2017-02-15 14:58:00

Kuna haja ya Kanisa kwa upya kuwa karibu na watu wa ndoa


Katika hali ambayo Maisha ya ndoa inazidi kudidimia , ni wazi kwamba kuna haja ya Kanisa kuwepo kwa upya  karibu na watu,maana yake Kanisa kuwa masamaria, na hiyo ni kwa wote wawe watawa,na mapadri kwani wote  ni ngano na magugu yaliyochanganyika pamoja .Kwa njia hiyo ni muhimu kwa Kanisa ambalo linazaliwa katika uhalisia wake mpya na ukawapo ujasiri wa wanawake kujigundua kuwa wao ni mama.Ni maneno ya Askofu Nunzio Galantino , Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Italia katika hotuba yake tarehe 13 Februari 2017 katika Chuo cha Kimataifa cha Shirika la Watoto wa Maria msaada wa Kristo  kwenye mkutano wa mafunzo kwa watawa wa Kisalesiani, juu ya mada "utamaduni wa  makutano  na Wosia wa kitume wa Baba Mtakatifu Francisko : Furaha ya Upendo ndani ya familia Kanisa na elimu.


Wosia wa kitume wa Baba Mtakatifu Francisko juu ya Upendo katika familia, ni lengo kwa Kanisa lote anasema, ina maana kwamba kile kilicho  andikwa hakiwezi kamwe kupunguzwa kwa maandishi maalumu na kwa hali yoyote , bali kupokea ujumbe wake.Wabatizwa wote  kwa mujibu wa nafasi yake mwenyewe katika Kanisa, wanaitwa kufahamu ujumbe huu.Ufumbuzi ni kujifunza kutoka ndani ya familia,kwa kawaida ni wazazi bila ubaguzi kwa heshima  na watoto, na kujaribu kutafuta kuelewa hatua mbalimbali zinazokabili  familia kutokana na ongezeko la maporoko ya madili na kufundisha uvumilivu kwa mtazamo wa pamoja katika safari ya kindugu.Askofu anasema kwa  “upande wetu, tunapaswa kujifunza sanaa ya hekima ya kichungaji dhidi ya wale walio toka mlango wa Kanisa na hawajisikii tena kama ni nyumba.


Kwa mtazamao wa Askofu Galantino anasema tabia ya wale walio fanya uzoefu wa udhaifu wa upendo wanawajibika kwa namna fulani kutafuta  namna ya kujongea , kwasababu hakuna hukumu, hata kwa mtazamo wa wale ambao wameweza kuungana upya kama jumuiya. Kwa njia hiyo ni mwaliko katika kuhamasisha watu wasio na ndoa ndani ya Parokia ili nao  waweze kuwa na hamu ya sakramenti licha ya dhana wanayojisikia. Pia kuwakaribisha wale ambao wangependa kushiriki katika maisha ya kisakramenti licha dhamana kufanya ndoa mara mbili. Aidha anasema, kinachobaki ni kutazama mwaka wa Jubilei ambao umememalizika hivi karibuni uendelee kuwa kocha wa kutuandaa , ili tusiendelee kuwa na mtazamo wa kichini chini kuhukumu, bali kuwa na tone la huruma ambayo inaangaza wengi.

 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.