2017-01-25 16:05:00

Judithi mwanamke mjane,mwenye hekima na matumaini kwa watu wake


Miongoni mwa sura za wanawake katika Agano la Kale , tunamwona mwanamke jasiri katika watu  anayeitwa Judithi. Biblia inaleta jina lake mbele ya Kampeni ya kijeshi ya Mfalme Nebukadneza, ambaye alikuwa anatawala Ninawi, yeye aliongeza himaya yake akawashinda na kuwatia utumwani  watu walio kuwa wamezunguka. Katika maelezo hayo, inaonesha  kwamba kuna maadui wasiyo shindwa na ambao wanapandikiza kifo na uhalifu ambao uhenda ukafika hata katika Nchi ya ahadi na kuwaweka katika hatari ya maisha watoto wa Israeli. Ni maelezo ya  Baba Mtakatifu Francisko wakati wa kutoa  Katekesi yake Jumatano 25 Januari 2017 katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican. Katekesi yake inaendelea na mfululizo wa matumani ya wakristo, wakati  huo akitazama mmojawapo wa sura ya mwanamke jasiri wa imani katika Kitabu cha Agano la kale.Jeshi la Nebukadneza kwa hakika chini ya uongozi wa Jemedali Holofernes aliweka majeshi ya kuzingira mji wa Yudea na Betulia , akakata vyanzo vya usambazaji wa maji  ambao ukasabisha upinzani wa watu.

Baba Mtakatifu Francisko anasema hali ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba wakazi wa mji walikwenda kuomba wazee ili wapate kujisalimisha kwa adui zao;  maneno yao yalikuwa ni mahangaiko na kutapatapa kwani walisema “ Hakuna mtu ambaye naweza kutusaidia , kwasababu Mungu ametuuza katika mikono ya maadui ili tuweze kuwawa mbele yao kwa kiu na mabaya yote.Bora kuwaita watu wote wa mji kujisalimisha kwa Oloferne na majeshi yao wapate kutuua,( Yud 7,25-26).Baba Mtakatifu anasema maneno yao hayo yana tokana na ukosefu wa kuamini Mungu na hivyo utafikiri inafanana na kwamba  badala ya kukimbia mauti, ni kubaki tu kujisalimisha  kwenye mikono ya wale wauaji.

Mbele ya mahangaiko hayo , kiongozi wao anashauri jambo la kuleta matumaini: kwasababu anawaleza “vumilieni kwa siku nyingine tano tu, tuki subiri, msaada kutoka kwa Mungu”.Anaongeza hayo yalikuwa ni matumaini dhaifu  kwa maana aliongeza akisema “ iwapo zitapita siku hizo bila msaada wowote, basi nitafanya kama mnavyotaka (Yud7,31).Hivyo siku tano zikaruhusiwa kwa kusubiri msaada wa Mungu, ni siku tano za kusubiri lakini ambazo tayari kuna mwisho wake. Baba Mtakatifu akasema kwa hakika hapakuwepo kati ya watu aliyekuwa na uwezo wa subira.Lakini ndipo katika hali ya kukaripia ilitoka kwa Yudith , mwanamke mjane , mwenye uzuri na hekima , ambaye aliweza kuongea na watu kwa lugha ya imani, akisema “ nyinyi mnataka kumjaribu  mwenye nguvu, hapana ndugu zangu! , msimfanye Bwana awe na hira , maana ni Mungu wetu, kama yeye hatataka kutukomboa katika siku hizi tano, Yeye anauwezo na nguvu ya kutulinda  kwa siku anazopenda yeye, au hata kuwaaribu hao maadui wetu. kwahiyo ninawasihi kuwa na subira ya wokovu kutoka kwake, tuombe ili aweza kuja kutukomboa, na atasikiliza kilio chetu , kama yeye atapendezwa (8,13.14-15.)

Kwa nguvu za nabii Yudithi , anawaalika watu wake wawe na matumaini kwa Mungu, kwa mtazamo wa kinabii, anatazama  upeo wa hali ya juu zaidi kumzidi kiongozi wao aliye wafanya wawe na hofu zaidi. Je Mungu ataweza , Baba Mtakatifu nasema kwa hakika , wakati wa siku hizo tano zilitolewa ,ni njia ya kujaribu utashi wake.Bwana ni Mungu wa ukombozi,kwa kila iana ya majaribu yote.Ni mkombozi kutuokoa kutokana na maadui na kutufanya tuishi, lakini pamoja na hayo, anayo mipingo isiyo julikana,  Baba Mtakatifu anasema , yawezekana ukombozi ukapitia hata  kwa kujikabidhi kwenye kifo.

Kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu anasema , tusimwekee Mungu sababu , bali tuwe na matumaini yanayo shinda hofu.Kutumainia yeye maana yake ni kuingia katika ishara zake bila majivuno  na kutegemea ukombozi wake, msaada wake utufikie kwa njia mbalimbali tofauti na mategemeo yetu.Sisi tunaomba kwa Bwana maisha , afya , upendo, furaha , ni haki kufanya hivyo , lakini tuwe na utambuzi kwamba Mungu anaweza kutoa maisha kutoka mautini,na kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anasema unaweza kufanya uzoefu wa amani hata katika ugonjwa,unaweza kuwa na utulivu hata mbele ya upweke, na hata  kuwa na heri katika machozi.

Anaendelea kusema, siyo sisi tunaopaswa kumfundisha Mungu anachotakiwa kufanya kwa ajili yetu  na kwa mahitaji yetu.Yeye mwenyewe anatambua vema zaidi yetu bali  tunachotakiwa kufanya ni kuamini na kujikabidhi kwake  kwasababu njia zake na mawazo yake ni tofauti na ya kwetu.Halikadhalika Baba Mtakatifu Francisko anasema njia ya Yudhith inatuelekeza njia ya matumaini, subira katika amani, katika sala na katika utii.Anaonya kwamba tusiwe watu  rahisi kujisalimisha katika kufanya kila iwezekanalo kutumia nguvu zetu , bali daima inabidi kubaki katika matashi ya Bwana.

Yudithi kwa hakika alikuwa na mpango wake , na kaufanya kwa ujasiri akafanikiwa kuwaletea ushindi watu wake, lakini hiyo yote ni kutokana na imani, kwa anayekubali kulindwa na mkono wa hakika na wema wa Mungu. Anamalizia akisema huyo ni mwanamke aliye jaa imani na ujasiri, aliwapa nguvu watu wake , wakati wako hatari ya kufikiwa na mauti, na kuwapeleka katika matumaini, ambapo ni mfano kwetu sisi wa kuigwa. Kwa kufuata njia hiyo utakuwa na furaha  na mwanga wa Pasaka , na utajikabidhi kwa Bwana kama maneno yasemayo,“ Baba kama unataka, niepushe kikombe hiki, lakini si kwa mapenzi yangu bali ni kwa mapenzi yako.(Lk 22,42).

Baada yakatekesi waliwasalimia watu wote waliofika na mawzo yake yaliwandea pia vijana , wagonjwa na wanandoa . Alikumbuka kwamba  Mama Kanisa anaadhimisha Sikukuu ya Kuongoka kwa Mtakatifu Paulo mtume wa Mataifa na kuwaeleza vijana ya kwamba sura ya Paulo iwe kwao mfano wa utume wa kimisionari, na wagonjwa kwamba watoe sadaka ya ugonjwa wao kwaajili ya Muungano wa Makanisa ya Kristo.Vilevile wana ndoa wapya alisema , waige mfano wa Mtume wa watu, kutambua  ukuu wa Mungu na upendo katika maisha ya kifamilia.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.