Kongamano linalowakilisha Jubilei ya Mama Maria wa msaada limefunguliwa tarehe 16 Februari 2017 katika madhabahu kwanye mji wa Cebu nchini Ufillippini chini ya usimamizi wa Mapadri wa Shirika la Redentoristi.Pamoja na Kongamano hilo mada zikazo tolewa hazitawasilisha mada za kirohotu peke yake, bali hata kujikita katika mada nyeti za kijamii , kama vile Kampeni ya Serikali ya Taifa kupinga madawa ya kulevya kwani inasemekana watu zaidi ya 7,600 wameathirika kwa kipindi cha miezi sita. Ni habari zilizo jaza kurasa za magazeti na kuleta mgawanyiko mkubwa kati ya Kanisa Katoliki na Serikali ya Rais Duterte.Padre wa Shirika la Redentoristi Cris Mostajo anaeleza hayo katika Shirika la Habari la fides akionesha pia ratiba kamili ya shughuliza za Kongamano linalo adhimisha miaka 150 tangu kufika kwa picha ya mama Maria wa msaada.
Ni zaidi ya washiriki 700 katika Kongamano hilo ,japokuwa Padre Cris anasema , hatuna
furaha hata kama waamini wa kifilipini ni wafuasi wa Bikira Maria, kwasababu hawajali
juu ya utamaduni wa kifo. Anasema “leo hii tunajikuta mbele ya huzuni wa hali halisi
ya nchi , ambapo mambo matakatifu na hasa ya maisha ya binadamu ni ukiukwaji tu ,
kwa kudai kwamba kufanya usafi katika kuondoa watu wasio tamaniwa, kwa njia hiyo
bado kuna haja ya imani ambayo iweze kujikita kwa kina ndani ya maisha ya waamini
wa Ufillippini “.
Katika Kongamano pia mada nyingine itahusu nafasi ya wanawake katika Kanisa, na mapokeo
ya mama Maria nchini Ufillippini.Hali kadhalika Padre Cris anasema, sakramenti ya
kitubio inaweza kuwa kiini cha uongofu binafsi wa watu, kwa mfano mtu mlevi na anayetumia
madawa ya kulevya wakifika kuungama ni mojawapo ya njia ya kuanza hatua ya uponyaji
na kujifunza.Anasema hayo kutokana na uzoefu kwani Mapadri hao wana andaa kozi mbalimbali
za kuwasindikiza watu wanao pambana na udhaifu ili kuondokana na hali hiyo ya ulevi
, madawa ya kulevya na kamali.Halikadhalika shuhuda kadhaa zitatolewa na mwamisionari,
walimu na wenye ndoa.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |