2017-01-30 14:23:00

Watawa kupanda miti ili kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa


Shirika la Watawa wa  Mtakatifu Theresa wa Mtoto Yesu huko Dedza Deanery Malawi, walipanda miti zaidi ya 200 katika eneo la Mlale kwa ruhusa ya watawala wa Serikali huko Masula Lilogwe. Wamefanya hivyo kwasababu ya kujibu wito wa Baba Mtakatifu katika huduma ya kutunza mazingira kama nyumba yetu kwenye hati ya utetezi wa Mazingira.Pamoja na kufanya kile alichosema Baba Mtakatifu Francisko,ni kwenda pia sambamba na wito  wa Umoja wa Mataifa katika kufikia lengo la Maendeleo endelevu katika utunzaji wa mazingira.Aliyasema hayo Sista Mulenga wa Shirika hilo.

Mbali na kazi za kitawa ambao hutumia muda wao katika sala, wameokuwa na mawazo ya kuunganika na wananchi wa Malawi na zaidi katika msimu huu wa kapanda miti ili kuchangia mwelekeo mzuri wa kuboresha mazingira.
Na pia aliongeza mtawa mwingine akisema kwamba sisi hatusamewi na athari za mabadiliko ya Tabianchi,kwani tunaishi katika jumuiya na kushirikiana na watu.Matatizo yao ni sawa na matatizo yetu na ndiyo maana tumefikiria kupanda miti hii.

 
Inabainika kuwa Dedza ni eneo ambalo tangu mwanzo lilikuwa na miti mingi , lakini kwa sasa limebaki wazi kutokana na wakazi kukata miti katika matumizi ya kuni.Hali kadhalika wanachangamotisha hata vijana kuiga mifano hiyo ili nao waweze kutenda kazi hiyo nchini kote.
Hivi karibuni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Malawi  Dk. Saulosi Chilima aliwatembelea Shule moja Katoliki ya watoto katika Jimbo Kuu la Lilongwe katika zoezi la upandaji wa miti kwenye Parokia ya Mtakatifu Patrick.

Kutoka 

Ameceablog

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.