2017-01-04 14:54:00

Kanisa la Ethiopia kupinga ukeketejaji wa wasichana


Inabidi kupambana dhidi ya ukeketeji wa viungo vya kike  kwa njia kuwafundisha, hayo yalisemwa hivi karibuni na Baraza la maaskofu kitengo cha  jamii na maendeleo ya Kanisa Katoliki la Ethiopia wakati wa semina yao  iliyofanyika mji Mkuu Addis Abeba ikiwa inawalenga hasa wakuu wa mashule na walimu.

 

Kwa mujibu wa shirika la Habari la Canaa , linalipoti ya kwamba wakati wa semina hiyo ,walipata kelelezo kikuu kinahosababisha  ukeketaji huo wa viungo vya wasichana na kuendelea kuwasukuma  hao kukubali ukeketaji huo ya kwamba  “ni matunda ya kasumba potofu inayowafanya wabaki na hofu ya kwamba wasipofanya hivyo hawastahili katika ndoa licha ya kutambua hathari zilizopo za ukeketaji.

 
Kwa mtazamo huo , katika semina walibaniisha njia inayoweza kutumika ambayo ni elimu, na hivyo walitoa wito hasa katika mashule ya  kikatoliki kuanza utekelezaji wa kupambana na ukeketaji huo kwa wasichana, kwa kuweka mpango huo ndani ya mtahala wa shule, wakiwahusisha moja kwa moja wanafunzi na wazazi wao. Lengo la kufanya hivyo ni kuongeza utambuzi na ufasaha wa tatizo hilo katika jamii.  Na ikumbukwe katika nchi ya Ethiopia, ukeketeji haurusiwi na ipo adhabu ya kisheria, pamoja na hiyo bado kasumba hizo zinafuatwa  hasa  katika maeneo ya Eparchia ya  Emdeber ambapo inahesabika kiasi kikubwa cha matukio hayo.


Hata hivyo semina iliyofanyika kwasabubu hiyo  ,siyo semina ya kwanza na wala siyo wito wa kwanza kwa Kanisa Katoliki la Ethiopia kupambana dhidi ya ukeketaji wa viungo vya kike, bali hata Februari 2013 , maaskofu hao kwa pamoja walipinga vikali juu ya jamabo hilo, wakisema jamabo hilo halina msingi wa kidini nana kuwaomba wawasaidie waathirika namana inavyostahili.

 

Sr Angela Rwezaula. 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.