2017-01-11 12:44:00

Papa asema msiweke matumaini yenu katika miungu mtapotea


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 11 Januari 2017 aliendelea na katekesi yake kama kawaida katika ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican.Katekesi yake , ilikuwa ni mwendelezo wa katekesi kuhusu matumaini lakini ikiongozwa na maneno matakatifu kutoka katika Zaburi ya 115 katika mistari  inayohusu kuabudu miungu. Baba Mtakatifu alinza akisema  ndugu zangu  mwezi  Desemba mwaka 2016  na sehemu ya kwanza ya Januari  tumeadhimisha  kipindi cha Majilio na baadaye Noeli: Ni kipindi cha mwaka ambacho liturujia inawaalika watu wa Mungu kuwa na mwamko katika matumaini.Kutumania ni mahitaji ya kwanza  ya binadamu: kwa sababu ni matumaini endelevu ya  kuamini maisha,  maana nyingine wanasema tunapaswa kuwa na fikara chanya.”

Muhimu ni yale matumaini ambayo yawe ndiyo kweli jibu la kuweza kutusaidia kuishi na kutoa maana ya kuishi kwetu.Na ndiyo maana mandishi matakatifu , yanaweka bayana ya kwamba tuwe makini, ili kuondokana  na matumaini ya uongo wa dunia hii inayotuandalia na kufunika yale yenye kuwa na mafao na kutonesha tu yale yasiyo kuwa na busara.Maandiko matakatifu yanatuonesha hayo kwa njia tofauti , lengo lake ni kututaka tupinge uongo wa miungu ambayo daima inazidi kumsonga na kumshawishi binadamu aondokane na  matuamaini hayo  na kumfanya kuwa kitu kitu cha matumaini.

Papa anasema zaidi ya hayo manabii walikuwa wakisisitiza  hilo na waligusia   sehemu nyeti ya safari mwamini.Kuwa na imani ni kile kitendo cha kuamini Mungu na hiyo inajitokeza zaidi unapokumbana na matatizo ya maisha,Papa aliendelea kusema “ binadamu anafanya uzoefu wa udhaifu wa imani na ndipo anahisi kuwa na  mahaitaji ya kuwa na uhakika wa aina mbalimbali na hasa ya kuwa na usalama wa aina yake na  kwa dhati.
Papa alisema Zaburi ya hekima inatusukuma kwa namna ya pekee  kutambua miungu ya dunia hii ambayo binadamu amekuwa akitegemea na kutumainia.

Zaburi hiyo ni ya 115 inayosema: Miungu yao ni ya fedha na dhahabu;imetengenezwa kwa mikono ya wanadamu. 5) Ina vinywa, lakini haisemi.Ina macho, lakini haioni. 6) Ina masikio, lakini haisikii.Ina pua, lakini hainusi. 7) Ina mikono, lakini haipapasi.Ina miguu, lakini haitembei.Haiwezi kamwe kutoa sauti. 8) Wote wanaoitengeneza wanafanana nayo,kadhalika na wote wanao tumainia. Mzaburi huyo anatuonesha kidogo kwa namna ya matani , lakini kiukweli  ni  hali halisi ya miungu .Na tunapaswa kutambua kweli siyo sanamu  zinazo husu shaba au vifaa vingine bali ni  miungu hata inayotengenezwa na akili zetu,  hasa tunapo itegemea kabisa  na kutubadilisha, na kwasababu hiyo ni dhahili ina onekana na tunafananishwa kabisa na  miungu hiyo inayotajwa katika zaburi.

Binadamu ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu lakini anatengeneza miungu wa sura yake, ndiyo  ni sura” Papa alisema , na kuongeza “lakini ni mfano  ambao haukufanikiwa , kwasababu haisikii , haifanyi kazi , na zaidi haiwezi hata kuongea. ”Ni Katika matumaini ya  Bwana wa maisha aliyeumba ulimwengu kwa Neno lake” Papa anasisitiza, "Mungu Bwana anaendelea kulinda maisha, bali anapingana na matumaini ya sanamu bubu. Kwa sababu fikra za kujiona  zaidi, kupenda  utajiri na  madaraka, kupenda mafanikio ,kujifikiria  wewe ndiye tu wa umilele, kutamani thamani ya uzuri wa maumbile uzuri na afya, vitu hivyo vikigeuka kuwa miungu hata ya kujitoa  nafsi yako  kwa gharama zozote zile ,kwa dhati ni mambo yanayo changanya akili  na moyo badala ya kukuwezesha  uwe na maisha ambayo baadaye yatakupeleke katika kifo.

Zaburi hiyo iko wazi Papa alisema , ”kwani  inakualika usiwe na  matumaini katika miungu, kwani utageuka kama miungu hiyo , sura zenye mikono mitupu ambayo haigusi, miguu isiyotembea , midomo ambayo haiwezi kuongea.hakna chochote ambacho unaweza kusema  kwani huna uwezo wa kusaidia, kuandaa mambo, kucheka, kutoa, au na kupenda. Pamoja na hayo mafundisho papa alisema kuwa “Hata sisi binadamu wa Kanisa, tunabiliwa na  kuathirika , hasa tunaoingia katika “malimwengu”. Tunapaswa kubaki katika ulimwengu, na kuutetea dhidi ya udanganyifu wa Ulimwengu. Kama inavyoendelea  Zaburi , tunapaswa kutumaini na kuamini Mungu mtoa  baraka:Israel, mtumaini Bwana (…) Enyi mlango wa Haruni , mtumaini Bwana ; Yeye ni msaada wao na ngao yao. 12  Bwana ametukumbuka, Naye atatubariki sisi. Ataubariki mlango wa Israeli, Ataubariki mlango wa Haruni,(115 . 9.10.11.12).

Papa alimalizia katekesi yake akisema  “hiyo ndiyo hali halisi ya matumaini.Ukimwamini Bwana unageuka kuwa kama yeye, na kutubadili tuwe watoto wake, tunao shiriki maisha yake. Matumaini  kwa Bwana , yanatufanya tuingie katika mwanga wa matendo ya kumbukumbu yake, ambapo  tunabarikiwa na kuokoka. Kwa njia hiyo tunaweza kuimba kwa furaha aleluya , utukufu kwa Mungu aliye hai kweli, na ambaye alizaliwa na Bikira Maria , aliteswa, akafa na kufufuka kwa wafu katika utukufu.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.