2017-02-21 16:56:00

Ziara ya Baba Mtakatifu katika Kanisa la Kianglikani mjini Roma


Baba Mtakatifu Francisko atafanya ziara ya kihistoria katika Kanisa la kianglikana  la Uingereza lijulikanalo kwa jina la watakatifu wote mjini Roma Jumapili 26 Februari 2017.Atakuwa ni Papa wa kwanza kuweka mguu katika Kanisa hilo  kama Askofu wa Jimbo la Roma. Ratiba  elekezi inaonesha kwamba wakati wa mchana Baba Mtakatifu ataungana katika mkutano wa muda mfupi pamoja na kubariki picha ya Kristo mkombozi ambapo pia atashiriki sala ya masifu ya jioni ya kianglikana ikiwe nyimbo na atatoa mahubiri yake.

Waamini watafanya marudio ya ahadi za Ubatizo na kubadilisha zawadi, na kumalizia na sala ya baba Yetu.Katika Ziara yake pia kutakuwa na uzinduzi wa makanisa mawili kushikamana kati ya Kanisa la watakatifu wote la kianglikani na wa parokia moja ya Roma linalo itwa  " kila mtakatifu" na baadaye baba Mtakatifu atajibu maswali kutoka katika mojawapo ya wajumbe wa  shirika hilo.Mwisho watamalizia na kipindi cha mazungumzo. Tukio hili linakuja kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 200 Kanisa hili la watakatifu wote iliyoanzishwa na kundi kidogo la  waamini wa Kanisa la Uingereza 27 Oktoba 1816.Kanisa hilo likajengwa baada ya muongo mmoja , ambalo muundo wake ni kama mojawapo ya Kanisa maarufu nchini Uingereza  kwa usanifu  wa zama za Victoria katika Barabara ya George Edmund.

Kanisa hili ni sehemu ya Dayosisi  ya Kingalikana iliyoko nchi za Ulaya yaani nchini Italia na Malta ambalo hivi karibuni limepata utambulisho kisheria kutoka katika Serikali ya Italia, likiongozwa na Mchungaji wake Canon Boardman na msaidizi wa mchungaji  Dan English.Jumuiya ya Kanisa la wainglikani wa Watakatifu wote ni shirika kubwa nchini Italia .Na Askofu wa Jimbo Robert Innes atamkaribisha Baba Mtakatifu akiwa pamoja na Askofu mwenzake David Hamid.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.