2017-02-16 15:32:00

Miaka 100 ya uwepo wa madhabahu ya Mama Maria Dantolingi India


Zaidi ya waamini 250,000  kati yao wasio kuwa wakatoliki , wameshiriki sherehe ya miaka 100 ya uwepo wa madhabahu ya Mama Maria wa Lourdes Dantolingi Orissa nchini India siku chache zilizopita.Sehemu hiyo ni maarufu katika mji huo kwa kutembelewa na mahujaji wengi .Madhabahu hayo ya parokia yalitabarukiwa mwaka 1917 na wamisionari kutoka Ufaransa walio fika katika Serikali ya india kwa ajili ya kuwasaidia watu kutokana na baa la njaa na janga la mlipuko wa  maradhi.

Habari kutoka katika gazeti la Osservatore Romano linasema Sherehe hizo zilianza kwa ngoma ya jadi ya kihindi na badaye ilifuata Ibada Takatifu ya Misa iliyo ongozwa na Askofu Mkuu  John Barwa wa Jimbo Kuu la  Cuttac-Bubaneswar akiwa na maaskofu wengine watano wa India,pamoja na mpadre 200, watawa 300 kutoka sehemu mbalimbali za nchi hiyo.Kwa upande  wa familia moja isiyo katoliki ni Pratap Sahu na Mke wake Priti wanatoa ushuhuda wa muujiza walio upata, kwamba kwa miaka mingi waliishi bila kumpata mtoto, na baada ya kwenda kwenye madhabahu hiyo  kuomba kwa mama Maria, wakafanikiwa mtoto.


Historia ya utamaduni wa Lourdes huko Orissa India, ilitokana na kipindi kigumu cha ukame ulio kuwa umewakumba na kusabibisha vifo vya mamilioni ya watu huko India. Kwa mwaka 1866 nchi ilipata baa la njaana kusababisha janga la kipindupindu na ndui iliyo wauwa  maelefu ya watu.Wakati wa Janga hilo ndipo wamisonari wa kwanza walifikia huko wakiwa ni wa Shirika la  Mtakatifu Francisko wa Sales.Wao walikusanya  maelefu ya watu waliokuwa wametengwa na pia watoto yatima na kuwakaribisha katika nyumba zao huko Surada.Na pia huko Dantolingi, wamisionari walikusanya watu walio kuwa na ugonjwa wa ndui na taratibu kuanza kuwapatia matibabu. Kwa maana hiyo mara baada ya janga hili , wakazi wa sehemu hiyo waliomba wamisionari kujenga madhabahu ili wapate kumshukuru Mama Maria kwa namana ya pekee kuwaokoa na njaa na balaa magonjwa ya mlipuko.

Padre Sanjeeb Kumara Beero Paroko wa Madhabahu hiyo anasisitiza kwamba kwa sasa katika eneo hilo wanaishi takribani watu 250,000 ni familia ambazo taratibu zinazidi kuongezeka.Kwa ushirikiano wa Parokia za Jimbo la Berhampur wanajaribi kuwasaidia mahujaji wote wanahofika katika madhabahu hiyo.Anaongeza “ siyo kwamba mahujaji wanafika mara moja kwa mwaka, bali wanafika mara moja kwa kila ijumaa ya mwezi , ambapo wao wanalazimka kuandaa mafundisho ya kiroho na kuandaa vipindi vya sala.
Halikadhalika Askofu  Aplinar wa Jimbo la Rayagada akiwa ni mwenyeji kutoka sehemu hiyo ya Dantolingi anasema tunayo furaha kubwa kuona familia hizi zinajenga mshikamano wa nguvu wa upendo na utulivu na watu wengine.


Aidha  Askofu Sarat Chandra Nayak wa Jimbo la  Berhampur  anakumbuka mafundisho ya familia yaliyoko katika wosia wa Baba Mtakatifu Juu ya familia furaha ya upendo na pia juu ya wosia wa Furaha ya Injili akisema  wosia huo unahusu kiini cha utume wa Kanisa , namna ya kuinjilisha leo ulimwenguni, kwa kila hali na maendeleo yatakayo jitokeza katika familia ,ni sawa sawa na  maendeleo ya Kanisa kwa maana  ulimwengu mpya unaanza sasa akihusisha maisha ya  ndoa, ambapo kwa namna ya pekee ndiyo mpango wa shughuli za kichungaji kwa mwaka 2017 katika Jimbo lake.
Maadhimisho ya miaka 100 ya madhabu hayo yameanza kwa utangulizi wa siku tisa za sala,ambapo kila siku ya maadhimisho ya sala , iliongozwa na mapadre mbalimbali na mada tofauti kwa waamini zimeotolewa.

 

Sr Angela rwezaula

Idhaa ya kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.