2017-02-13 14:30:00

Nchini Misri bado kuna changamoto ya kujua kusoma na kuandika


Patriarki Ibrahimu Isaac Sedrak baada ya kumaliza hija ya maakofu wa Misri mjini Roma na Baba Mtakatifu amefanya mahojiano na Gazeti la L'Osservatore Romano. Hija hiyo ni tukio ambalo Maaskofu kutoka kila jimbo hupata nafasi ya kufanya hija Takatifu na kukutana na Baba mtakatifu katika kuwakilisha taarifa za jimbo lao kuhusu shughuli za kiuchungaji.Katika mahojiana hayo, anaongea juu ya mahitaji ya ushuhuda na  thamani ya binadamu na ukristo , akikazia  mahitaji zaidi ya elimu na afya ya nchi yake, kwani mambo hayo anasema ni mojawapo ya changamoto pamoja na kwamba mazungumzo bado ni muhimu katika nchi yeke.

Anapoongea juu ya Misri anasema,siyo kuongea kama mkristo bali ni kuongea kama mzalendo wa Misiri, maana uzalendo ni kitu muhimu ambacho ni lazima kukazania daima na kujenga uhusiano kwa ndugu na wa kiislam na kwa namna ya pekee ni watu wenye tabia ya wazi na wanapendelea mazungumzo ya pamoja.Aidha anasema uhusiano wao kati ya waislam, kwa sasa kuna maeguzi kwa sababu ya uwepo wa uhuru wa kujieleza, japokuwa bado kuna ukosefu wa uangalizi wa makini. Kwa hakika anasema unapo ongea juu ya dini, kuna hatari ya wengine kutokuelewa vizuri, kwani watu wa Misri ni watu rahisi ,ingawa wapo wengine ambao hutumia nguvu na vurugu wakashindwa  na kutofautisha  wema.

Askofu anasema idadi kubwa ya watu hawapendi hizi itikadi kali ambazo kwa hakika hazitoki kwa Mungu na wala siyo dini , kwa sababu watu wa Misri kwa sasa  wanapoteza kidogokidogo utambulisho wao , tabia ya nchi na ustaarabu wake wa kale, na ndiyo maana watu  wana kuja juu kwaajili ya kutetea usataarabu huo unaotaka kupotea.Akielezea juu ya kutafuta nafasi za kukutana , anasema tatizo kubwa ni katika elimu ambayo kwa bahati mbaya jamii ya Misri ina ukosefu mkubwa katika sekta hiyo,ushuhuda unatokana na uwepo wa asilimia 40% wasiyo jua kusoma na kuandika.

Hilo ni tatizo msingi la ukosefu wa kazi,ambapo wazazi hawatumi watoto wao shuleni , badala yake wanatuma watoto wao wafanye kazi. "Je tunaweza kufanya nini?",anauliza, "diyo  Mashule ya Kanisa  katoliki yanasaidia sana katika sekta hii , lakini haiwezi kuwafikia wote katika sekta ya jamii. Kwa upande wa wasio jua kusoma na kuandika , anasema wanaandaa kozi fupi zinazo husu maisha, ambapo ndani ya kozi hizo ni pamoja na kuwafundisha maana ya maisha na  ukristo shirikishi ambapo watoto hufanya mazungumzo juu yake.Kwa upande  wa waislam hawaishi  uzoefu huo kama njia ya uinjilishaji wa moja kwa moja bali ni kujisikia kuheshimiwa bila kuwa na unafiki , hili ni jambo muhimu. Pamoja na ukosefu wa kusoma na kuandika , bado pia kuna tatizo jingine la  ujinga wa kutokujua dini.

Misri ya Kaskazini ni sehemu ambayo ni masikini na imetelekezwa , ambapo kuna ndugu zetu waislam wenye msimamo mkali.Miaka iliyopita kulitokea makubalino kati ya serikali na ndugu hao. Wao walikuwa hawakujishughulisha na mambo ya kisiasa , baadala yake ni kuunda shule ambazo walifundisha mambo mengi , lakini zaidi ni kupinga dini yenyewe.Na hiyo ilijenga matabaka ambayo kwa sasa tunaona matokeo yalivyo.Lakini ki ukweli wamisiri ni watu wa amani lakini ukigusa suala la dini ni jambo ambalo ni nyeti sana,kwa namna hiyo sisi wakristo wa Misri tunatambua jinsi  gani ya kuishi na kufanya mazungumzo yanayo husu mambo ya dini, na kwa njia hiyo tunatambua ni mada zipi za kugusia ili kuweza kushirikishana katika mazungmzo ya pamoja.

Askofu pia anaongea juu ya kipeo cha uchumi kinacho zidi kuongeza matatizo ambapo anabainisha ya kwamba ni utalii kupungua ukosefu wa kazi  na pia ukosefu wa maendeleo ya viwanda.Licha ya hayo pia bado kuna ongezeko la watu linaleta pia changomoto mpya na  kubwa  kwa nchi ya Misri.Kwasababu wanazaliwa watoto milioni moja kwa kila mwaka, kwa maana hiyo ni kusema kwamba kila darasa  shuleni  kuna watoto mia moja .Ni vigumu kijifunza kwa namna hiyo hayo ni matatizo dhahiri yanayohitaji majibu ya kweli, na kanisa linalizimika kuwajibika , kwasababu mashule ya Kanisa Katoliki ni kwaajili ya wote na walimu kwa ujumla wapo wa kutosha tofauti na shule za serikali ambapo hazitoshelezi mahitaji ya elimu kwa njia hiyo mahitaji ya elimu kwa watoto yanategemea wazazi wao.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.