Wakati kaskazini na magharibi ya Ethiopia wana vumilia uzito mkubwa wa El Niño, kipeo kipya cha ukame kimejitokeza katika maeneo ya wafugaji wa kusini na kusini-mashariki, kati ya mikoa ya Oromia, kusini mwa Somalia , ambapo mvua ni haba, imechelewa kaida yake , na kusababisha uwepo wa malisho madogo na upatikanaji wa maji. Asilimia 80% ya waethiopia wanategema kilimo na mifugo kuinua kipato chao.Hali hiyo pia imeathiri hata nchi jirani za Somalia na Kenya.Na athari zaidi za ukosefu wa mvua, zitasababisha malisho madogo kwaajili ya mifugo katika miezi ya kwanza ya 2017, na kufanya kama kawaida yao kuhama kutokana na ukosefu wa chakula au vifo vya wanyama wao.
FAO imeomba msaada wa haraka kwaajili ya wachungaji wa Kaskazini ambao wanateseka
na ukosefu wa mvua baada ya mafuriko ya El Nino.Hizo ni taarifa kutoka Shirika la
Chakula Duniani FAO; wanasema kwamba misaada ya kibinadamu imetolewa kuwasaidia karibia
miaka 50 hivi lakini ukosefu wa mvua wakati wa msimu wa kupanda na pia mvua za El
Nino zimendelea kusababisha jumuiya ya wafugaji kuwa na shida kubwa ya maji katika
mikoa ya Kusini.
Kwa kujibu suala hili inabidi kusaidia familia ambazo zimeathirika kwani walipoteza
kila kitu, au kuuza wanyama na mali zao au wengine kukopa na kurundika madeni.Pamoja
na hayo taarifa inaonesha kwamba kutokana na misaada iliyotolewa imepunguza idadi
ya watu watakao hitaji msaada wa chakula kwa mwaka 2017, kufikia milioni 5,6 pungufu
hiyo ni mara mbili ya takwimu ya mwaka jana 2016 ya mwezi 8 iliyokuwa imetangazwa
na Shirika la misaada ya kibinadamu kwa upande wa nchi ya Ethiopia.
Hati ya Shirika la misaada ya kibinadamu iliyopitishwa hivi karibuni, imeandaliwa
kwa mapana kwa pamoja na Serikali ya Ethiopia wakishirikiana pamoja na mashirika ya
Umoja wa Mataifa ,yasiyo ya kiserikali na wadau wengine wa maendeleo. Hati hiyo inatazama
mada mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu upatikanaji wa maji na lishe.Na inaonesha
kwamba ni sekta ya kilimo inahitaji msaada kwa upande wa wachungaji katika maeneo
ya wakulima na wafugaji. Jumla ya dola za kimarekani milioni 42 inayotakiwa na kwa
sekta ya kuweza kufikia familia milioni 1.9 hasa katika mikoa yenye wafugaji huko
kusini na kusini mashariki mwa Ethiopia kwaajili ya ukame.
Na Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.
All the contents on this site are copyrighted ©. |