Tarehe 30 Januari Katibu Mkuu wa Baraza la maaskofu wa Uganda aliitisha washiriki 30 kutoka Jimbo la Hoima, na washiriki hao walitoka katika Kamati 9 za maandalizi ya Sikukuu ya Mshahidi wa Uganda, itakayofikia kilele chake tarehe 3 Juni 2017. Mkutano huo ulihutubiwa na Askofu Vincent Kirabu wa Jimbo la Hoima.Pamoja na maandalizi yanayo fanyika taarifa inasema kwamba ni zaidi ya wanakwaya 4000 wameanza maandalizi ya nyimbo kwaajili ya sherehe ya tarehe 3 Juni . Wanakwaya hao wamechaguliwa kutoka kila Parokia za vikarieti 3 za majimbo ambazo ni Jimbo la Hoima Kabale na Masindi.
Hayo ni maadhimisho ya kumbukumbu ya mashahidi , 45 wote wakiwa na Wakatoliki na Waanglikani
walio chomwa moto kwa agizo la mfalme Kabaka Mwanga II na baadaya Mfalme wa Buganda
kati ya mwaka 1885 na 1887 wakitetea Imani yao kwa Mungu. Mashahidi 20 walitangazwa
wenye heri tarehe 6 Juni 1920 na Baba Mtakatifu Benedikto wa XV na tarehe 18 Oktoba
1964,Baba Mtaktifu Paul VI akawatangaza kuwa watakatifu, wawili kati yao ni Mtakatifu
Andrea Kaggwa na Mtakatifu Anatoli Kiriggwajjo wakiwa wote wawili kutoka katika la
Jimbo la Hoima.
Maadhimisho kwa kawaida hukusanya mamilioni ya mahujaji kutoka pande zote za dunia
mara ya mwisho kuadhimisha sikukuu ya mashahidi katika Jimbo la Hoima ilikuwa mwaka
2001.Hali kadhalika Jimbo la Hoima limekubali kuandaa maadhimisho ya Sikukuu ya mashahidi
terehe 3 Juni 2017 katika madhabahu ya Namungongo .
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe za mashahidi wa Uganda kwa mwaka 2017
tarehe 3 Juni katika madhabahu ya Namugongo ametoa taarifa ya kwamba Takribani ya
dola za 41,806 zenye thamani ya shilingi milioni 150 za Uganda zimesha tolewa kutoka
katika maparokia na makampuni mbalimbali. Anatoa pongezi kwa mchango huo akiwa na
matumaini makubwa kufikia malengo ifikapo mwezi Aprili mwaka huu . Hata hiyo kadirio
la sherehe zinatakiwa zifikie takribani dola za kimarekani 13,353. Na hivyo anasema
kwamba majimbo yanategemea kuanzisha njia nyingine katika kuhamasisha michango hiyo
ili kufikia lengo.
All the contents on this site are copyrighted ©. |