ujenzi wa jumuiya ya Kanisa, vilevile kwa wana ndoa wapya anasema wajenge familia zao katika upendo ule ule unao waunganisha na Bwana Yesu na Kanisa lake.

 

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.