2017-02-06 16:02:00

Wafuasi waangazie ulimwengu kwa ushuhuda wa mwanga na chumvi


Injili ya Mtakatifu Mathayo bado inatuongoza na maneno ya Yesu akiwa Mlimani , kama vile Jumapili iliyopita alituonesha pia  heri akiwa mlimani vilevile. Maneno ya Yesu yanaeleza juu ya utume wa wafuasi wake ulimwenguni.(Mt 5,13-16)Yesu anatumia mifano ya chumvi na Mwanga akiwalenga mitume wake wa kila nyakati na hivyo hata sisi.Ni maneno ya utangulizi yaliyotolewa na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili tarehe 5 Februari 2017 wakati Kanisa linaadhimisha liturujia ya Juma la  tano la kipindi cha kawaida cha mwaka, kwa waamini na mahujaji wote waliokusanyika katika Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Yesu anatualika tuangaze mwanga kwa njia ya ushuhuda na matendo mema kama isemavyo Injili ya kuwa “ ungaze mwanga mbele ya watu na matendo yenu mema yaweze kuonekana  ili Mungu aliye mbinguni apate kusifiwa(Mt 5,16).

Haya maneno yanaonesha kwamba sisi tunaonekana kuwa mitume wake kweli aliye mwanga katika ulimwenguni , siyo kwa maneno tu , bali ni katika matendo yetu.Na zaidi kazi yetu kubwa ni namna tunavyoishi iwe kwa  wema au ubaya lakima uacha ishala kwa wengine. Kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu anasema tunayo kazi na wajibu kwa tunu tuliyopokea ya mwanga wa imani ambao huko ndani mwetu kwa njia ya Kristo kwa kazi ya roho Mtakatifu  ambayo hatupaswi kuitunza kama vile ni binafsi .Tunaitwa tufanye ingazwe katika ulimwengu , na kuwazawadiawengine katika matendo yetu  mema.Dunia ya leo inahitaji mwanga wa Injili  kubadili, kuponya na kumhakikishia ukombozi yoyote anayepokea mwanga na hivyo hatuna budi kuwasambazia wengine kwa njia ya matendo yetu.

Mwanga wa imani yetu , tunapo utoa hauzimiki , bali hutoa nguvu. Kinyume ni kwamba unazimika  iwapo hatulishwi na upendo na matendo mema .Mfano wa mwanga uakutana na  ule wa chumvi. Injili inatuonesha ya kamba mitume wa Kristo ambao ni sisi, ni chumvi na mwanga.Baba Mtakatifu anaeleza kwamba chumvi ni kiungo kitoacho radha , na hutunza vyakula visiwe na chachu au kuharibuka.Zama za Yesu hapakuwepo na Jokofu ! kwa maana hiyo , utume wa mkristo katika jamii ni ni kutoa radha katika maisha , na imaai , ma upendo ambao Yesu alitupatia , wakati huo huo ni kujilinda na wadudu waalibifu ambao ni ubinafsi , wivu, masengenyo na mambo mengine .Wadudu hawa hualibu virutubisho vya jumuiya zetu , ambazo zinapaswa kuangaza katika vituo vya mapokezi , mshikamano na mapatano.

Ili kutimiza lengo la utume huu sisi wenyewe tunapaswa kuwa mstari wa mbele kuwa huru kwa kupinga mambo ambayo yaweza  kuzuia mwanga na chumvi, ni mambo ya kiulimwengu yanayo kwenda kinyume na maneno ya  Yesu na Injili, kwani hakuna mwisho wa kujitakasa , bali kila siku na daima tunapaswa kujitakasa. Kila mmoja wetu anaitwa kuwa mwanga na chumvi katika sehemu ambayo tunaishi kila siku tukitimiza kazi halisi ya kutangaza maisha katika roho ya Injili kwenye mtazamo wa ufalme wa mbingu. Mama Maria  Mtakatifu awe msaada wa ulinzi , kama mtume wa kwanza wa Yesu na mfano wa waamini wanao ishi kila siku katika historia ya wito na utume wao.Mama Maria atusaidie kujitakasa katika kuangazwa kwa  Bwana ili baadaye nasi tuwe mara nyingine tena chumvi ya dunia na mwanga wa ulimwengu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.