2017-02-13 15:11:00

Dharura ya ugonjwa wa mlipuko wa Hepatitis "E" kuenea nchini Chad


Nchini Chad kumezuka ugonjwa wa Epatitis "E" ambao umeenea katika Mji wa Am Timan katika ukanda wa Mkoa wa Kusini Mashariki ya Salamat.Shirika la madakatari wa kutoa misaada ya kibinadamu wametoa taarifa hiyo ambapo  tayari walikuwa wamegundua kesi ya kwanza Septemba 2016 .Tangu wakati huo Shirika hilo lisilo kuwa la kiserikali limepata kutibu wagonjwa 885 wakiwa na dalili za ugonjwa huo ,na dadi inazidi kuongezeka karibia kesi mpya 60 kila wiki zinatokea.

Hepatitis E inaambukizwa kutoka kwa  mtu na mtu na mara nyingine kwa  njia ya matumizi ya maji na vyakula au kinyesi cha watu walio ambukizwa na virusi hivyo.Taarifa zina sema kuwa matokeo ya hatari ya magonjwa ya mlipuko ni kubwa kwasababu ya ukosefu wa upatikanaji wa maji safi .
Kwa sasa ni wafanyakazi 600 wa Shirika la madaktari wa kutoa misaada wa kibinadamu wako wanafanya kazi ya kubaini kesi mpya za ugonjwa huo  na kuwatibu, halikadhali  kuboresha usambazaji wa maji safi katika mji wa  Am Timan.

Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni kuweka dawa katika kisima maji  kikubwa kilicho juu ya mnara katika mji. Usafishaji wa maji ni kipengele msingi cha dharura ili kuzuia kuenea kwa magonjwa yanayo tokana na maji,kama vile hepatatitis E. Pamoja na kutoa huduma za matibabu katika Hospitali ya Am Timan, Shirika la madaktari wamezindua pia kampeni kwa kiwango kikubwa cha kupulizia dawa katika mabwawa 72 yanayo sambaza maji katika mji wa  Am Timan, kadhalika  wameanzisha mafunzo kwa ajili ya kueleza umuhimu wa kunawa mikono kwa maji na sabuni, lakini maji yaliyo tiwa dawa, kwa njia hiyo ni dharura ya haraka kuingilia kati zaidi katika suala la maji na usafi.

 

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.