Kuhudumia masikini ni kazi lakini ni matumaini, ni maneno ya Sista Emiliana Saptaningsih
wa Shirika la mioyo mitakatifu ya Yesu na Maria anayetoa huduma kwenye utume wa maeneo
duni huko Ufilippine ,lakini ni maeneo yasiyo takiwa kuishi mtu.
Watu walianza kushi mitaa ya maeneo hayo tangu mwaka 1980 kando kidogo ya Mji Mkuu
Manila , sehemu hiyo kwa sasa inajulikana “Bagong Silang.Taratibu mtaa huo ulipanuka
na kujaa watu masikini watokao katika mji Mkuu Manila ili kupata mahali pa kijihifadhi.
Tangu kuanza kwa kwake, Bagong Silang imekuwa na watu wengi zaidi ya 300,000 wanaoishi
Katika jitihada za kudhibiti hali hiyo wakuu wa vitongoji walijitahidi kuwapatia familia
nyingi eneo kuanzia mita za mraba 50-60 ili wapate kujenga nyumba zao . Hata hivyo
miundo mbinu ya ndani ilikuwa siyo ya kutosha kuwasaidia wakazi kutokana na wingi
wao na pia ukosefu wa huduma msingi muhimu.
Katika hali hii ndipo ikaanzishwa kituo cha Mtakatifu Damian, kilichoanzishwa na Shirika
la Mioyo Mitakatifu ya Yesu na Maria mwaka 2012 .Watawa na watu wa kujitolea wanashiriki
kikamilifu katika huduma ya waoto wenye utapiamlo na mama wajawazito kwa misaada
kwa njia ya miradi. Hali kadhalika wanayo mipango mingine kwa lengo la wakazi wanaoishi
maeneo hayo ikiwa ni elimu,kwa kutoa mafuzo ya ufundi mbalimbali na upatikanaji wa
wafadhili kwaajili ya watoto wapate kusoma shule.
Juhudi za mipango hii ni kujaribu kutoa matumani kwa watu , sista Emiliana anasema
kuwa watu hawa anapaswa wakidhi haja ya mahitaji yao kwa uwepo wa vifaa mbalimbalimbali,
lakini pia ni muhimu kuangalia mahitaji yao kiroho.Anaongeza masikini wa Bagong Silang
wana moyo mkuu ambao unazidi kuboreshwa kwa matumaini katika maisha yao endelevu.
“utume wetu ni kuwasaidia waboreshe maisha yao na pia waweze kutambua uwezo wao walio
nao na kuwasindikiza kiroho”. Anamalizia kwa kubainisha kuwa jumuiya katoliki inafanya
juhudi za pamoja ili kwafikia , kuwasindikiza na kuwatibu masikini wa maeneo hayo
duni.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |