Amani ndiyo iwe ajenda ya kikao cha 1127 cha mwaka katika Baraza la OSCE, hayo
yalitamkwa na mwakilishi wa Vatican, katika Baraza la kudumu la OSCE Monsinyo Janusz
Urbanczyk wakati wa Mkutano wao wa mwaka huko Vienna 12 Januari 2017.
Monsinyo Janusz alianza hotuba akimkaribisha , Waziri wa Mambo ya nchi za Nje wa Austria
Bwana Sebastian Kurz katika Shirikisho la umoja wa nchi za Ulaya kurudi kwa mara nyingine
tena katika Baraza la kudumu, kwasababu ya kuchukua nafasi ya wenyeji wa kukaribisha
vikao vya OSCE kwa mwaka 2017 nchini Austria.Na alihaidi kwamba Vatican itakuwa na
ushirikiano na kutoa msaada kwa kipindi chote watakachokuwa wenyeji wa vikao vya
OSCE Austria.
Mwaka 2017 umeanza na kivuli cha migogoro mingi kutokana na mashambulizi ya kigaidi
katika mikoa ya baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya kwa mwaka 2016.Ni lazima tukubali
kwamba watu wengi wamekuwa na wasiwasi na kutambua vema juu ya matokeo ya migogoro
, fitina na ugaidi, ambao unazua wasiwasi na hofu kwa siku zijazo badala ya kujiamini
kwa hisia za usalama.
Ili kuhakikisha, wasiwasi katika hali halisi unatoweka kwa ajili ya amani, ni lazima
uwepo ushirikiano wa pamoja katika ajenda ya baraza letu. Vatican iko tayari kusaidia
juhudi zitakazofanyika katika mikutano ya Austria kuwa mwenyeji ,kwa kutafuta haraka
mipango ya kupunguza matatizo na migogoro kwa uamninifu kati ya washiriki 57 kutoka
mataifa mbalimbali ili kupambana na siasa kali na vikundi vyenye msimamo mkali.
Halikadhalika, Monsinyo Janusz anasema Vatican imeunga mkono Baraza la mawziri huko
Umburg iliyopitisha uamuzi juu ya wajibu wa OSCE kukabiliana na kipeo kikubwa cha
wakimbizi na wahamiaji , watu wanaokimbia vita , manyanyaso na mateso kama vile umasikini,
ubaguzi, mambo hayo ni vipengele muhimu katika nchi zetu kwa miaka ijayo.
Aidha tunawapongeza Austria kuwa wenyeji na kwa ahadi yake ya kuendelea na kasi iliyofanywa
na Uswis , Serbia na Ujerman kuhusu wahamiaji, na wakimbizi wa ndani,hasa tangu wakimbizi
wengi waingie kutoka mikoa ya MENA kutokana na ukosefu wa uhuru, ikiwa pamoja na uhuru
wa dini au imani zao.Nchi zinazoshiriki zinapaswa kuhakikisha kwamba watu wote wanafurahia
haki za binadamu, kama asemavyo Baba Mtakatifu Francisko.
Tunahitaji kuchua hatua dhidi ya vyanzo na siyo madhara tu ya matukio, kwani sababu
nyingi zingeweza kushughulikiwa wakati uliopita, na hivyo maafa na athari zake vingeweza
kuzuilika.Monsinyo anasema lakini hata sasa kabla hatujachelewa kwa kiasi fulani tunaweza
kutenda jambao ili kumalizia majanga haya na kujenga imani.
Vilevile, Monsinyo Janusz alipongea juhudi ya Mashirika mbalimbali kwa ushirikiano
katika harakati za kuokoa watu kwenye Kanda za Meditreanea, na kusema Baba Mtakatifu
amekuwa akirudia wito juu ya mifumo ya fedha na uchumi ya kwamba iweze kuendeleza
maendeleo ya binadamu na kuhakikisha unakuwepo ulinzi kwa huduma ya nyumba yetu
kwa njia ya sera nzuri za kimazingira.Aidha aliendelea kusema changamoto ya haraka
tuliyo nayo ni kulinda nyumba yetu ya kawaida na pia kuleta familia nzima ya binadamu
katika kutafuta maendeleo endelevu, ambapo tunajua kwamba madiliko yawezekana .
Kwa miaka 40 zaidi mradi mkubwa ulizinduliwa na kutiwa saini na Helsinki Final Act na Vatican inatoa msisistizo maalumu wa mwelekeo wa tatu wa kulenga haki za binadamu ili kulinda heshima ya binadamu wote , bila ubaguzi wa rangi ,jinsia , lugha au dini.Kwa jinsi hiyo Vatican inaunga mkono kutoa msaada kwaajili ya kuimarisha na kuweka vipaumbele kwa ujumla katika ukubwa wa binadamu kwenye Baraza la Osce ambalo limekuwa mwenyejiwake Austrria .Munsinyo anasema kwamba Vatican inao uhakika kwamba chini ya usimamaizi OSCE inawezekana kufikia makubaliano juu ya maazimio ya mawaziri wa Baraza juu ya kuimarisha juhudi za kupambana na ubaguzi wa aina yoyote dhidi ya waislaim, wakristo na baadhi ya madhehebu madogo kama vile mapambano dhidi ya ubaguzi wa wayahudi.
Anatoa wito juu ya kuwapo na mazungumzo na ushirikiano ambao unaweza kukuza kujiamini kutokana na maridhiano , kuheshimiana na kuelewana ,na hizo ndiyo njia za kufikia amani.Pamoja na juhudi hizo Monsinyo Janusz ansema, bado kuna mambo mengi yana hitajika kufanywa ili kuendeleza kweli hali halisi ya usawa kati ya wanawake na wanaume kama vile kupambana na ukatili dhidi ya wanaweka , suala ambalo linazidi kuwa changamoto kubwa linalo athiri wanawake wengi , na kwa kiasi kkubwa ni ukiukwaji wa utu wao na haki msingi za binadamu.
Aidha mwakilishi wa Vatican anabainisha kwamba jumuku la madaraka aliyo pewa na OSCE
kuwa na ofisi zake Austria kwa mwaka 2017, kwa masuala muhimu yaliyopitishwa mwaka
huu kwa kushirikiana , lazima kutatuliwa. Na mwisho akiwatakia mafaniko mema katika
kukuza zaidi usalama na ushirikiano kati ya wawakilishi wa nchi 57 huko Marekani,
pamoja na wajumbe 2,017 kwenye Baraza la OSCE Huko Austria.
Kauli mbiu ya Kikao cha Mei 2017 utakuwa ni wanaume na wanawake wote kutoka mashariki
na magaharibi katika kujenga mazungumzo ya kidiplomasia, maelewano , ambayo itakauwa
ni alama na nguzo na hatua muhimu kuelekea amani , usalama na ushirikiano.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.
All the contents on this site are copyrighted ©. |