2017-01-06 14:17:00

Madaraja ya mshikamano kati ya nchi ya Italia, Camerun na Syria


Madaraja ya mshikamano kati ya Italia, Camerun na Syria kufanywa na vyama mbalimbali visivyo vya kiserikali kwaajili ya kumsaidia mwanadamu wa sasa anaye endelea kuteseka na hali ya maisha, na vyama hivyo ni kama ifuatavyo:Chama cha Patrizio Paoletti kwa ushirikiana na New Life for Children na Amal kwaajili ya Elimu wamezindua mradi wa Elimu katika eneo la Kills , kwenye mpaka wa Uturuki na Syria.Mradi huo umepokea watoto karibia 45,000 wakiwa wanakimbia kutoka eneo la Aleppo.


Kazi ya wanachama hao wamejikita katika mitaala ya shule katika ulimwengu, na lengo lao ni kutoa msaada wa vifaa vya ufundishaji kwa elimu na kwa wahudumu wa kituo  cha elimu “Bayt Al Amal””maana yake nyumba ya matumaini. Utaratibu huo ulioundwa na Amal kwa Elimu, kwaajili ya kuwasaida watoto na watu wazima wakimbizi wa Syria waweze kuwa  na kutuo cha maisha ya kijamii na elimu.
Hayo yalielezwa na mhusika mkuu wa Chama cha Paoletti, Bwana Marco Benini juu ya dhamira ya  miradi na mipango ya kijamii inayofanywa na vyama hivyo.

AFRIKA
Tukigeukia sehemu ya pili ya ni kwa upande wa Afrika ,  mahali ambapo inasemekana “ kuwa na mtoto mlemavu ndani ya familia ni kama vile umeadhibiwa na walemavu hao hawana maisha mema ya baadaye kwasababu ya kubaguliwa au kutelekezwa.Hayo ni maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa shirika la kutoa huduma lisilo la kiserikali la DOKITA ,Bwana Mario Greco akisema; lakini pamoja na hayo vituo vya afya vyenye uwezo wa kusaidia watoto wenye mahitaji maalumu , ki ukweli ni vichache sana na vinagharimu sana.Pamoja na kugharimu,bado kuna sababu nyingine ambayo mara kwa mara familia nyingi nazo zinachangia zenyewe kuwaondoa au kuwaficha watoto walemavu , kwa kasumba ya utamaduni wa kuwazia kwamba watoto  hao wamelaaniwa mbinguni  au kwasababu ya rasilimali za kiiuchumi kuwa ndogo.

Camerun ni moja ya nchi za Afrika inayosemekana kwamba kuna matukio mengi ya ulemavu  kwa watoto,ni asilimia 23% ya wenye umri kati ya miaka 2 na 9 wanaishi na mmoja akiwa na ukosefu wa akilli, na mara nyingi imetokana na magonjwa kama vile malaria , ukoma , surua  na  zaidi kinachodhofisha ni utapiamlo.


Ili kutoa jibu halisi  la ukosefu wa huduma za afya kwa watoto walemavu na yatima , Huko  Kusini mwa Camerun  , ni zaidi ya miaka 35 , shirika la kutoa huduma ya kibinadamu isiyo ya kiserikali  DOKITA ilianzisha vituo kadhaa maalumu. Kati ya hivyo ni “Foyer de l’Esperance, a Sangmelima”, ni mashirika ambayo  kila mwaka wanatoa huduma ya matibabu na mazoezi ya watoto walemavu wapate kupona na pia pia huduma ya ukaribu wao kwani  ni zaidi ya watoto 6,000 na vijana wenye ulemavu.
Muhusika  Sista Laura Figueroe , mmisionari wa shirika la watoto wa mama Maria mkinngiwa wa dhamabi ya Asili akiwa pamoja na shirika la DOKITA ni kitovu cha maisha kwa mamia elfu ya watoto” maalum”

Ili kusaidia  huduma ya mtawa Laura na "Foyer e L’esperance", tangu tarehe 8 hadi 28 Januari 2017 , Shirika lisilo  la kiserikali la Dokita limezindua Kampeni iitwayo  “Wote ni sawa”.Ni kwa kutuma fedha   kwa  njia  ya ujumbe wa sms kwenye namba ya mshikamano 45519 ,fedha zitakazo kusanywa zitatumika  kununua vifaa vipya kwaajili ya tiba ya viungo vya mwili , na kwaajili ya kufunga maabara.Michango hiyo pia itasaidia katika mtaala wa elimu na hasa kwaajili ya elimu ya msingi kwa watoto wenye kuwa na mahitaji maalum na kwa miradi mbalimbali ya kuendeleza  jamii, kiuchumi , kutamaduni kwa vijana wanye ulemavu.

 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.